Naomba Msaada wa BitLocker Recovery

SaidAlly

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
2,374
Reaction score
2,312
Mkolon and tcoal9

Salaam wakuu na wengineo ambao watakua na utaalam wa tatizo langu.

Nina externa Hard disk, kila ninapoiweka kwa laptop inadai BitLocker password.
Nimehangaika sana katika net kutafuta solution sijapata zaidi ya kutakiwa either niwe na hiyo password au Password ID recovery key.

Kwa kumbukumbu zangu sijawahi ku-activate hiyo BitLocker na ilijitokeza baada ya rafiki yangu kuichukua ili akacopy movies na alipoiweka kwa pc yake ikamdai password, since then hata nilipoiweka tena kwa laptop yangu ikaanza kudai hiyo password. Nimejaribu njia nyingi za kui-disable hiyo BitLocker lakini kwa hiyo hard disk inataka password kwanza niifungue.

Sasa hata sijajua chanzo cha hilo tatizo maana mie sijawahi ku-activete hiyo kitu. Mie natumia window 7, nikiiweka kwenye window nyingine kama vista inanidai software ya ku-install hiyo hard disk.

Naomba msaada kwa anaefaham solution ya hii kitu!

Natanguliza shukrani!
 
BitLocker ni software ya encryption ya Microsoft ambayo inakuja na baadhi ya version za Windows, kuwasha Bitlocker kwenye external drive (BitLocker To Go) ni tendo la makusudi na haiwezi kujiwasha yenyewe, so ni wewe au mtu mwengine amewasha hiyo BitLocker, kama hiyo PC na HD ni second hand pia fikiria hilo.

Hakuna njia ya "kuizima" BitLocker bila ya kuwa na password au recovery key, software hii ingepoteza maana yake yote kama hilo lingekuwa linawezekana. Kama hauna pass au key basi data zako zimepotea, unaweza kuformat HD na kuanza upya.

Kama wakati wa kuwasha BitLocker mtumiaji alitengeneza Recovery key basi inaweza kuwepo kwenye PC. Tafuta text file zote, pia nenda search (Windows + F) andika BitLocker Recovery Key hii itatafuta file zote zenye hayo maneno, key inafanana na hivi
 
Kang and Livanga!

Asanteni!

Ngoja nijaribu then ntawajulisha matokeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…