Naomba ufafanuzi kuhusu hili la kuagiza vitu kutoka nje ya Tanzania

issaramadhani

Member
Jan 29, 2017
14
4
Msaada jamani nahitaj kuagiza Kifaa flan hv kidogo kutoka China ila kuna mtu alinambia lazima niwe na S.L.P yangu ili mzigo wangu ufike hapo. Sasa mimi sina hiyo S.L.P na nahitaj kuagiza. Je, mzigo wangu ntaupata vip? Msaada wana JF
 
Siyo lazima uwe na S.L.P yako.Wewe cha kufanya agiza halafu mzigo ukifika posta makao makuu ya Dar utapigiwa simu.Cha msingi jaza namba yako ya simu kwa usahihi kabisa na huo mzigo hakikisha kuwa una track number.
 
Unaagiza kwa kampuni, mtu binafsi agent au wewe peke yako? Tuanzie hapa kwanza.

Suala la S.L.P sio tabu maana unaweza kuingia makubaliano na mtu au taasisi/kampuni ukatumia S.L.P yao mzigo ukatumwa kwa anuani yao wakakupatia.
 
Unaagiza kwa kampuni, mtu binafsi agent au wewe peke yako? Tuanzie hapa kwanza.

Suala la S.L.P sio tabu maana unaweza kuingia makubaliano na mtu au taasisi/kampuni ukatumia S.L.P yao mzigo ukatumwa kwa anuani yao wakakupatia
Naagiza Alibaba kaka
 
Back
Top Bottom