Jinsi ya kutengeneza kashata

Mawaiba

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
417
151
Habari za wiki end wakuu.

Kama nitakuwa nimekosea katika kuziita 'kashata za ubuyu', basi naomba mnielewe nichomaanisha. Nasikia huwa zinatengenezwa kwa kutumia unga wa ubuyu, huwa watoto wanazipenda. Shida yangu nikuomba kama kuna anaejua jinsi ya kuzitengeneza anijuze, yaani mchanganyiko wake unakuwaje na hatua ya kuzifanya mpaka ziwe tayari kwa kuliwa.

Asanteni sana.

Coconut burfi- kashata za nazi....

Mahitaji...
Nazi iliokunwa......
Maziwa (vizuri ukitumia maziwa ya sona ya kikopo ni nzuri zaidi)....
Hiliki ya unga....
Siagi kidogo sana kama kijiko kimoja cha chakula.....

Namna ya kutaarisha....

1)katika pan weka siagi isubiri ipate moto kidogo
2)weka nazi iliokunwa changanya vizuri alafu mimina maziwa pamoja na hiliki..
3)changanya vizuri hadi ichanganyike alafu epua...
4)tandandaza katika sahani na weka alama za kukata kabisa
5)weka katika friji ili kashata zishikane
6)kata tayar kwa kuliwaa...
Kashata zinapendeza kula na kahawa....

KASHATA ZA MAYAI

Mahitaji:
1. Sukari nusu kg,
2. Samli (aseel ) nusu kg,
3. Mayai 15 mpaka 16,
4. Maziwa mazito ya sona,
5. Iliki kijiko kimoja cha chai,
6. Arki ya vanilla Na rose kijiko kimoja chai.

Namna ya kupika:
Yeyusha samli yako iwe liquid, iache ipoe kdg isiwe moto sana. Then kwenye bakuli safi weka samli yako, sukari Na mayai yako. Piga au changanya kwa mchapo mpaka vichanganyike vizuri. Then minina mchanganyiko wako kwenye sufuria ya kiasi ambayo haitokupa tabu kukoroga then weka kwenye jiko lako kwa ajili ya kuanza mapishi. Moto usiwe mkali sana wala mdogo sana.

Anza kukoroga kwa mwiko usiachie mkono ili isigande kwenye sufuria au kuungua kabla kuwiva.

Endelea kukoroga itaanza kuwa nzito kama crumble eggs, Endelea kukoroga itaanza kubadilika rangi taratibu from white to brown light. Ikianza kuwa brown light weka iliki Na arki zako huku bado unaendelea kukoroga.

Ikianza kukoza brown minina maziwa ya sona kiasi nusu kikopo. Then koroga koroga kdg tu kiasi maziwa yachanganyike then epua.

NB: maziwa ya sona unaweka karibia kuepua)
Vile vile usiache kuwa brown dark itakuwa haina test nzuri.

Tunaendelea: ukisha epua sufuria mimina mchanganyiko wako kwenye sinia ya kiasi yenye nafasi nzuri. Unapomimina, mimina upande mmoja kwa sababu samli huwa inabaki nyingi so utapata kuinua sinia yako upande Na kuitoa samli yote. Ukiacha sinia ikalala Kashata zako zitakua Na samli nyingi Na zitakuwa Si nzuri. Kata kata kashata zako vi square wakati bado haijapoa.

Iegemeze sinia yako sehemu ili samli itiririke upande mmoja Upate uitoe kwa kijiko.

Ukisha hakikisha samli haiteremki tena laza sinia yako usubiri kashata zigande. Inachukua masaa kadhaa kuganda so make sure huzibandui kashata mpaka zigande vizuri.

Zikisha kuganda vizuri bandua uweke kwenye bakuli zipate kuhifadhika vizuri. Kashata zako tayari, Ni nzuri kula kwa gahwa.

