BekaNurdin
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 2,267
- 2,041
Ndugu wana jamvi, salaam.
Kuna mahali (kijijini) nimepita nikaona kwa mbali umati umekusanyika bila wasiwasi, nikadokezwa kuwa inauzwa nyama ya nyati mahali pale. Ndipo nilipochukua hatua kusogea mahali pale ili nami niambulie japo kidogo. Waliponiona shughuli ya kuuza ikasimama kwa muda kwani walinitambua mimi si mwenyeji wa eneo lile kwahiyo wakawa na wasiwasi pengine nisije nikawatia matatizoni. Walipogundua kuwa mimi siyo mtu hatari kwao (sijui walijuaje!) wakanikaribisha na biashara ikaendelea. Kitoweo kile kilinunuliwa na watu wote bila kujali itikadi za dini. Nauliza hivi, nyati anachinjwa na nani? Anachinjwaje? Mwongozo wa dini gani unafuatwa wakati wa uchinjaji?