Nani rafiki yako?

Kuwa rafiki wa nafsi yako mwenyewe....

Hivi leo, ni nani ambaye anaweza kuwa rafiki yako wa kweli, na ukasema mble ya watu kuwa huyu ni rafiki yangu kipenzi. mfano, hata mkeo leo anasaliti, mama mzazi na hata baba wote wasaliti. niende wapi?
 
Ningekuwa na uwezo ningekushauri uachike halafu ujifunze ndoa ni nini kisha uolewe upya

Haya maelezo yako yanaonesha umeolewa kwa sababu umezaliwa ukakuta kuna kuolewa na sio unajua nini maana nna sababu ya kuolewa
Pole sana!
pole yako na wewe tunaishi kwa akili na kumwomba mungu binadamu haaniniki hasa mliekutana ukubwani najua hujaoa ukioa utajua nini namaanisha .ubwage moyo na wewe ubwagiwe pole yako wenzio wananyolewa wewe unapaka superblack badala ya maji ???hatuishi sayari nyingine na haya yanatokea kwenye hihihi EARTH PLANET so be carefully when you talk about marriage kama sio mwanachama.
 
Ukweli ni ukweli wala hauwezi kubadilishwa na chochote!

Narudia tena hujui nini maana ya ndoa kama ungejua usingesema haya
Watu kuwa waovu haiondoi msingi wa ndoa

Mara nyingi sana matatizo mengi ya kindoa husababishwa na wana ndoa wenyewe hasa wenye mtazamo kama wako

Kuna kitu kingine nimekiona kwenye maelezo yako,inaonekana wewe humuamini mumeo na mnaishi kimazoea sana,kama hakuna migogoro kwenye ndoa yenu basi tarajieni kuingia kwenye migogoro siku sio nyingi!

Kwenye maelezo yako umemtaja Mungu,hivi unamjua Mungu ni nani Nivea ??
 
Last edited by a moderator:
Hivi leo, ni nani ambaye anaweza kuwa rafiki yako wa kweli, na ukasema mble ya watu kuwa huyu ni rafiki yangu kipenzi. mfano, hata mkeo leo anasaliti, mama mzazi na hata baba wote wasaliti. niende wapi?

swali lakio ni gumu kwani mioyo yetu imejaa unafiki..
 
kama huna ndoa huwezi kuwa mshauri mzuri wa ndoa ,utashauri kimazoea tu nakuhukumu! Mimi kwenye mggoro kamwe hutasikia !!na ni miaka mingi haijawahi tokea so usiniaminishe unachoamini wewe siishi mars mimi narudia tena naishi kwenye dunia ambayo nashuhudia mengi yakitokea so siwezi ishi kama mjinga bila alert! Nisubiri yanikute naishi kwa akili huku nikimwomba mungu sana.kuhusu kumjua mungu-inawezekana mungu ninayemjua mimi sio unayemjua wewe nafikiri kaa kwenye unachokiamini usiniaminishe unachokiamini!
 
Hiyo haikuwa pointi yangu

Narudia tena siku ukijua ndoa ni nini na kama unahitaji kuishi kwa furaha[sio raha] utajifunza hayo
Wewe unaishi kama askari alieko vitani kila wakati anahisi kuvamiwa
Matatizo unayoyaleta kwa kuishi hivyo huyajui lakini unahatarisha maisha yako kwa kiwango kikubwa sana hata kuliko kuishi bila tahadhari kama ulivyosema wewe

kuhusu kumjua mungu-inawezekana mungu ninayemjua mimi sio unayemjua wewe nafikiri kaa kwenye unachokiamini usiniaminishe unachokiamini!

Sikumaanisha nikubadilishe kwenye kile unachokiamini wewe
Lakini hii kauli inaonekana inatoka kwa mtu ambae amechoka sana na hataki kujishughulisha tena kujijua na kuijua kweli

Vipi kama Mungu unaemjua wewe sio halisi?
Vipi kama namna unavyomjua Mungu sio sahihi jambo linalopelekea ukosee kwenye mambo mengi?

Kujifunza sio vibaya

Natamani sana uyafurahie maisha kwa uhalisia wake wewe na familia yako kama huyafurahii
Lakini haya ni mawazo yangu tu unaweza kuachana nayo kama hayakufai au nakosea na hayana uhalisia wowote!
 
ni kweli unakosea na hayana uhalisia wowote!
ila nashukuru kwa kujitahdi kuvaa uhalisia!
 
ni kweli unakosea na hayana uhalisia wowote!
ila nashukuru kwa kujitahdi kuvaa uhalisia!

Mbona hizi kauli zako zinakinzana?

Kama ninakosea na maelezo yangu hayana ukweli wowote ni uhalisia gani niliojitahidi kuuvaa?
 
Hivi leo, ni nani ambaye anaweza kuwa rafiki yako wa kweli, na ukasema mble ya watu kuwa huyu ni rafiki yangu kipenzi. mfano, hata mkeo leo anasaliti, mama mzazi na hata baba wote wasaliti. niende wapi?
rafiki wa kweli ni miguu yangu yangu popote nipo nae
 
WaTZ bwana.... tuanaongoza kulitaja jina la Mungu, makanisa na misikiti inajaa kila kukicha... ila tumejaa kila aina ya udhalimu!
I'd rather not mention his name!
 
Hivi leo, ni nani ambaye anaweza kuwa rafiki yako wa kweli, na ukasema mble ya watu kuwa huyu ni rafiki yangu kipenzi. mfano, hata mkeo leo anasaliti, mama mzazi na hata baba wote wasaliti. niende wapi?

Hakuna rafiki wa kweli, siku zote mbaya wako ni mtu wa nyumbani kwako. Uliyemuamini na ukamwambia kila kitu chako. Mtu asiyekufahamu ni ngumu kukudhuru maana hajui una uwezo wa kiwango gani.
Tunahitaji marafiki, mume, mke, dada, kaka kwa sababu hauwezi kuishi peke yako kama uko kisiwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…