Naomba makadirio ya gharama ya kumlipa fundi kuanzia msingi kuezeka kwa ramani hii

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,759
5,289
wakuu habarini...naomba msaada wa kujua garama ya kumlipa fundi ili anijengee nyumba kama hiyo pichani.

Vyumba viwili vidogo vidogo 3*3. Sebule yenye dining, choo kiwanja kipo, tofali 6500 za kuchoma zipo bati na vingine naendelea navyo mdogo mdogo..kwa sisi ambao hatuoa nadhani itanitosha hii.

Pia kama kuna maoni na ushauri nitafurahi wakubwa zangu.

Napenda kujua gharama ya fundi tu ni kama bei gani.

b341c482902d938ec7a6d4e2ebb05854.png
 
Gharama za ufundi inategemea na ulipo, mnaweza kulelewana kuanzia msingi hadi kukamilisha boma, cha kufanya watangazie kazi ili waombe na wakupe quotation zao, then chagua kulingana na vigezo vyako.
 
Kwa Morogoro lakini.
1. Msingi hadi kozi ya mwisho =1.7M
2. Kupaua au kuezeka =900,000

(Itategemeana na nguvu ya kupanga bei na fundi na fundi)
 
Gharama za ufundi inategemea na ulipo, mnaweza kulelewana kuanzia msingi hadi kukamilisha boma, cha kufanya watangazie kazi ili waombe na wakupe quotation zao, then chagua kulingana na vigezo vyako.
Sawa mkuu lakin kwa mfano isizid bei gani..kwa mkoa wowote ule kwa kupitia raman hiiyo
 
gharama ya ufundi isizidi 30% ya gharama ya material.

Pia jenga in stages, wabongo ukiwapa kazi kubwa wanajua unahela then watawaza kukupiga/kukuibia.

Anza na msingi, then ujenz mpaka kumaliza boma, then bati.

hata kama unacash, usijenge yoote kwa pamoja, na uwe unalia kweli kwa mafundi kuwa huna hela
 
Mimi fundi wa kwanza alitaka m 2, wa pili akatakata 1.5 m, wengine walitaka 900K so nikampa wa 900K na kazi kapiga nzuri tu, kupaua ni 400k japo wengi walitaka 450K, kikubwa waambie wazi kwamba mwenye bei nzuri ndo atapata kazi, maana hawa mafundi wetu wana bei zisizokuwa na uhalisia
 
Dah huko uliko mnajenga kwa bei poa. Huku moro wanatupiga aisee.
 
gharama ya ufundi isizidi 30% ya gharama ya material.
Pia jenga in stages, wabongo ukiwapa kazi kubwa wanajua unahela then watawaza kukupiga/kukuibia.
Anza na msingi, then ujenz mpaka kumaliza noma, then bati.
hata kama unacash, usijenge yoote kwa pamoja, na uwe unalia kweli kwa mafundi kuwa huna hela
Asante sana..ushaur mzuri sana huu
 
Back
Top Bottom