Nani wa kulaumiwa hapa jamani

Nani wa kulaumiwa hapa jamani

neha mimi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
344
Reaction score
152
Habar zenu wapendwa, jamani mimi kuna jambo lanitatiza ni kuhusu hii ndoa ambayo naishuhudia kutetereka kwake kama sio kufa kabisa ni hivi; miaka kadhaa iliyopita walifunga ndoa lakini mume na mke wakawa wanaishi mikoa tofauti ni kutokana na kazi zao lakini baadae mume akamshuri mke wake atafute uhamisho ili amfuate mumewe mwanamke akakataa.

Basi maisha yakawa yanaendelea kama kawaida lakini kumbuka mwanamke anaishi kwao hivyo mumewe akirudi likizo afikie ukweni then aende lodge kulala na mkewe na sio kwamba alikuwa hana pa kuishi la hasha mke alipangishiwa nyumba nzima eti kodi ilipoisha akarudi tena kwao eti hataki kukaa mwenyewe ana mtoto na msichana wa kazi.

Basi bwana baada ya mda kwenda sana na watu kumshauri sana ndo mwanamke akaamua kutafuta uhamisho ili amfuate mumewe tena bila kumwambia kibali kilivyokamilika ndo akamwambia mimi nakuja huko sasa basi mume kamwambia asiende coz na yeye anakaribia kuhama mke ashapata uhamisho wa mkoa huo wakati mume anakaribia kuhama sasa hapo ndo mke anahaha ile mbaya anawaza labda mumewe ana mke mwingine ndo mana hataki aende.

Hivi hapo nani wa kulaumiwa jamani manake mwanamke analalamika anaona kaonewa na ni mkorofi huyo, ushauri pliiz kuokoa hii ndoa changa.
 
Sasa hapo kuna kutafuta mchawi tena? mwanamke wakati anakataa kutafuta uhamisho alitoa sababu gani za msingi? na kwanini afanye taratibu za uhamisho kimya kimya wkt mwanzoni alikataaa? hivi wengine kwenye ndoa huwa wanalazimishwaaaaa au wanaamua toka mioyoni mwao?
 
Ni wazi kuwa hakuna mawasiliano mazuri baina yao! Kama nia ya kila mmoja kufanya taratibu zake za uhamisho bila kumwambia mwenzie ilikuwa ni kwa lengo la kumsuprise mwenzie basi wanastahili kupongezana maana wote wamefanikiwa na kila mmoja wao na hata mimi nimekuwa suprised!
 
Mawasiliano mazur n nguzo ya mapenzi. Hiv unafanya uhamisho mumeo wa ndoa hajui haikuji kabjsa!!! Sasa matokea yake amekosa bara na pwani...hiv wanawake wenzangu nan kawaambia ndoa n kushindana na kuleta utemi kwa mumeo??? Hata kama kitu hutaki unaongea nae taratibu mnaelewana...na sio kuamua kujichukulia maamuz mkononi...haya sasa bibie aendw huko anataka kwenda mume nae anarud patam hapo....kosa lake n kuamua kua mkimya na kutomshirikisha mumewe halaf umepangiwa nyumba nzima kwenu kufata nin na ww ushakua mke wa mtu!!! Akili zake zimo kweli kodi imeisha alisema kwa mumewe??? Halaf hizi ndoa za kuish mmoja kaskazi mmoja kusi haina mashiko kabisa!!! Hainikuti hii yaan tunaweka misimamo na maelewano kabla y ndoa najua hata ndoa ikiwepo naelekea wapi baada ya hapo hao wanandoa wana tofaut zao ndan kwa ndani and wasipokua makini very soon ndoa inaparanganyika....
 
Tatizo dogo sana hilo ,maana hata hiyo shida na ugumu siiwoni,aidha mke anaweza kukenseli ,la si hivyo anaweza kuchukua au kubadilisha uwe uhamisho wa muda ,kama atapata huo uwamuzi wa mwanzo basi asiwache kwenda huko kwa mumewake japo wiki na akipata huo uhamisho wa muda atakwenda na kurejea na mumewake ,Jingine Je mume ikiwa yumo kuhama ni nini time limit ya kuhama kwake ?
 
Mawasiliano mazur n nguzo ya mapenzi. Hiv unafanya uhamisho mumeo wa ndoa hajui haikuji kabjsa!!! Sasa matokea yake amekosa bara na pwani...hiv wanawake wenzangu nan kawaambia ndoa n kushindana na kuleta utemi kwa mumeo??? Hata kama kitu hutaki unaongea nae taratibu mnaelewana...na sio kuamua kujichukulia maamuz mkononi...haya sasa bibie aendw huko anataka kwenda mume nae anarud patam hapo....kosa lake n kuamua kua mkimya na kutomshirikisha mumewe halaf umepangiwa nyumba nzima kwenu kufata nin na ww ushakua mke wa mtu!!! Akili zake zimo kweli kodi imeisha alisema kwa mumewe??? Halaf hizi ndoa za kuish mmoja kaskazi mmoja kusi haina mashiko kabisa!!! Hainikuti hii yaan tunaweka misimamo na maelewano kabla y ndoa najua hata ndoa ikiwepo naelekea wapi baada ya hapo hao wanandoa wana tofaut zao ndan kwa ndani and wasipokua makini very soon ndoa inaparanganyika....
hata mi nashindwa kuelewa jaman na huyo mama mtu anamruhusu vip mwanaye arudi kuishi nyumban bila idhini ya mumewe
 
Sasa hapo kuna kutafuta mchawi tena? mwanamke wakati anakataa kutafuta uhamisho alitoa sababu gani za msingi? na kwanini afanye taratibu za uhamisho kimya kimya wkt mwanzoni alikataaa? hivi wengine kwenye ndoa huwa wanalazimishwaaaaa au wanaamua toka mioyoni mwao?

awe na sababu gani jeuri tuu alisema hataki kuhamia huo mkoa yan hapo ni jeuri naona kama wanafanya kukomeshana mwanaume jeuri mwanamke ndo usisema
 
nimechoka.nta comment asbh.maana wote wawil jeur.mama mkwe nae kiazi tu.nin kupokea bint wakat usha muoza..
 
h mume akamshuri mke wake atafute uhamisho ili amfuate mumewe mwanamke akakataa

mwanamke akaamua kutafuta uhamisho ili amfuate mumewe tena bila kumwambia
jaman manake mwanamke analalamika anaona kaonewa na ni mkorofi huyo ,ushauri pliiz kuokoa hii ndoa changa
Kwa maneno yako mwenyewe mwanamke ndio mkorofi na wa kulaumiwa
 
Kuna vitu hata havihitaji ushauri maana ni kama unapaka rangi upepo tu...
 
Wote wawili hawajitambui. Hivi how come unaishi mbali na mkeo au mumeo. Eti kisa kazi. Kwani huko mikoani hakuna kazi? Lol mimi nilisha apa simwachi mke wangu nyumba. Tutafuatana kila mahali ninapo kwenda. Kama akikosa kazi atafuga hata kuku.
 
Kaka angu, m.mke uyo yupo wapi siku hizi, thubutu yake. wabishi kama chuma,
 
ukitaka ku short circuit ndoa yako muishi miji tofauti.

mume hata siku moja hapewi taarifa. mume anaombwa na baada ya idhini yake ndio mke anatenda
 
Back
Top Bottom