Eid Mubarak

KASHATA ZA UFUTA
Jinsi ya kuandaa
. Osha vizuri ufuta kisha anika juani ukauke
. Weka sufuria jikoni, kisha weka sukari ndani ya sufuria, acha sukari ichemke hadi iwe kama inayeyuka
. Mimina ufuta ndani ya hiyo sukari, vichanganye hadi vichanganyikane kabisa
. Unatoa kidogo kidogo unatengeza shape ya duara kwa kuvibumba mkononi
Kashata zipo ready
 
Hizo hata mm sijawahi. Ila najua kashata aina nyingi hupikwa kwa kutengeneza shira. Basi jaribu na huo unga wa ubuyu labda zawezawekwa na tangawizi pia. Try kidogo uone inakuwaje....wanasema practice makes perfect
 
eeh! ushaona njaa haya "kalaga baho"

Wapo pro cooks humu, ulishawahi kuona tangazo kama lako hata siku moja?!!!! kama pishi unalijua wewe inakugharimu nini kumwekea mtu akajifunza, kila kitu pesa pesa pesa...ukiendekeza njaa utakosa mengi! maxence angeendekeza njaa unafikiri angeruhusu mtu kuingia bure jf, unaingia bure na kupost vinamba vyako vya simu public kwa sababy kuna watu hawakuendekeza njaa! Kama uko deliberate hebu weka hiyo recipe kisha andika pale chini "I'M BROKE PLEASE DONATE" utaona utarushiwa hata zaidi ya ulichokuwa unategemea!
 
Wapo pro cooks humu, ulishawahi kuona tangazo kama lako hata siku moja?!!!! kama pishi unalijua wewe inakugharimu nini kumwekea mtu akajifunza, kila kitu pesa pesa pesa...ukiendekeza njaa utakosa mengi! maxence angeendekeza njaa unafikiri angeruhusu mtu kuingia bure jf, unaingia bure na kupost vinamba vyako vya simu public kwa sababy kuna watu hawakuendekeza njaa! Kama uko deliberate hebu weka hiyo recipe kisha andika pale chini "I BROKE PLEASE DONATE" utaona utarushiwa hata zaidi ya ulichokuwa unategemea!

nimekuelewa mkuu.
 
Kwa anayejua kutengeneza kashata za Nazi anielekeze jamani.Nilishawahi kutengeneza ila hazikuwa ngumu sijui nilikosea wapi?
 
Coconut burfi- kashata za nazi....

Mahitaji...

Nazi iliokunwa......

Maziwa (vizuri ukitumia maziwa ya sona ya kikopo ni nzuri zaidi)....

Hiliki ya unga....

Siagi kidogo sana kama kijiko kimoja cha chakula.....

Namna ya kutaarisha....

1)katika pan weka siagi isubiri ipate moto kidogo

2)weka nazi iliokunwa changanya vizuri alafu mimina maziwa pamoja na hiliki..

3)changanya vizuri hadi ichanganyike alafu epua...

4)tandandaza katika sahani na weka alama za kukata kabisa

5)weka katika friji ili kashata zishikane

6)kata tayar kwa kuliwaa...

Kashata zinapendeza kula na kahawa....
 
Coconut burfi- kashata za nazi....

Mahitaji...

Nazi iliokunwa......

Maziwa (vizuri ukitumia maziwa ya sona ya kikopo ni nzuri zaidi)....

Hiliki ya unga....

Siagi kidogo sana kama kijiko kimoja cha chakula.....

Namna ya kutaarisha....

1)katika pan weka siagi isubiri ipate moto kidogo

2)weka nazi iliokunwa changanya vizuri alafu mimina maziwa pamoja na hiliki..

3)changanya vizuri hadi ichanganyike alafu epua...

4)tandandaza katika sahani na weka alama za kukata kabisa

5)weka katika friji ili kashata zishikane

6)kata tayar kwa kuliwaa...

Kashata zinapendeza kula na kahawa....

Shukrani sana Mamie na kama naongeza sukari naiweka wakati gani?Na kwenye friji naziweka kwa muda gani?

Usinichoke shosti yangu.
 
