Naomba kujua utaratibu wa ku-renew passport

Infopaedia

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
1,231
1,489
Habari za saahizi wakuu. Poleni na mjadala wa kipaumbele kipya (unga) cha taifa.
Nipo Mwanza na ninataka kuhuisha (renew) hati yangu ya kusafiria. Utaratibu unakuwaje, na gharama zake.
 
kwa taratibu za awali.. ilikuwa unajaza fomu na kupiga fingerprints na unaambatanisha na copies hitajika na picha na old passpt unalipia 50k
unawakabidhi uhamiaji.. baada ya siku kadhaa unapokea New book!!
 
Hawatumii details zako zilizopo kwenye data base yao?, Kama wafanyavyoTRA kwenye kuhuisha leseni ya udereva.
 
Pasport yangu ilipotea baada kuchanganyikiwa alipokufa mke wangu 2009, sikumbuki hata no yake wala copy yake sina. niliipata 2006 na ilikuwa inaishia 2016, hapa nikitaka kupata nyingine nitatumia utaratibu gani? nilikuwa sijawahi kusafiria.
 
Nadhani inabidi uende polisi ukatoe taarifa ya kupotelewa na hati ya kusafiria. Ukiwa na picha 2, na shilingi elfu mbili. Polisi watakupa barua ya kuonyesha umepotelewa na hati yako. Hiyo barua ndo utawasilisha uhamiaji ili zifanyike taratibu za kupata hati nyingine. Pale polisi kumbuka kwenda na chenji kamili ya elfu mbili.
 
Utaratibu ni uleule kama unavyoomba kwa mara ya kwanza.Kuanzia barua ya mtaa mpaka nwisho.....
 
Habari za saahizi wakuu. Poleni na mjadala wa kipaumbele kipya (unga) cha taifa.
Nipo Mwanza na ninataka kuhuisha (renew) hati yangu ya kusafiria. Utaratibu unakuwaje, na gharama zake.
Unatakiwa na kuwa na Pasipoti ya zamani halafu unakwenda ofisi ya Uhamiaji unajaza fomu za maombi na ku-attach picha nne za pasipoti na kuandika barua ya kuomba kubalishiwa pasi mpya kwa Kamishna Jenerali. Hakuna kingine zaidi ya kulipia na kuondoka ukisubiria pasi yako mpya. Mengine ni ushawishi wa kuvunja sheria
 
Back
Top Bottom