Kwanza: Wenyeji ni Wasafwa.Japo walio wengi hawaishi mjini bali pembezoni ya mji. Wakazi wengi ni Wanyakyusa na Wakinga, japo pia yapo makabila mengin:Wanyiha,Wanyamwanga,Wandali,na mengineyo mengi.
Maswali yako:
1. Gharama za maisha zikoje ukilinganisha na sehemu nyingine? (Chakula,Nyumba za kupanga mf. chumba kimoja cha self au chumba na sebule kinaweza kupatikana kwa bei gani? )Japo ni moja ya majiji ya Tanzania,lakini gharama yake ya maisha ni nafuu sana:chakula, usafiri hauna foleni.Kwa maisha ya kawaida Tshs 5000-10000 inatosha kwa siku. Nyumba ya kupanga inategemea na eneo.Block T,Sae,Forest Mpya,Uzunguni (Kati ya 200000-1000000) kwa mwezi. Maeneo ya kawaida: 50,000-150000 kwa mwezi
2. Hali ya hewa?Ni baridi Mei-Agosti usiku inaweza kufikia nyuzi joto 0 kwa baadhi ya siku wakati wa usiku mchana nyuzi 15 jotoridi. Ila kwa kawaida joto huwa kati ya nyuzi 28-15 siku za kawaida. Ni mji wenye vumbi sana hasa wakati wa kiangazi (Septemba)huwa kuna tufani ya vumbi...
3. Biashara gani ambayo haijasambaa sana (mf. Maduka ya nguo za watoto/watu wazima, restaurants, saluni,internet café n.k) Binafsi: naweza kushauri mgahawa (restaurant) wa kisasa.Mji ule una mapungufu hayo,pengine kwakukosa wageni wengi kama watalii? Duka la nguo unaweza,ila jiandae kupambana na Wakinga a.k.a Wachaga wa Mbeya.
4. Shule nzuri za chekechea kuanzia 2yrs (gharama na upatikanaji). Jaribu UWATA, St.Mary's kwa kutaja chache kati ya nyingi.
Mchango wangu kwa ufupi.