Habarini wapendwa,
Leo naomba kuongea na wale wenzetu mliokwisha kupata kazi; ni mbinu gani mumeweza kutumia hadi mkafanikiwa, maana mimi naona kwa upande wa ajira mambo bado magumu.
Nimezunguka kila sehemu nimefka kila mahali nimetuma maombi sehemu mbalimbali lakini bado sijafanikiwa. Sasa hivi mwaka wa 3 sasa tangu nihitimu chuo lakini bado na-hustle kutafuta kazi pasipo mafanikio.
Hebu dondosha mbinu moja wapo ambayo wewe ilikuwezesha kupata kazi pengine mimi au graduate mwenzangu anayepambana kusaka ajira inaweza kumsaidia.
5 years tangu ni graduate na still counting,, nimepiga interview kama tatu hivi zile za kiofficial acha hizi za mitaani na zote chali Utumishi-x, Ngorongoro-x, Tanapa-x
Eeh nikaona huu ungese sasa nikajiongeza kupata leseni ya udereva daraja C na ndiyo linalonilisha hapa saizi.
Driving imeanza tangu namaliza kidato cha 4- mpaka naingia chuo nilikuwa na leseni Daraja E C3 nilichofanya ni kujiongeza kusogea hapo C-kavuLeseni ya udereva daraja C plain si hadi uwe na zile c ndogo kama c1 zenye miaka mitatu.. je ulikuwa nazo
Sent using Jamii Forums mobile app
una maanishaaaa!!!!!!
Andaa CV yako iwekee manjonjo ya kufa mtu, mjanja kiasi jifunze vitu vya kukusaidia katika kazi na kuwa jasiri.
Baada ya hayo, kuna njia hizi hapa chini ibuka nazo sasa zitumie.
1. Tuma barua za maombi ofisi yoyote unayotaka kufanya kazi (usiombe kujitolea ktk mfumo huu). Chagua ofisi matawi na usiogope kupeleka barua yako ikiwa na wasifu wako.
2. Kaa chini anza kutafuta mabosi, HRs au Mameneja wa taasisi unayotaka kuomba kazi. Hakikisha unapata taarifa zao za kutosha pamoja na mawasiliano yao. Pata muda wasiliana nao kisha omba appointment nao. Ukifika kuwa jasiri na jifanye kweli kweli unamjua (si unazo taarifa zake) muombe ajira kibingwa hachomoi.
3. Unaweza andika barua ya kujitolea kwa taasisi ambayo inaonekana ngumu kuingilika mfano serikalini nk.
4. Omba kila kazi utakayoona inafaa kwako kwa kazi zilizotangazwa kwa kusoma vizuri mahitaji na hakikisha unaendana na sifa tajwa kuhusu hiyo kazi.
5. Tafuta washkaji (wadada masekretari wa maofisini) waaminifu tengeneza nao connection ya michongo ya kazi.
6. Tumia mitandao ya kijamii inasaidia.
7. Unaweza enda nje ya mji uliopo kwenye makampuni ukaomba kazi na ukapata.
Karibu.
Mwaka wa tatu unalia lia hvyo unatakiwa ukae atleast 5years ,kuna jamaangu alikaa 9 years bila kupata ajira.Habarini wapendwa,