Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,645
- 6,468
Anza biashara ya kuuza vocha(za kurusha)Niende moja kwa moja kwenye mada,
Wakuu ipo hivi kuna hela nimetumiwa hapa kiasi cha shilingi elfu tisini na nane (98,000).Lakini mtumaji aliye nitumia hiyo hela sijui kajichanganya vipi bhana badala aitume kwenye M-pesa yeye kaituma kama salio la kawaida kama mnavyo ona hapo chini kwenye picha [emoji116][emoji116][emoji116].
Hivyo wakuu naombeni msaada wenu hii hela naitoaje umu nimewapigia vodacom wameniambia hawawezi kuirudisha kwenye M-pesa. Hivyo nimeona nije kwenu wakuu mnipe ushauri wenu. View attachment 1252198
Jiunge kifurushi cha 98375....Utakuwa mteja wao mzuri kweli.
Kama wamekataa basi hakuna namna endelea Kula bando mpaka iishe na Kama unakibanda au mtu umwaminiye mpe awe anakurushia vifurushi mpaka iishe akukabidhi keshi.
Duh! Hiyo elfu 98 mpaka ije iishe ni leo mkuu mbaya zaidi hiyo biashara sijawahi fanya.Anza biashara ya kuuza vocha(za kurusha)
Hamna namna. Watangazie watu wa karibu, kazini nyumbani etcDuh! Hiyo elfu 98 mpaka ije iishe ni leo mkuu mbaya zaidi hiyo biashara sijawahi fanya.
Hongera sana mkuu kwa kumaliza mwaka vizuri, naamini hakuna kitakacho kupita JF
Hamna namna. Watangazie watu wa karibu, kazini nyumbani etc
Asante sana mkuuIlishawahi kunitokea. Nilinunua laki badala ya ten.
Nilichokifanya niliongea na wadau nikawapa ofa ya kuwapatia vocha ya Tsh. 10,000 kwa malipo ya 9000.
Nilifanikiwa kuokoamo Tsh. 81,000 + Vocha ya ten.. Elfu tisa ikaenda na maji.
Pole sana mdau.
Mkuu, hiyo unamuambia aliyekutumia hiyo hela airudishe, inarudi kwenye akaunti yake kisha anatuma tena
Transaction yoyote inaweza kuwa reversedMmh! Itawezekana kweli hii mkuu maana imekuja kama vocha
Hii mbinu voda wenyewe watakua hawaijui eeehMkuu, hiyo unamuambia aliyekutumia hiyo hela airudishe, inarudi kwenye akaunti yake kisha anatuma tena