Ukitaka kujenga usipatane na fundi mmoja. Tafuta wengi wakupe quotation zao na kila mmoja mfahamishe atakaefikia bei ya chini ndiye utakae mpa kazi utapata majibu.
Wakati najenga kuna mafundi walifikia mpaka 5.5m msingi na boma. Uwezi amini nikapata fundi wa 2.5m na ni fundi nzuri sana. Nyumba vyumba 4, sebule, dining, jiko, store, vyoo public 2, mpaka nikashangaa kwa nini bei zinatofautiana sana.