Nani ni waziri wa wizara ya Nishati na Madini, January Makamba au William Ngeleja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani ni waziri wa wizara ya Nishati na Madini, January Makamba au William Ngeleja?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkeshaji, Feb 26, 2011.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakuu Salaam;
  Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia jinsi Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. January Makamba jinsi alivyokuwa na sauti ya kuwa msemaji mkuu wa wizara hiyo hasa katika mambo yahusuyo umeme. Yaani amekuwa na sauti hata kumshinda waziri mwenye dhamana na wizara hiyo Mh. William Ngeleja. Je kiutaratibu anachokifanya January ni sawa ama anavuka mipaka ya kazi yake? Au ni kuwa waziri wa wizara husika ha-perform ndiyo maana January anasikika sana?
   
 2. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  J. Makamba ilikuwa awe waziri wa nishati na madini public opinion ikaenda against matakwa ya mkwere!
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Januari, kama tulivyosema huko nyuma, ana ajenda ya kufanikisha na kwa bahati mbaya sana ajenda hiyo hata huyo waziri ni zao la ajenda hiyo. Sisi wengine tumeshakemea sana hilo katika thread zilizotangulia, lakini livyo sasa ni dhahiri kwamba huyo waziri ambaye kwa sasa amekuwa kimya baada ya kuchafua hali ya hewa na Dowans yake, hana la kuwaambia watanzania aliodhani ukiwakaririsha kwamba wenye Dowans ni wale wanaoonekana Brela basi tutakubali. Maskini hakujua kwamba watanzania walishamjua kitambo na wana hasira na anayoendelea kuyafanya kwa maslahi ya king makers wake na hata kuisaliti mamlaka iliyomteua.

  Januari Makamba amefanya kile ambacho wazungu wanasema "he has walked into the Lion's lair and is struggling to roar like the lion". Kamwe hawezi kufuta nyayo za mzee Shellukindo katika Kamati hiyo hata akiamua kuhamia ofisi za wizara au kuhamia pale Tanesco. Amepata CD mpya inayoitwa mgao wa umeme lakini uzuri ni kwamba Mungu ataitoa upya CD hiyo kwa kujaza mabwawa halafu baada ya hapo atabaki hana wasikilizaji na chati ya hiyo CD itaporomoka. Kwa ujumla Januari atafute namna nyingine ya kulipa madeni yake aliyochukua kutoka kwa hao waliomuweka madarakani. Na siyo kuingilia majukumu ya mhimili mwingine wa dola ambao yeye hayumo! TUMEKUCHOKA JANUARI!
   
 4. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Swali lako lilitakiwa linzie ikulu.

  Ni nani rais wa nchi hii maana JK ni kama front desk man tu.
  Watu kama:
  - RA
  - EL
  - Chenge
  - Karamagi
  - Mkono
  - n.k wana vnyadhifa na vyeo vya kufa mtu serikalini. Ukishamjua rais ni rahisi kuwajua mawaziri wake
   
 5. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Salama Ng. Mkeshaji,
  Hawa watu hata mimi siwaelewi vizuri lakini ninachoamini kwa uhakika wote wapo kwenye Payroll ya Dowans. Kati yao hakuna aliye na dhati ya kuwasaidia wanyonge kuondokana na tatizo la giza. Ngeleja na RA (Hidden Presidential Powers) wana historia ya upamoja katika kutengeneza fedha inawezekana ndo maana Ngeleja yuko ktk Wizara ile (kuficha uozo na kuwezesha ulaji wa Bosi wake halisi). Unakumbuka alisema Serikali inajiandaa kuwalipa Dowans hata kabla kikao cha Baraza la Mawaziri kukaa? (Nakwambia siku hawa jamaa wakiondoka madarakani utajua mengi!). Jauary Makamba ni mtoto wa Katibu Mkuu wa Chama, alikuwa Ikulu na baadaye kuwa Mbunge wa Bumbuli (Pengine kwa Nguvu ya Baba na Ikulu).
  Makamba Mzee alisema anayepinga kulipwa Dowans ndani ya Chama anaweza kurejesha kadi na kwenda zake anakotaka. Sasa leo January naye kelele kibao Mitambo ya Dowans itumike!.. itumike!. Unadhani yote haya ni bahati Mbaya? Huu ni mpango rasmi wa RA ambaye kimsingi ndiye Amri Jeshi ndani ya Mtandao ulioileta awamu ya nne madarakani. Anachotaka RA ni mabilioni yake akatumie na rafiki zake.
  Kelele zote za hawa watu (Ngeleja, January Makamba, Baba yake, na wengine wengi) ni kugombea penzi la bosi wao RA ili ikiwezekana awawezeshe kufikia ndoto zao kama kupata urais, uwaziri na hata uspika. Na amini, hawa jamaa wanajipendekeza kiasi cha kuweza kufanya jambo lolote hata la kujidhalilisha ili kumfurahisha huyu Bwana.
  RA, mbinu na fedha zake ndiyo sababu ya unafiki wote wa wanasiasa wa Tanzania. Wengine hata hawajui kama utajiri wake (RA) unatokana na wao wanasiasa wenyewe. Anawafadhili katika kampeni kwa Bilioni 20 za serikali/umma kama ilivyokuwa kupitia KAGODA halafu baadaye anaondoka na kiasi kilichobaki na kupewa zabuni nyingine nyingi ambazo hata utekelezaji wake unakuwa hovyo kwa malipo ya juu.
   
