Mwan mpambanaji
JF-Expert Member
- Apr 3, 2008
- 482
- 131
Ndugu wanaJf
Habari za uhakika kutoka kwenye baraza la uongozi la chadema mkoa,lililokaa kwa siku mbili mfululizo,kujadili hali halisi ya kisiasa Arusha mjini,limegundua makosa mengi ya kiuongozi ngazi ya wilaya,na mara baada ya majadiliano kamati tendaji yote ya wilaya ikaamua kujiuzulu kwa hiari, ili kupisha viongozi wapya.
Hivyo Nanyaro ambaye ni diwani wa Levolosi na mmoja wa vijana wenye ushawishi mkubwa wa siasa za upinzani Arusha mjini, kuteuliwa kuongoza task force ya wilaya,yenye lengo la kuimarisha chama, na kuratibu zoezi la uchaguzi wa wilaya.
Hata hivyo mwenyekiti wa mkoa amesisitiza kuwa CHADEMA ni imara,na Nanyaro ameteuliwa kwa kuwa ni mmoja wa viongozi wanaokijua chama Arusha kwa undani,na mwenye rekodi nzuri ndani ya chama
Hivi utaratibu ukoje ndg zangu? kikao kilichokaa jana kilikuwa cha kamati tendaji ya mkoa, imekuwaje ikajadili suala la wilaya ya arusha peke yake? vipi kuhusu wilaya zingine?
Hongera NanyaroNawashukuru sana kwa pongezi zenu za dhati,natambua matarajio makubwa ya umma unaotamani migogoro ya chadema iishe,kimsingi kikao cha siku mbili kilikuwa cha baraza la mashauriano ya mkoa,kilizungumzia wilaya zote,na hali ya kisiasa kwenye wilaya zote za mkoa wa Arusha zinaendelea kutekeleza maazimio ya chama kama tulivyokubaliana kwenye baraza la 1april,kwa Arusha mjini baraza likagundua matatizo mbalimbali ya kiuongozi,ndipo kamati tendaji ikaridhia kujiuzulu ili kupisha uchaguzi wa watu watakaoweza kukiimarisha chama zaidi,hasa ikizingatiwa hali ya Arusha mjini ilivyo
Nashukuru kuwa viongozi wenzangu wamenipa heshima hii kubwa ya kuendeleza pale wenzangu walipofika.
Ni kweli chadema tuna misingi,matawi,na kata,hivyo moja ya majukumu yangu makuu ni kuhakikisha chama kinakuwa imara kuanzia ngazi ya chini kabisa,yaani msingi,hii ni pamoja na kuelekea kwenye uchaguzi wa wilaya
Mapambano yanaendelea