Nani wa kulaumiwa mkanganyiko wa zoezi la sensa.

Dr. - Nadhani ni DEBIT ya kwenye Bookkeeping
PHD na sio PhD.
Sockholm na sio Stockholm

Hapa DSM kuna shule ya msingi Chuo Kikuu kwa hiyo anayehitimu pale anapata cheti cha shule ya msingi sasa anaposema Sockholm University ana maana nyingine.
 
Suala la kuto kuhesabiwa kwa baadhi ya wananchi wa Tanzania hususani wanao toka kwenye dini ya kiislamu serikali haikwepi lawama.Nasema serikali haikwepi lawama kwa sababu moja kuu,haiwezekani serikali ifumbie macho kitendo cha takwimu zilizo tolewa ambazo baadae serikali hiyo hiyo ikaja na staili ya kukanusha.

Wakati takwimu ambazo zimechafua hali ya hewa yaliyotolewa na kubainisha Waislamu wapo 32% na Wakristo 52% serikali ilikuwa wapi mpaka leo hii hali imechafuka ndo serikali inastuka na kukanusha kuwa si za kweli.

Pia aliyetoa takwimu hizo ambazo mpaka sasa zimekwisha pelekea baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kuwekwa ndani na kuonja machungu ya kupinga kuhesabiwa amechukuliwa hatua gani.Kitendo cha kutoa takwimu za kupika katika nchi iliyo na dini tofauti ni hatari kwa mustakabali wa hali ya amani tuliyokuwa tunajivunia.

Serikali imekuwa bingwa wa kuvifungia vyombo vya habari pale vinapo dhihirisha ukweli na uzembe unao fanywa na serikali lakini cha ajabu mpaka sasa hatujaona hatua zozote kwa TBC kufungiwa ama kupewa onyo kali kwa taarifa ambazo tunaamini hata hii sensa inaweza isilete takwimu sahihi aidha kwa kuhujumiwa ama wananchi kutoa taarifa zisizo rasmi.

Sheria ya sensa na makazi ina zungumza nini ikiwa mtu ataamua kuto kuhesabiwa ama kutoa taarifa zisizo za kweli.Kimsingi inajionyesha serikali imefikia maamuzi ya sensa kwa stahili yake ya zima moto bila kuwashirikisha wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kidini na asasi za kiraia.Kushirikishwa kwao toka awali kungesababisha muafaka kupatikana mapema na kuepuka sinto fahamu iliyo jitokeza

Nachukua fursa hii kuiomba serikali yetu tukufu kuachana kabisa na taratibu zake ambazo zina weza kusababisha hali ya amani kutoweka kwa kudhibiti watu ambao kwa kutumia dhamana zao ndani ya serikali wanaamua kuropoka na kusababisha matatizo makubwa.Serikali ina vyombo vyake kwa kutumia maafisa habari wake,lakini cha kushangaza mpaka hali hewa ichafuke ndo serikali ichukue maamuzi yakukanusha na kuomba radhi.

Mwisho Watanzania tusikubali kutumiwa kama chombo cha kupitishia maamuzi ya kizima moto kwa ajili ya maslahi fulani kwa wakati fulani.Tunajua umuhimu wa sensa lakini tuna shirikishwaje katika kufikia maamuzi.Nawatakia sensa njema kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu ila kwa hili lililojitokeza serikali ijifunze na kuacha kukurupuka kwa maamuzi ya kizima moto.
 
Walitoa takwimu za uongo wote wanatakiwa kuwajibishwa. na hata wakitukamata kwa kukataa kuhesabiwa waongeze magereza, lakini hili suala la sensa litaingiza nchi kwenye machafuko kama nguvu zaidi zitatumika.
note my words
 
Walitoa takwimu za uongo wote wanatakiwa kuwajibishwa. na hata wakitukamata kwa kukataa kuhesabiwa waongeze magereza, lakini hili suala la sensa litaingiza nchi kwenye machafuko kama nguvu zaidi zitatumika.
note my words


Kilicho kosekana ndani ya serikali ni hekima,think tank ya taifa ndo imekwenda hakuna wa kumsema mwenzake,tatizo akili ndogo ndiyo inayo tumika kuendesha akili kubwa
 
1.serikali 2.baadhi ya waislamu 3.wanaodai mjusi. 4.baadhi ya mapolisi.5.baadhi ya walimu.6.wanaharakati na wanasiasa waliomafichoni. Tafadhali wana jf.nisaidieni kwa hilo.
 
Back
Top Bottom