Tafadhari nijuzeni ubora wa gari aina ya Subaru Forester
Naona hujapata majibu ya kutosha. Acha niongeze na langu.
Hili Gari nilishalindesha, na pia mjomba wangu mmoja anakula bata nalo huu mwaka wa 6. Yote ni toleo la mwaka 2004. Kwa mtazamo wangu, ili toleo ni bora kuliko la mwanzo; kimuonekano na pia ground clearance.
Subaru Forester Gari tamu sana. Angalia usinogewe, maana linachanganya faster, alafu comfortable kinoma. Spare zake bei kubwa, ila ni original, unaweka leo, kuja kuweka tena... Unasema kweli muda umekwenda.
Mkikutana kwenye tuta na V8, unaliovertake. Linaitwa gari la vijana for a reason. Kuhusu mafuta, usinunue yenye turbo. Ya kawaida ipo vizuri. Inakula mafuta sawa na Rav4, pamoja na Harrier. AWD iko poa sana. Hukwami aisee, linapopita Rav4, nawewe unapita. Lina bonge la space ndani, sio kama Rav4.
Conclusion:
Hili ndio la muhimu, kama huna plans za kuuza na unataka kufunga nalo ndoa ya kikristo, nunua. Kama unaplan kubadilisha in 1 year, I strongly recommend against it. Maana utaagiza mpaka hapa for 10-11m alafu utakuja kuliuza bei moja na Passo, 5-7m. Ningekuwa kwenye your position ningechukua Rav4 old shape, value yake haishuki. But kama unataka wajukuu waliendeshe na unapenda mbio, chukua forester.
-callmeGhost