*TANGAZO*
*Mkuu wa CHUO CHA TEHAMA CHA VETA KIPAWA anakutangazia nafasi ya kusoma kozi Maalum ya Ufundi simu kwa muda wa Wiki 6. Mafunzo haya yatawanufaisha washiriki 400 kwa ufadhili wa ADA pekee toka Serikalini.*
Mafunzo haya yatakuwezesha mwanafunzi kusoma hatua zote tatu za mafunzo yaani;
1. Hatua ya Awali *(BASIC)*
2. Hatua ya Kati *(INTERMEDIATE)*
3. Hatua ya Juu *(ADVANCE)*
Utakapofaulu na Kuhitimu, utatunukiwa *CHETI* kutoka *VETA* kitakachokuwezesha kupata *LESENI* kutoka *Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)* inayokupa kibali kufanya kazi ya ufundi Simu.
Mafunzo haya yatakuwezesha kufahamu na kupata ujuzi juu ya;
1. *Misingi ya utengenezaji wa vifaa vya kielekitroniki*
2. *Kutambua na kutatua matatizo ya simu za mikononi (SOFTWARE & HARDWARE)*
3. *Elimu ya Ujasiliamali*
4. *Utambuzi wa Sheria, taratibu na kanuni za Mawasiliano zinazoongoza tasnia nzima ya ufundi wa Simu*
*Mafunzo haya ni BURE. Mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 15/7/2020*
Huu ni ufadhili unaotolewa na *Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania* kupitia *Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF)* chini ya *Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).*
Fomu za maombi ya ufadhili zinapatikana kupitia
http://tiny.cc/ufundiSimu au Tembelea tovuti ya Chuo
www.vetakipawa.ac.tz
Mafunzo yatafanyika katika chuo cha TEHAMA cha VETA KIPAWA kilichopo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Ilala, Kata ya Kipawa (Karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere.
*Kwa maelezo zaidi Piga simu 0714 720 381*
*IMETOLEWA NA MKUU WA CHUO CHA TEHAMA VETA CHA KIPAWA*
Sent from my CPH1803 using
JamiiForums mobile app