Naomba kuufahamu Mkoa wa dodoma Katika nyanja hizi.

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,055
Wakuu habari za majukumu ya kila siku.

Naombeni kufahamu mkoa wa dodoma katika sehemu hizi

1. kilimo.
Mazao gani yanalimwa mkoa huu. Ingekuwa vema utaje na wilaya linapolimwa zao hilo.
Wateja wa mazao hayo wanatoka wapi.

Upatikananji wa mashamba na umwagiliaji.

2. Ufugaji.
Wilaya zinazofuga kwa wingi. Aina ya ufugaji (movable au permanent settled)
Aina ya mifugo inayofuga.

Kama ni ng'ombe je wapi wanafuga ng'ombe wa maziwa, nyama, kawaida kwa wingi.

3. Viwanda vya usindikaji mazao shamba na mifugo.
Kuna viwanda vingapi vya nyama, maziwa na vingine vinavyotumia malighafi ya mazao shamba na wanyama.

Wateja wa kuu wa bizaa zinazozalishwa kutoka viwanda hivyo.

3. Maji
Upatikanaji wa maji katika wilaya zote za dodoma.
Vyanzo vya maji, na hali halisi ya maji yanavyopatikana hasa dodoma mjini.

4. Umeme
Upatikanaji wa umeme katika wilaya zote.
Hali ya kukatika umeme hapo dodoma mjini.

5. Gharama za chakula na malazi
Gharama ya chakula katika mkoa huo, namaanisha kwenye mgahawa(chakula cha kawaida, mgahawa wa kawaida)
Ghaharama za nyumba za kupanga dodoma mjini na wilaya nyingine.

6. Makabila na Tabia zao
Tabia ya wakazi wa dodoma mjini, kabila ambalo ni dominanti.
Hali ya kiuchumi ya watu wa dodoma mjini na pembeni za wilaya zinazozunguka dodoma mjini.

ukarimu wao upoje, wizi, ubaguzi na mambo mengine yanayohusu tabia.

Nihayo tu wanajukwaa, naomba hata kama unajua sehemu ya hivyo vipengelee unisaidiee.
 
Back
Top Bottom