Uzuri wa huyu jamaa ANAJUA kila kitu......watu wengine NUKSI?..
Sasa hivi atasema alikuwa anaishi Jirani na Timbarland, subirini.
Heshima yako mkuu,
- Nimesema siku nyingi sana kwamba katika maisha unapokuwa hujui, then huna choice zaidi ya kuwasikiliza wanaojua, wakuelemishe. Ni clear kwamba kwenye maisha tunazaliwa tofauti, wengine tulizaliwa very active na kupitia mambo mengi sana kwa wakati unaotakiwa, na besides hata system yetu ya kiutawala ilikuwa ina-encourage mambo mengi ambayo siku hizi hakuna tena.
- Tumecheza mpira, kuanzia ya shule za msingi, sekondari, vyuoni, na JKT, kwenye haya mashindano ambayo siku hizi hayapo tena, tumekutana na watu mbali mbali na wa kila aina, ambao wengi wao siku hizi ndio viongozi wetu wa taifa, wamiliki wa biashara kuu nchini, maarufu wa shughuli mbali mbali katika taifa, na wengine ni watu wa kawaida, halafu growing up location that is another story of itself. Kuna wakati mmoja mpira wa miguuu ulikuwa ndio deal, wakati mwingine u-DJ ukawa deal, ikaja ubaharia ndio deal, ndio maana tukapata nafasi ya kujaribu kila kitu katika maisha, sasa I can see the problem kwamba wengiwetu siku hizi hatukupata hizi nafasi, kwa hiyo wale tuliopitia tunapotoa our experience tutaendelea kuwa alliens na kwamba tunajua kila kitu. Tatizo sio kuwa jirani na nani, hapana the ishu ni kama unaweza kuoanisha ujirani na ukweli wa hoja unayo-represent.
- Nilipokuwa NYC, nimepiga sana Disco kwenye club as a DJ as part time, huku ninafanya kazi, na kwenda College pia at the sametime, nimetayarisha sana maonyesho ya miziki NYC na hata hapa nilipo mpaka leo ninaendelea once in a while kufanya hizo shughuli za maonyesho, infact sasa hivi ninafanya research ya kuwawezesha FM Academia Wazee wa Mujini, kwenda US baada ya kumaliza ziara yao ya UK, kwa hiyo mkuu wangu rest assured kwamba hudanganywi tunaposema experience, ila ni ukweli mtupu na cha muhimu ni hoja kama inakubaliana na the claimed experience.
- Tunapoingia hapa kujadili mada, huwa tunaingia with confidence and in a serious manner ama sivyo hatugusi kabisa mada kama hatuna anything on it, tunakaa pembeni na kula elimu ya bure kutoka kwa wengine, otherwise samahani sana kwa kukukwaza kutokana na experience mbali mbali tunazoziweka hapa maana mpaka kumuita bin-adam mwenzio nuksi kwa sababu tu mawazo yake hayakubaliani na yako, that is deep, ningekuelewa ungesema jamaaa ni muongo na ushaidi ni huu sawa, lakini ni nuksi na anajua kila kitu ina maana nimekukwaza, kwa hiyo samahani sana mkuu, nilikuwa najaribu tu kuchangia mada kulingana na experience yangu na Muziki, infact betweeen the two yaani Rose na Bahati, I would rather invest on Rose maana italipa no matter what!
Unless kama hukutaka nishiriki kwenye this Mada, ninakuelewa pia, samahani kwa lecture ndefu lakini muhimu sometimes, na tutaendelea kuweka experience zetu inapobidi na pia kuelimika kutoka kwa wengine kama wewe na experience zenu.
Respect.
FMES