Kwa hiyo inawezekana haya anayoyafanya alishajiandaa kuyafanya akiwa waziri wa wizara hiyo. Bahati mbaya hakupata nafasi hiyo. Lakini kwqa kuwa alishaweka wazo hilo inakuwa vigumu kwake kusahau hivyo anajikuta anafanya kazi kama waziri na si mwenyekiti wa kamati.J. Makamba ilikuwa awe waziri wa nishati na madini public opinion ikaenda against matakwa ya mkwere!
Januari, kama tulivyosema huko nyuma, ana ajenda ya kufanikisha na kwa bahati mbaya sana ajenda hiyo hata huyo waziri ni zao la ajenda hiyo. Sisi wengine tumeshakemea sana hilo katika thread zilizotangulia, lakini livyo sasa ni dhahiri kwamba huyo waziri ambaye kwa sasa amekuwa kimya baada ya kuchafua hali ya hewa na Dowans yake, hana la kuwaambia watanzania aliodhani ukiwakaririsha kwamba wenye Dowans ni wale wanaoonekana Brela basi tutakubali. Maskini hakujua kwamba watanzania walishamjua kitambo na wana hasira na anayoendelea kuyafanya kwa maslahi ya king makers wake na hata kuisaliti mamlaka iliyomteua.
Januari Makamba amefanya kile ambacho wazungu wanasema "he has walked into the Lion's lair and is struggling to roar like the lion". Kamwe hawezi kufuta nyayo za mzee Shellukindo katika Kamati hiyo hata akiamua kuhamia ofisi za wizara au kuhamia pale Tanesco. Amepata CD mpya inayoitwa mgao wa umeme lakini uzuri ni kwamba Mungu ataitoa upya CD hiyo kwa kujaza mabwawa halafu baada ya hapo atabaki hana wasikilizaji na chati ya hiyo CD itaporomoka. Kwa ujumla Januari atafute namna nyingine ya kulipa madeni yake aliyochukua kutoka kwa hao waliomuweka madarakani. Na siyo kuingilia majukumu ya mhimili mwingine wa dola ambao yeye hayumo! TUMEKUCHOKA JANUARI!
He is going to fix umeme problems in your country. Nendeni kwenye public hearing ya umeme na dowans ili na nyie msikike. Acheni conspiracy wakati kamati is being incredibly transparent. Au kwa sababu Mheshimiwa Makamba sio mbunge wa Chadema kwa hiyo umeme sio ishu tena. Yaani watu mnakubali kukaa kwenye giza ili mheshimiwa Makamba asifanikiwe kwa sababu ni CCM.
It is true that we now know all these IPTL/CTI position/mpango wa gesi, na data zingine kibao kwa sababu ya kazi ya kamati yake. And we will know even more once the report is coming out. Hebu waTanzania muwe na mentality ya kufix problems na sio kubaki kutoa lawama kwa nini tatizo limetokea.
Nadhani hujawaelewa wachangiaji, na pili huelewi mgawanyo wa madaraka.
Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali itekeleze majukumu yake. Kamati za bunge haziwajibiki kwa wananchi au serikali moja kwa moja bali kwa bunge.Mzee Shelukindo alipofanya uchunguzi wa awali kuhusu Richmond alifikisha taarifa yake mbele ya bunge, na bunge likaitaka serikali ifaye uchunguzi, ndipo miujiza ya TAKUKURU ilipoanzia.
Baada ya kutoridhishwa, bunge likaunda kamati ya Mwakyembe na matokeo yake tunayajua. Ikafikisha mapendekezo kwa serikali ambayo iligoma kuyatekeleza, hapo hakukuwa na jinsi kutokana na katiba ya nchi inayompa Rais uwezo wa kila kitu.
Makamba kama kamati zingine za bunge zilizopo na zilizotangulia anatakiwa afikishe taarifa zake ndani ya bunge na si kuongea na vyombo vya habari kila siku. Yeye si msemaji au mtendaji wa wizara ya nishati na madini. Lakini pia fahamu January uwepo wake pale una maana kwa masilahi fulani. Kwahiyo kufanikiwa kwake si kwa ajili ya umma bali person gain. Kama ni kufanikiwa, kwanini Makinda hataki suala hili lijadiliwe bungeni? jiulize! nani anamkwaza January kama unavyotaka tuamini!
Yeye akiwa msaidizi wa Rais wa zamani anajua kila kitu kuhusu umeme, Dowans, Richmond na madudu mengine mengi tu. Hili suala la kujitokeza mara kwa mara ni kutafuta cheap popularity.
Jiulize kwanini Ngeleja anakwepa suala hili! anajua wazi kuwa kuna utata na unaweza kuiweka serikali pabaya zaidi. Sasa wanaitumia TANESCO kukamilisha mission. TANESCO ni serikali ile ile, wajumbe wake wanateuliwa na Rais kwa ushirikiano na waziri husika. Kuwapa kazi ya kumaliza Dowans ni kujivua madaraka na kuendesha mambo kwa remote. Tunajua hili.
Swali lako lilitakiwa linzie ikulu.
Ni nani rais wa nchi hii maana JK ni kama front desk man tu.
Watu kama:
- RA
- EL
- Chenge
- Karamagi
- Mkono
- n.k wana vnyadhifa na vyeo vya kufa mtu serikalini. Ukishamjua rais ni rahisi kuwajua mawaziri wake
Wakuu Nguruvi3 na Mkeshaji wala msijisumbue na huyo Selemani. Angalieni kila topic inayomuhusu Makamba, kuanzia baba hadi mtoto yeye atatetea..... Nafikiri jibu mmelipata na jibu lako mkuu Nguruvi3 nadhani kijana atalitafakari.