Naomba kujibiwa maswali haya kuhusu safari ya Dar es Salaam to Botswana

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,887
3,349
Hujambo?
Karibu kwenye mjadala mawazo yako ni muhimu sana kwangu na pia naimani na wengine yanaweza kuwasaidia.

Mwezi wa 11 mwaka huu nimeamua nichukue likizo yangu ya mwaka,lakini pia likizo yangu hii nataka niitumie vema kutembelea nchi ya botswana.

Kwanini nimeamua kuitembelea nchi hii
1.Moja ya nchi ya afrika ambayo nilitamani tangu nikiwa mtoto kuitembelea achilia mbali S.A.

2.Watu wengi husema ni nchi ambayo inafursa na nimekuwa nikiona wabongo wengi wakienda huko na wakirudi mambo yao huwa yamenyooka.

3.Watu wanasema ni moja ya nchi yenye passport yenye nguvu afrika so mbotswana anaweza kuingia nchi 73 bila visa.
Na hapo ndio napataka kwani kunakitu nimekipanga baada ya miaka miwili ijayo kukifanya.

Sasa basi napenda nifahamu mengi kabla ya safari yangu kwa maana huko niendako sina mwenyeji yaani mwenyeji wangu ni pesa nitakayokuwa nimeiandaa.
Natamani kujua kabla ya safari ni vitu gani nihakikishe niwetayari ninavyo au nitegemee kukabiliana navyo nitakapofika botswana?.

Je ili tour yangu iwe njema niandae kiasi gani for go and return?.

Nauli kutoka DSM to botswana, go and return inagharimu kiasi kwa ndege na shirika gani zuri la ndege nitumie?.

Vitu gani vya kuviepuka nitakapofika Botswana?

Jiji gani zuri la kufikia ambalo lina mishemishe pia ambalo nitaweza kujifunza vitu vizuri vya kunijenga kimaendeleo?

Hoteli zinagharimu kiasi gani zenye hadhi ya kati kwa kulala na kwa usalama na pia mitaa ipi ni salama zaidi?

Je pesa ya kule inathamani gani kwenye kubadilisha yaani mfano 10 pula ni sawa na shilingi ngapi ya tanzania?.

Pia nitegemee kukutana na nini kipya ambacho hakipo hapa kwetu tz nitakapofika botswana?.

Je ni jiji,au mitaa ipi watanzania wengi naweza kuwapata nikifika botswana ili japo nikawasabahi?.

Natumai nitapata majibu mengi yatakayonisaidia juu ya safari yangu.
 
Shukrani Mkuu safari njema. Botswana kuna wabongo wengi wengine hata hawataki kurudi nyumbani na si ajabu baadhi wamo humu na wanaweza kukusaidia sana kufurahia safari
yako.
Asante sana mkuu wish botswana kutamu ndo maana hawataki kurudi tz
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndiyo mkuu....we are not meant to live in one place inatakiwa kufunguka kutafuta green pasture sehemu nyingine.

Binafsi sina information kuhusu Botswana lakini nimesikia mengi mazuri kuhusu Botswana. Kuanzia passport yao yenye nguvu hadi uhitaji wao wa exparts husussani doctors.

Hapa JF ingeanzishwa TRAVEL FORUM ingekuwa poa sana. Kwenye forum watu tungepeana taarifa kuhusu upatikanaji wa visa nchi tofauti duniani. Pia experience tofauti za watu wanaosafiri nchi tofauti dunia. Upatikanaji wa studying visa nchi tofauti na mambo yote yanayohusiana na safari overseas.

Hii forum ikiwepo member wa JF akiingia anajua anaenda Travel Forum kupata info. Tofauti na ilivyo sasa hivi ukitaka experience za watu kuhusu safari abroad mpaka upekue nyuzi tofauti inatumia mda mwingi.

Invisible ona ili pendekezo. Itasaidia pia wana-diaspora kutupatia taarifa za life abroad.
 
Naam huo ndiyo ukweli. Kule wasomi wetu wahasibu, madaktari, wahandisi etc wanathaminiwa sana na kulipwa vizuri. Sasa nani atataka arudi mahali ambapo hathaminiwi na mshahara wenyewe njiwa hautoshi hata kwa gharama za kila siku za maisha achilia mbali kama unataka kufanya mambo ya maendeleo.

Asante sana mkuu wish botswana kutamu ndo maana hawataki kurudi tz
 
Naam huo ndiyo ukweli. Kule wasomi wetu wahasibu, madaktari, wahandisi etc wanathaminiwa sana na kulipwa vizuri. Sasa nani atataka arudi mahali ambapo hathaminiwi na mshahara wenyewe njiwa hautoshi hata kwa gharama za kila siku za maisha achilia mbali kama unataka kufanya mambo ya maendeleo.
Ahaa haki ya mama nikienda naweza nisirudi kwa maana huu upepo unaoendelea hapa tz haufai.
 
Mambo mengine muwe mnauliza Google, hapa tukiwapoteza sisi hatumo! Hukumbiki shibekijijini njaa mjini aliingia kichwa kichwa akapewa ushauri ndani ya siku 2 akapanda bus kwenda South? Yuko wapi sasa?
 
Daktari hongera kwa safari kwenda Botswana kutokea Dar unapanda Taqwa bus linaloenda Bulawayo kupitia Livingstone wewe unashuka hapo Livingstone unaelekea Kazungura boarder ni mpaka kati ya Zambia na Botswana hapo kuna kivuko upande wa Botswana ukivuka unagonga pass unapanda bus zinazokwenda Fransistown au Gabs moja kwa moja kutoka kazungura mpaka Fransistown ni 550km na Fransis Town mpaka Gaborone ni kama 440km kuingia Botswana lazima uwe na address na simu ya mwenyeji wako kama utakaa hapo miji iliyopo Bots ni Gaborone,Nata,Pahalapye,Maharapye,Fransistown mara nyingi fursa zinakuepo katika mji mkubwa kama Gaborone au Fransistown..sijajua wewe unataka kufanya shughuli gani pale nauli kutoka Dar kwa Taqwa ipo 70usd mpaka Livingstone na kazungura mpaka Fransistown pula 250 na mpaka Gabs pula 300 kama tsh 60,000 mpaka 70,000 kutokea hapo boarder gharama ya hotel ni rand au pula 300 ukienda Gabs waambie tax driver akupeleke kwa wachina wana affordable hotel harafu nzuri zipo Kagiso hapo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom