Jinsi ya kutengeneza kashata

Vipimo:

Karanga - Kilo

Sukari - 5 vikombe

Maji - 2 vikombe

Maziwa ya unga - 2 vijiko vya chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Saga karanga zilizokaangwa na kumenywa mpaka zilainike kiasi.Kisha changanya maji na sukari weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo kama shira. Changanya unga wa karanga na maziwa ya unga kisha mimina kwenye hiyo shira.Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata.Paka mafuta treya kisha mimina na utandaze upesi upesi.Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha ipoe kabisa.Panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa pamoja na kahawa.
 
Habarin wana jamii forum poleni na majukumu

Mimi ni kijana wa chuo mjasiriamali ninahusika na uuzaji karanga za mayai na za kawaida kwa bei ya jumla .Nimekaa nikafikiria nikaona niongeze biashara nyingine yakutengeneza kashata za karanga na kuuza bei ya jumla

Ila nilikua naomba mnielekeze jinsi yakutengeneza kashata za karanga sababu nimefwatilia video YouTube nasijaelewa ila nimepata kamwongozo kadogo ambacho nikuziandaa karanga tu naombeni msaada.

Asanteni
 
Vipimo: anza na karangu nusu na sukari nusu,iliki km punje Saba HV zinatosha kuleta kaharufu kazuri. kwanza zitoe uchafu karanga zako pili zikaange bila mafuta mpaka uzione zmekuwa kavu...zitoe maganda zote! ukimaliza zitwange sanaa kwenye kinu mpaka uone zinatoa mafuta! Baada ya hapo chukua maji kiasi cha nusu lita bandika jikoni, tia na ile iliki (uitwange). Acha sukar ichemkeeeee sanaaaa impaka iive...utajuaje km imeiva? ukiishika na vidole viwili utaona inanata! au ukichukua mwiko ukifanya km unairudishia kwenye sufuria utaiona ni nzito unavutana! hapo utatia zile karanga zako ulizotwanga! utakorogaa bila kuachia mkono! ukiicha sekunde tu unaungua chini! utakoroga mpaka utakapoona imekuwa nzito utaimimina kwenye sinia ulilolipaka mafuta kidogo! utaicha mpaka ipoepoe utaanza kukata na kisu kikali shape unayopenda! ukipika mara kwa mara utagundua utakapokosea! pika nusu nusu mpaka utakapokuwa mtaalam utapika nyingi..kila la kheri
 
Shukran ubarikiwe
 
Back
Top Bottom