Mahitaji:

1. Sukari nusu kg,

2. Samli (aseel ) nusu kg,

3. Mayai 15 mpaka 16,

4. Maziwa mazito ya sona,

5. Iliki kijiko kimoja cha chai,

6. Arki ya vanilla Na rose kijiko kimoja chai.

Namna ya kupika:

Yeyusha samli yako iwe liquid, iache ipoe kdg isiwe moto sana. Then kwenye bakuli safi weka samli yako, sukari Na mayai yako. Piga au changanya kwa mchapo mpaka vichanganyike vizuri. Then minina mchanganyiko wako kwenye sufuria ya kiasi ambayo haitokupa tabu kukoroga then weka kwenye jiko lako kwa ajili ya kuanza mapishi. Moto usiwe mkali sana wala mdogo sana.

Anza kukoroga kwa mwiko usiachie mkono ili isigande kwenye sufuria au kuungua kabla kuwiva.

Endelea kukoroga itaanza kuwa nzito kama crumble eggs, Endelea kukoroga itaanza kubadilika rangi taratibu from white to brown light. Ikianza kuwa brown light weka iliki Na arki zako huku bado unaendelea kukoroga.

Ikianza kukoza brown minina maziwa ya sona kiasi nusu kikopo. Then koroga koroga kdg tu kiasi maziwa yachanganyike then epua.

NB: maziwa ya sona unaweka karibia kuepua)

Vile vile usiache kuwa brown dark itakuwa haina test nzuri.

Tunaendelea: ukisha epua sufuria mimina mchanganyiko wako kwenye sinia ya kiasi yenye nafasi nzuri. Unapomimina, mimina upande mmoja kwa sababu samli huwa inabaki nyingi so utapata kuinua sinia yako upande Na kuitoa samli yote. Ukiacha sinia ikalala Kashata zako zitakua Na samli nyingi Na zitakuwa Si nzuri. Kata kata kashata zako vi square wakati bado haijapoa.

Iegemeze sinia yako sehemu ili samli itiririke upande mmoja Upate uitoe kwa kijiko.

Ukisha hakikisha samli haiteremki tena laza sinia yako usubiri kashata zigande. Inachukua masaa kadhaa kuganda so make sure huzibandui kashata mpaka zigande vizuri.

Zikisha kuganda vizuri bandua uweke kwenye bakuli zipate kuhifadhika vizuri. Kashata zako tayari, Ni nzuri kula kwa gahwa.

Eid Mubarak
 
Hi wana jf,msaada jinsi ya kutengeneza huu ubuyu usio na mapeke(mbegu)

========================
======================================

Zanzibar Spices said
Ni kwamba unachukua Unga wa Ubuyu, unachanganya na Rangi uipendayo,hizi rangi zinauzwa maduka tele hadi mitaani na ni kama rangi zile tu za kwenye Ice cream za mtaani za mia mia, then unaweka Sukari na kuuchanganya Unga wa Ubuyu hadi sukari iwe kwenye kiwango cha ladha unayoitaka.

Unaweka Maji kidogo kulingana na Kiwango cha uwiano wa Unga kama ulivyofanya kwenye michanganyo hapo juu.

Kisha unaupiga kama vile unakanda matofali vile,kwa muda kiasi hadi uwe Mgum na kukaza,then ukiisha kaza ndio unaanza kukata vipande unavyotaka kwa utulivu. Unaweza kuongeza na Spices zingine

Ila kama upo Dar,
Neda Kule kwa Somanga,ni maarufu sana Jiji la Dar kwa biashara hii.
Ni Babu wa Kisomali yupo pale Magomeni kama njia ya kwenda Tandale Uzuri, ukimaiza kituo cha Fundikira kifuatacho ndio kwa Somanga,hata mtoto mdogo ukimuambia atakupeleka.

Anauza Ubuyu wa Vanila,na pia anauza Unga wa ubuyu ambao tayari una rangi.
Wewe unanunua unachekecha,unatoa mizizi,then unaweka Sukari na kuanza kuupiga ili ujikaze na kisha kutaka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom