Naomba kujua PAYE ya mwenye mshahara wa Tsh.1,000,000/=

mughosia

Member
Jan 15, 2016
25
5
Jamani naomba anayejua paye ya mwenye mshahara wa approx Tsh.1000,000/=
Maana huku kijiweni tumebishana hadi makoo wamekauka....
 
Kanuni ni moja tu , hiyo toa kiasi unachokatatwa mfuko wa hifadhi ya jamii na bima ya afya. Jibu utakalopata toa laki saba na ishirini. Ukishapata jibu tafuta 30% ya hiyo tofauti, halafu mwisho jumlisha na 101,900 . Jibu utakalopata ndio kodi yako. Tuchukulie unakatwa 5% mfuko wa hifadhi sawa na 50,000 bima ya afya 3% sawa na 30,000. Jumla 80,000. 1000,000_80,000=920,000 . Kwa kuwa mshara wako unazidi 720000 utatoa na hyo. 920000_720000=200000. Tafuta 30% ya laki 2=60,000. Unajumlisha 60,000 +101,900= 161,900. Kodi yako ni 161,900/= (namshukuru mwl wangu wa finance dr. Thimoth wa irdp leo inanisaidia kuelekeza watu )
 
Sehemu nyingi za kazi wanakata 10% ya mshahara kama mchango wa mwajiriwa katika mfuko wa hifadhi ya jamii hivyo anaweza akaitumia hiyo formula uliompa kukokotoa, na pia PAYE inakokotolewa kutokana na kiasi kinachobaki baada ya kuondoa mchango huu wa hifadhi ya jamii tuu hamna makato mengine kma mf. Bima ya afya kama ulivyoweka hapo
 
Pspf mwajiriwa anakatwa 5% ila mashirika mengine ni hiyo uliyosema. Cha msingi amepata tu picha
 
Kanuni ni moja tu , hiyo toa kiasi unachokatatwa mfuko wa hifadhi ya jamii na bima ya afya. Jibu utakalopata toa laki saba na ishirini. Ukishapata jibu tafuta 30% ya hiyo tofauti, halafu mwisho jumlisha na 101,900 . Jibu utakalopata ndio kodi yako. Tuchukulie unakatwa 5% mfuko wa hifadhi sawa na 50,000 bima ya afya 3% sawa na 30,000. Jumla 80,000. 1000,000_80,000=920,000 . Kwa kuwa mshara wako unazidi 720000 utatoa na hyo. 920000_720000=200000. Tafuta 30% ya laki 2=60,000. Unajumlisha 60,000 +101,900= 161,900. Kodi yako ni 161,900/= (namshukuru mwl wangu wa finance dr. Thimoth wa irdp leo inanisaidia kuelekeza watu )
Hiyo Tshs.101,900/= ni ya kitu gani mdau?
 
Pspf mwajiriwa anakatwa 5% ila mashirika mengine ni hiyo uliyosema. Cha msingi amepata tu picha
Makato ya pension hayaangalii mfuko bali mwajiri....mwajiriwa wa serikali atakatwa 5% na serikali watachangia 15% while wa private mwajiriwa 10% mwajiri 10..otherwise kama mwajiri atamua kukukata 5%
 
Mwajiri ambaye ni serikali makato ya pension ni 5% kwa mwajiri na mwajiriwa 15%.
 
Kanuni ni moja tu , hiyo toa kiasi unachokatatwa mfuko wa hifadhi ya jamii na bima ya afya. Jibu utakalopata toa laki saba na ishirini. Ukishapata jibu tafuta 30% ya hiyo tofauti, halafu mwisho jumlisha na 101,900 . Jibu utakalopata ndio kodi yako. Tuchukulie unakatwa 5% mfuko wa hifadhi sawa na 50,000 bima ya afya 3% sawa na 30,000. Jumla 80,000. 1000,000_80,000=920,000 . Kwa kuwa mshara wako unazidi 720000 utatoa na hyo. 920000_720000=200000. Tafuta 30% ya laki 2=60,000. Unajumlisha 60,000 +101,900= 161,900. Kodi yako ni 161,900/= (namshukuru mwl wangu wa finance dr. Thimoth wa irdp leo inanisaidia kuelekeza watu )
iko kwenye finance au Accounts,maana nakumbuka niliisoma kwenye account 1 topic ya payroll account.
 
Kundi hilo la mshahara unaozidi laki 720 formula ni:
PAYE= 101,900 + 30% ya kiasi cha mshahara kinachozidi 720,000. So, hiyo ni fixed component kwenye hiyo formula ya kukokotoa kodi.
Safi mkuu hapa umerahisisha sana.
 
Nionavyo kumbe kuna uwezekano wa watu wawili wanaopata kiasi sawa cha mshahara wakawa wanakatwa kiasi tofauti cha PAYE. Nasema hivyo kwa sababu kwa mujibu wa taratibu kabla ya kupiga hesabu ya PAYE inabidi kwanza utoe michango ya mifuko ya jamii ambapo katika mifuko mingine mfanyakazi anachangia 10% na mingine 5%. Kwa hiyo kama mimi napata gross salary ya Tshs. 1,000,000/= na kama nachangia 10% kwenye mfuko wa jamii PAYE yangu itatoka kwenye 900,000/= wakati mwenzangu apatae gross salary sawa na ya yangu na kama anachangia 5% yeye PAYE itatoka kwenye 950,000/=. Sijui kama niko sawa hapo?
 
Back
Top Bottom