Ndugu yangu kupata namba za simu ya Mh Rais ni kazi ngumu, kupata nafasi ya kuongea naye ni Ngumu zaidi.
Ninachokushauri, fuatilia ziara za Mh Rais katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Akifika katika mkoa wako, ninaamini atasimama na kusikiliza kero za wananchi kama ambavyo amekuwa akifanya. Nyoosha mkono na mweleze dukuduku lako. Atakusikiliza na atakusaidia.
Pili, kuna yule maza wa Mirathi alidai kuwa alishaongea na Mh Rais. Basi mtafute huenda ana namba za Mh ila ni ishu sana kuzipata, tupilia mbali kuongea naye.
Tatu, eleza dukuduku lako humu. Kwa inavyoonekana, Mh Rais huwa anatembelea humu na unaweza kubahatika akakusoma. Pia, kuna wateule wake wengi humu wenye nafasi ya kuongea naye hivyo watamfikishia ujumbe wake. Wapo pia wazee wa Kaunda suti, nao watakusaidia.
Nne, andika barua kisha uielekeze kwa Mh Rais. Japo ana majukumu mengi lakini huenda Shida yako ikatatuliwa.
Tano, jenga urafiki na Bashite Daudi. Jamaa huwa anampigia Mh Rais hata kwenye mikutano ya hadhara. Kwa hiyo naamini atakupa hata wewe nafasi ya kuongea naye.
Sita, nenda Clouds Fm. Redio pendwa ya Mkulu. Mwaga povu lako hapo. Tiririka na baada ya siku mbili tatu, Rais atakuwa kakusikia.
Saba, japokuwa najua bangi imepigwa marufuku fanya mbinu uipate. Vuta pafu kadhaa, shusha vitu. Kisha, kama alivyosema Kamishina wa Kupambana na Madawa ya kulevya kuwa inaleta Hallucination, utajikuta unaongea nae na umueleze shida yako.
NAKUTAKIA KILA LA KHERI.