Habari wana JF, ninaomba kupata ufafanuzi kuhusu swala hili. Matangozo ya ajira hasa ktk taasisi za serikali yanapotolewa huwa wanasisitiza kuwa, kama unaomba nafasi ya kazi na huku umeajiriwa ktk utumishi wa uma basi barua yako ya maombi ipitie kwa muajiri wako. Sasa naomba nifahamishwe faida za kuipitisha na hasara zake kama hutoipitisha barua kwa mwajiri wako.