sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,685
- 1,111
Kuna swali liliulizwa humu ndani na mtu maarufu lakini halikujibiwa,ngoja nami leo nirudie lile swali. Hivi ni nani huwa mshauri wa washauri wa wanao washauri viongozi wetu! Huenda halikujibiwa kwa kuwa swali labda halikueleweka.
Ushauri siku zote huwa wa aina mbili,ushauri chanya au ushauri hasi,ikiwa kila wanalofanya viongozi wetu hulifanyia kazi kwanza kwa kupata ushauri ndipo walizungumze hapo kuna mashaka makubwa,ndiyo maana nami nauliza leo ni nani huwa anawashauri washauri wanao washauri viongozi wetu.
Kauli za siku hizi zitolewazo na viongozi wetu zinasikitisha sana kama sikufedhehesha,huenda washauri wao hawafanyi kazi ya kushauri vizuri au washauri wa watoa ushauri(think tank) wa viongozi ni tatizo,na kama wanafanya kazi yao ipasavyo basi tatizo lipo kwa viongozi. Kama tatizo lipo kwa viongozi,chanzo kitakuwa wananchi ambao ndiyo waliwaweka pale bila kuwachuja sawa sawa.
Taifa linaendelea kuwa mhanga wa kauli tata za vilongola wetu, si kwa bahati mbaya laaa ,bali kwa dhamira halisi inayoongozwa na utashi wao binafsi bila kujali ustawi wa taifa na athari zitokanazo na kauli tete.
Tumekuwa tukiitwa wachochezi kwa kuwa tunaitumia haki yetu ya kikatiba kuhoji na kukosoa kwa lengo la kuwakumbusha viongozi wetu kwa kuonekana tunaichonganisha serikali na wananchi wake. Lakini wanashindwa kuelewa kauli na matendo yao yanatosha kuwa kichocheo cha chuki dhidi ya serikali wanayoiongoza. Ndiyo maana napata shaka juu ya washauri hawa.
Ushauri una Tabaka mbili,moja kukubaliwa na mbili kukataliwa. Ikiwa ushauri wao mzuri hausikilizwi basi tuna tatizo kama taifa. Viongozi wasio hambilika na wasio shaurika ni tatizo kwenye taifa, ndiyo maana kwenye majonzi huongea kejeli na kwenye burudani huleta huzuni.
Tuna kazi kubwa sana kuzirudisha fikra zetu kwenye usahihi wa kuziwajibisha zifanye kazi ipasavyo,ni kauli ya Mungu ndiyo sahihi ikisema iwe inakuwa lakini kauli za binadamu zisipo tazamwa kwa umakini huweza kusababisha maangamizi,tujitazame,tujisahihishe taifa letu litajengwa na wale tu wenye moyo safi.