 6. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo inawezekana haya anayoyafanya alishajiandaa kuyafanya akiwa waziri wa wizara hiyo. Bahati mbaya hakupata nafasi hiyo. Lakini kwqa kuwa alishaweka wazo hilo inakuwa vigumu kwake kusahau hivyo anajikuta anafanya kazi kama waziri na si mwenyekiti wa kamati.
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nadhani time will tell. Sakata la mgawo wa umeme likiisha sijui atahamia wapi. Kwenye madini? Hatujui. Tusubiri tuone.
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  none of the above is capable to handle that position
   
 9. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Hivi hizi kamati za bunge zinafanyaje kazi, wenyeviti wake wanapeleka / ripot wapi ya kazi zao? It's in the bunge I suppose. Sasa huyu January vipi?
   
 10. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni vema January akaelimishwe ya kuwa kazi ya bunge ni kusimamia utendaji wa serikali na KAMWE siyo kufanya kazi kwa niaba ya serikali.
   
 11. S

  Selemani JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  He is going to fix umeme problems in your country. Nendeni kwenye public hearing ya umeme na dowans ili na nyie msikike. Acheni conspiracy wakati kamati is being incredibly transparent. Au kwa sababu Mheshimiwa Makamba sio mbunge wa Chadema kwa hiyo umeme sio ishu tena. Yaani watu mnakubali kukaa kwenye giza ili mheshimiwa Makamba asifanikiwe kwa sababu ni CCM.

  It is true that we now know all these IPTL/CTI position/mpango wa gesi, na data zingine kibao kwa sababu ya kazi ya kamati yake. And we will know even more once the report is coming out. Hebu waTanzania muwe na mentality ya kufix problems na sio kubaki kutoa lawama kwa nini tatizo limetokea.
   
 12. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,174
  Trophy Points: 280
  January Makamba ni nshambaa...!! Kuna umuhimu Wa kupimana akili ndipo uwe mbunge
   
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Nadhani hujawaelewa wachangiaji, na pili huelewi mgawanyo wa madaraka.
  Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali itekeleze majukumu yake. Kamati za bunge haziwajibiki kwa wananchi au serikali moja kwa moja bali kwa bunge.Mzee Shelukindo alipofanya uchunguzi wa awali kuhusu Richmond alifikisha taarifa yake mbele ya bunge, na bunge likaitaka serikali ifaye uchunguzi, ndipo miujiza ya TAKUKURU ilipoanzia.
  Baada ya kutoridhishwa, bunge likaunda kamati ya Mwakyembe na matokeo yake tunayajua. Ikafikisha mapendekezo kwa serikali ambayo iligoma kuyatekeleza, hapo hakukuwa na jinsi kutokana na katiba ya nchi inayompa Rais uwezo wa kila kitu.

