Naogopa mamlaka waliyozidishiwa wakuu wa wilaya na mkoa kwa walimu

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,061
Ndugu Wapendwa wa JF,
Kwa uzalendo mkubwa juu ya nchi yangu Tanzania napenda nianze na nukuu ya Abrahan Maslow aliyewahi kusema,
“Ukiwa na nyundo unaona kila tatizo kama msumari”. Vilevile nimnukuu Plato aliyewahi kusema “Maamuzi mazuri huegemea maarifa na siyo umri” na mwisho nimnukuu Tata Madiba 'Nelson Mandela' aliyewahi kusema
“Elimu ni silaha yenye nguvu yenye uwezo wa kuibadilisha dunia."

Walimu wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013.
Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel
Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga.
Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka kwenye vitambulisho (passport size).
Akitangaza uamuzi huo, Mulongo alisema tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa Januari 27, kuchunguza tuhuma dhidi ya walimu hao kujihusisha na mapenzi na wanafunzi imebaini ukweli baada ya kuwahoji wanafunzi kadhaa.
“Ni fedheha na haivumiliki kuona walimu wakifanya mapenzi na wanafunzi wao. OCD wakamate walimu wote na uanze uchunguzi mara moja na kukusanya ushahidi utakaowezesha wahusika kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza Mulongo.
Hapa ndipo ninapopata tatizo juu ya wamiliki nyundo hawa maana wanaona kila tatizo ni msumari. Licha ya kuwakamata walimu tajwa hapo juu hakuna hata mwalimu mmoja aliyekamatwa na mwanafunzi akizini nae zaidi ya tetesi tu hivyo hakuna ushahidi wa kujitosheleza, imebidi walimu wakasote rumande huku ushahidi ukitafutwa.
Siwatetei walimu hao, tena ikibidi wakamatwe nchi nzima maana huku Kinyanambo, Mafinga kama ni tetesi za walimu kubinuka na jambo la kawaida na mara nyingine wanafunzi wenyewe huzua tetesi, lakini isiwe kwa lengo la ili mradi tu uonekane nawe umetumbua jipu. Je, mwalimu anatakiwa kuwajibishwa na Mkuu wa Mkoa wa Utumishi? Kwa jinsi nilivyoyasoma mazingira walimu wanaweza kushinda kesi, nani atakayewalipa fidia?
Walimu wa Tanzania wenye rekodi ya kutandikwa na mikwaju na maDC Ni vema makosa yao yakashughulikiwa kwa ufasaha. Unamkamata mwalimu Malifedha kisa amewachangisha wanafunzi fedha kwa ajili ya vitambulisho na kumdhalilisha mbele ya jamii, je unajua umeathiri saikolojia ya walimu wangapi? Tume iliyotoa ripoti kwamba wamiliki wa shule za binafsi huwanunua walimu wazuri kutoka shule za umma ni ripoti feki, ripoti kamili ni kwamba serikali haiwathamini walimu kama zamani.
Mwisho nimalizie kwa kumnukuu Abrahamu Linlccon: “Raisi wa 16 wa nchi ya Marekani aliyewahi kusema “Unaweza kuwadanganya watu wote kwa muda fulani na baadhi ya watu wakati wote ila huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote” Kama watumbua majipu mnatudanganya pahala tutajua tu maana hamkosi kuongozana na wandishi wakiwa na kamera zao kama inavyojionyesha katika picha!
 

Attachments

  • MAGESA.jpg
    MAGESA.jpg
    74.5 KB · Views: 39
Tatizo walimu wamekuwa wanyonge kila mpenda sifa anajichukulia sifa kwao, ninachoelewa hapo hamna kesi maana hata hao waliofanyiwa hivyo wataogopa kujitokeza na wakijitokeza kesi haitakuwa na nguvu maana hamna ushahidi wa kimazingira na uthibitisho wa daktari kwa wanafunzi hao wamebaka viongozi waache kutafuta sifa kwa mgongo wa walimu.
 
Kkuna zoezi la kuchagua wakuu wapya wa mikoa na wilaya mpaka sasa aliyehakikishiwa ni mmoja.waliobaki wanatafuta vibali
 
Kkuna zoezi la kuchagua wakuu wapya wa mikoa na wilaya mpaka sasa aliyehakikishiwa ni mmoja.waliobaki wanatafuta vibali
Inawezekana ukawa sahihi kabisa mkuu, kwasababu mazingira ya hatua zinazochukuliwa yana kila ishara ya mashaka
 
Hili jambo linakera sana, ghafra wanasiasa wamekuwa watakatifu na watumishi wamekuwa mashetani. Nawashauri watumishi wajipange wajue namna ya kujinasua kwenye mtego huu.
 
Back
Top Bottom