Naomba mtoe tip kwa wahudumu


Hata huyo aliyekuzidishia alizidiwa na ukali wa maisha ndo maana alifanya hivo. Imagine hana chanzo kingine cha kipato na muda wake mwingi anautumia pale na akitoka amechoka anaenda kulala, aaamke arudi tena shift ifuatayo?
 
Nilienda kwenye bar ya mshkaji wangu japo sinywi pombe kama safari kili castle hazishuki kabisa naona chungu sana, nikaagiza robertson ndogo na coke ninywe nikimsubiri na muhudumu hanijui basi nimekunywa mpka ikakata mwamba hajafika nikaomba bill yangu nikaletewa 40k nikauliza imekaaje hii muhudumu akanijibu kirahisi ndio bei yake.
sawa nikalipa mwamba akaja akataka kulipia nikamwambia tayari nimelipa,kibaya jamaa akamwambia muhudumu arudishe hela atalipa tulimaliza maongezi bas demu akarudisha 20k ikabidi nimuulize hiyo 20k nyingine imelipia nn mwamba aliwaka pale pale akavuta uzi kwa muhudumu mwingine yule dem kibarua kikaota nyasi fasta nilijiskia vibaya ila sio siri alikua anajifaidisha na kuharibu biashara ya mshkaji.

Kweli maslahi ya wahudumu yanatakiwa yazingatiwe ila wanazingua pale wanapoamua kuharibu biashara inaumiza sio siri
 

Hali ngumu inampelekea mtu kuwa mwizi! Huo kweli ni wizi hata mi siungi mkono kuzidishiwa bei au bill! Juzi kati nimeenda kunywa sehemu, nimepiga zangu vyombo naomba bill yule kazidisha hela. Nikamuuliza hii imekaaje? Mara ooh, mara ooh, nikamchana pale pale. Dada mara mia uniombe lakini sio kufanya hivi. Mnaboa sana wahudumu. Nikapita hivi
 
Me nmeshindwa kusoma
 
Sisi tunaopata huduma kwenye vyombo vya usafiri sasa
 
Binafsi mimi nikitoka out lazima nimpe mhudumu tip na nitawaeleza faida yake. Kwanza unatengeneza mahusiano ya customer service, kuna baa maarufu Dar nikiendaga yaani yule mhudumu akiniona napata service nzuri sana. Yaani kama mm mtu wa kunywa JD sijui barafu zimekata utakuta kila saa anapita kuhakikisha niko poa. Mhudumu siku nyingine labda nimekuja na wana tuko kinyonge tunaweza mtuma akatuletea pisi pale pale. Kuna siku ndio nilikuja kuamini bwana hawa wahudumu wanajua watu. Tulikaa mahali masela kama kawa tunakunywa na kucheki game. Akaja mbaba wa makamo hivi ku join meza huku akiwa anaongea sana trying to blend with the squad. Sasa mm nikatoka kwenda washroom yule mhudumu akanidaka akaniambia yule jamaa ni shushu so tuwe makini na vitu tunavyoongea mbele yake. Aisee na vile sisi tulikuwa UKAWA damu ikabidi nitonye wana. Ni mengi naweza adisia ila ukiwa mtu wa bar jaribu kujenga hayo mahusiano, ila usije ukamla [emoji23][emoji23]
 

Kweli kabisa! Ukimla tu umeharibu mahusiano. Anaanza kuleta wivu usionamaaana wakati wewe ni mpita njia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…