  Makamba kama kamati zingine za bunge zilizopo na zilizotangulia anatakiwa afikishe taarifa zake ndani ya bunge na si kuongea na vyombo vya habari kila siku. Yeye si msemaji au mtendaji wa wizara ya nishati na madini. Lakini pia fahamu January uwepo wake pale una maana kwa masilahi fulani. Kwahiyo kufanikiwa kwake si kwa ajili ya umma bali person gain. Kama ni kufanikiwa, kwanini Makinda hataki suala hili lijadiliwe bungeni? jiulize! nani anamkwaza January kama unavyotaka tuamini!
  Yeye akiwa msaidizi wa Rais wa zamani anajua kila kitu kuhusu umeme, Dowans, Richmond na madudu mengine mengi tu. Hili suala la kujitokeza mara kwa mara ni kutafuta cheap popularity.
  Jiulize kwanini Ngeleja anakwepa suala hili! anajua wazi kuwa kuna utata na unaweza kuiweka serikali pabaya zaidi. Sasa wanaitumia TANESCO kukamilisha mission. TANESCO ni serikali ile ile, wajumbe wake wanateuliwa na Rais kwa ushirikiano na waziri husika. Kuwapa kazi ya kumaliza Dowans ni kujivua madaraka na kuendesha mambo kwa remote. Tunajua hili.
   
 14. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siku nitakapothibisiwa kuna tofauti kati ya William Ngeleja na January Makamba, ndio nitaweza kuchagia hoja, kwa sasa:hand:
   
 15. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Watu wengine huwa wanadandia mada bila kuielewa. Mkuu nadhani umemjibu vizuri sana. Thanks.

  [/QUOTE]
  Originally Posted by Selemani [​IMG]
  He is going to fix umeme problems in your country. Nendeni kwenye public hearing ya umeme na dowans ili na nyie msikike. Acheni conspiracy wakati kamati is being incredibly transparent. Au kwa sababu Mheshimiwa Makamba sio mbunge wa Chadema kwa hiyo umeme sio ishu tena. Yaani watu mnakubali kukaa kwenye giza ili mheshimiwa Makamba asifanikiwe kwa sababu ni CCM.

  It is true that we now know all these IPTL/CTI position/mpango wa gesi, na data zingine kibao kwa sababu ya kazi ya kamati yake. And we will know even more once the report is coming out. Hebu waTanzania muwe na mentality ya kufix problems na sio kubaki kutoa lawama kwa nini tatizo limetokea.
  [/QUOTE]
   
 16. Y

  YE JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakuu Nguruvi3 na Mkeshaji wala msijisumbue na huyo Selemani. Angalieni kila topic inayomuhusu Makamba, kuanzia baba hadi mtoto yeye atatetea..... Nafikiri jibu mmelipata na jibu lako mkuu Nguruvi3 nadhani kijana atalitafakari.
   
 17. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  na kama raisi sio mkwere basi hata waziri wa hiyo wizara sio ngeleja,ni hao wasaidizi wa RA
   
 18. S

  Selemani JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Negroe u already know! The idea is not to allow silly/dumb/stupid ideas to become reality just because of niggazz hating. Ukimwaga point za ukweli folks will be willing to listen but if you bring hypocrisy RA sijui Ngeleja, lawyer Vodacom, Ufisadi, Iran; GTFOH! We do big things, and that include fixing umeme problem, regardless you are chadema au CCM. The plan is to come with the out of the box ideas to fix umeme for good. If u want be the part of it, this is your time--if not, you will be on the wrong side of history! Plus this is online, don't forget that. We are ina virtual world.
   
 19. K

  Kishili JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 293
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa nini seriakali ya makamba haina mpango wa kununua mitambo ya MW260 ila inataka ikodishe tena kwa RA kwa gharama kubwa zaidi ya ile ya kununua halafu baadaye tena kesi na malipo zaidi. Kwa kweli kama noma na iwe noma ndiyo maana wameanza vitisho kwa wananchi kwa hofu ya CHADEMA
   
 20. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wote ndugu moja toka CHICHIMU.

  Sulu ya umeme haitaji mijadala mirefu. Kila mtu anajua ni nini kinatakiwa kufanyika ili kumaliza tatizo la umeme. Solution ni kujenga tu vyanzo imara vya kuzalisha umeme kwa kizazi hiki na kizaza kijacho. Tunajua kutoka na kubadilika kwa hali ya hewa hapa nchi ni busara tena kutegemea maji ya mvua. Tunatakiwa tuwe na alternatives nyingine kama makaa ya mawe, gasi alisilia, uranium na upepo.

  Tuachane na mipango ya kukodisha majenereta kabisa, kwani tunalipa hela nyingi kwa matapeli tu bure.

  Halafu hivyo vyanzo vipya vya umeme lazima vimelikiwe na serikali yenyewe. Ikiwezekana tuanzishe agency au kampuni nyingine ya kuzalisha umeme na kuwauzia Tanesco. Hii itaongeza effeciency kwani kila mmoja atapimwa kwa performance yake.
   
Loading...