Huu wangu ni ushauri tu kwa vijana wenzangu ambao bado tuna muda mrefu siku za usoni kuweza kufanya kazi/kuajiriwa!! Assume hivi sasa umeacha au kufukuzwa kazi au kitu chochote sawa na hayo! And, kwa sasa ni member wa NSSF huku ukisotea mafao yako na hujui utayapata lini.......!! In short, ktk hali ya kawaida, fao la kujitoa NSSF unaanza ku-claim after six months! So, kama utapata ajira sehemu nyingine, then fikiria haya yafuatayo:
1. Salary yako kwenye ajira mpya!
Hili ni muhimu sana kuangalia ili kufanya uamuzi wa busara ujiunge na mfuko gani. Kama mshahara wenyewe ndio hii mishahara yetu mingi ambayo, inapotokea kufukuzwa au kuacha kazi tu; basi on the same month unakua katika hali mbaya; basi ogopa NSSF kama ukoma! Unakuta mtu anapata basic ya TZS 600,000/=! Mtu kama huyu simtarajii kama anaweza kufanya savings ya kutosha itakayomwezesha ku-survive for six more months bila kazi. So, mtu kama huyu anapofukuzwa kazi ama mkataba wake kwisha, then kuna uwezekano mkubwa hayo yakamkuta wakati hata laki tano hana kwenye akiba yake!! Na unapoenda NSSF kuchukua chako, utaambiwa usubiri miezi sita wakati akiba uliyonayo ni ya kukuwezesha ku-survive mwezi mmoja! Na kumbuka, hiyo miezi sita ni kwa ajili ya kufungua madai, so cash money itaingia mkononi mwako at least seven months tangu utoke kazini! Kwahiyo, katika mazingira kama hayo basi iogope NSSF kama ukoma!
In contrast, kama salary yako inaweza kukuwezesha ku-save amount ya kutosha; kwamba at any given month, basi unaweza uka-save angalau TZS 300,000/=, then NSSF is best for you! WHY? In short ni kwamba, pale mkataba wako unapoisha au kufukuzwa basi kuna uwezekano ukawa umejiwekea akiba ya kutosha kidogo kukuwezesha ku-survive kwa miezi sita zaidi! Kuna uwezekano ukaja kupata mpunga wako wakati ndo unaanza kutaka ku-collapse na hivyo kuwa na additional months za kuweza ku-survive wakati unatafuta mchongo mwingine! Unless kama u've entrepreneurial ability, kujiunga mifuko inayotoa mafao mapema si busara endapo mshahara wako ni mzuri!! Sizani kama nimeeleweka....!! Assume mshahara wako ni mzuri to the point kwamba mkataba wako unaisha huku una akiba ya angalau TZS 2,000,000/= in your bank account. Na good enough, upo kwenye mfuko ambao unatoa mafao ya kujitoa kwa haraka zaidi; say within 3 months! Hii maana yake ni nini? Ni kwamba utalipwa mafao yako wakati bado una akiba ya kutosha. Ama kwa lugha nyepesi, badala ya mafao yako kuanza kuingia kwenye mkondo wa matumizi seven months after kuacha kazi(from NSSF), sasa mafao hayo yataingia kwenye mkondo wa matumizi only after three months! Hapo ni kwamba, hata kama ni kuashiwa basi utaishiwa mapema zaidi kwavile umechukua mpunga mapema zaidi!
BUT, kwavile mishahara mingi ni midogo sana, basi jambo la maana ni kuigopa NSSF!