Nani mwenye jukumu la kulipa kodi Nchi hii?

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,191
13,831
Mtikisiko nguo kuchanika unaoendelea Bungeni sasa hivi unaoendeshwa na wabunge waliobaki wa CCM kwa hakika unashangaza.

Pendekezo la bajeti iliyosomwa na Waziri wa Fedha Dr Mpango inaelekea kupata mkwamo ambao haukutarajiwa kutoka kwa wabunge.
Swala ni wazi, wabunge wetu hawataki kulipa kodi!!

Ni swala la kusikitisha kwa maana kodi imekuwa iklipwa karibu na kila mwananchi apataye kipato cha aina yoyote ile.

Sasa wabunge wetu kuataa kulipa kodi, swala linakuja.

Je? Nina nani akatwe kodi ili wabunge walipwe mishara na mafao yao minono?
Huku mitaani, heri ukutane na polisi kuliko hawa jamaa wasaka kodi na mawakala wao wa TRA.

Sina haja ya kuweka mafao ya wabunge hapa jamvini lakini kwa jinsi wananchi wengi wanavyogombea vyeo hivyo wakati wa uchaguzi, mafao hayo si madogo.

Wabunge wetu, hasa wa CCM wajiulize vizuri na kwa umakini wa dhati kabisa,

Nani ana jukumu la kuwalipa kipato chao kisichokatwa kodi?
 
Mtikisiko nguo kuchanika unaoendelea Bungen sasa hivi unaoendeshwa na wabunge waliobaki wa CCM kwa hakika unashangaza.
Pendekezo la bajeti iliyosomwa na Waziri wa Fedha Nd Mpango inaelekea kupata mkwamo ambao haukutarajiwa kutoka kwa wabunge.
Swala ni wazi, wabunge wetu hawataki kulipa kodi!!

Ni swala la kusikitisha kwa maana kodi imekuwa iklipwa karibu na kila mwananchi apataye kipato cha aina yoyote ile.
Sasa wabunge wetu kuataa kulipa kodi, swala linakuja.
Je? Nina nani akatwe kodi ili wabunge walipwe mishara na mafao yao minono?
Huku mitaani, heri ukutane na polisi kuliko hawa jamaa wasaka kodi na mawakala wao wa TRA.

Sina haja ya kuweka mafao ya wabunge hapa jamvini lakini kwa jinsi wananchi wengi wanavyogombea vyeo hivyo wakati wa uvhaguzi, mafao hayo si madogo.

Wabunge wetu, hasa wa CCM wajiulize vizuri na kwa umakini wa dhati kabisa,
NANI ANA JUKUMU LA KUWALIPA KIPATO CHAO KISICHOKATWA KODI?

Kama wakikataa rais avunje bunge hao wabinafsi wakatafute ajira isiyo na kodi. Awakumbushe Mwl Nyerere alichofanya 1973 wabunge walipopinga muswada wa kodi ya mapato. Wabunge walikuwa hawakatwi kodi ya mapato kutoka kwenye mishahara yao na sasa wanakatwa.
 
Mtikisiko nguo kuchanika unaoendelea Bungen sasa hivi unaoendeshwa na wabunge waliobaki wa CCM kwa hakika unashangaza.
Pendekezo la bajeti iliyosomwa na Waziri wa Fedha Nd Mpango inaelekea kupata mkwamo ambao haukutarajiwa kutoka kwa wabunge.
Swala ni wazi, wabunge wetu hawataki kulipa kodi!!

Ni swala la kusikitisha kwa maana kodi imekuwa iklipwa karibu na kila mwananchi apataye kipato cha aina yoyote ile.
Sasa wabunge wetu kuataa kulipa kodi, swala linakuja.
Je? Nina nani akatwe kodi ili wabunge walipwe mishara na mafao yao minono?
Huku mitaani, heri ukutane na polisi kuliko hawa jamaa wasaka kodi na mawakala wao wa TRA.

Sina haja ya kuweka mafao ya wabunge hapa jamvini lakini kwa jinsi wananchi wengi wanavyogombea vyeo hivyo wakati wa uvhaguzi, mafao hayo si madogo.

Wabunge wetu, hasa wa CCM wajiulize vizuri na kwa umakini wa dhati kabisa,
NANI ANA JUKUMU LA KUWALIPA KIPATO CHAO KISICHOKATWA KODI?

Utashangaa JPM anadeal na wapinzani wanaomshauri posho ziondolewe. Anaacha kutumia uzalendo wa kuwasuport. Hapo naona kama magu anateleza.

Hivi hawa wabunge ccm wanataka nani awalipie kodi? Au wanafikiri kodi hushuka kutoka mbinguni? Wasipolipa maana yake wewe mlalahoi ndio utakayewalipia kofi. Je sisi ndio tuliwaomba wagombee huo ubunge?

Da ingekuwa hapa ni korea kaskazini wangenyong........ maana ni wahujumu uchumi
 
Asilimia kubwa wabunge wetu wanagombea kutafuta hela huko. Ni aina ya ajira kwao.
 
Walipe kodi kama sisi hawako juu ya sheria
Kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi wa nchi hii.
Wabunge kutolipa kodi ni sawasawa na kutaka kutumikiwa, wajijue kuwa wamechaguliwa ubunge ili kutumikia wananchi na si vinginevyo.
Ati ooooh wana michango mingi, mara majimboni wanatakiwa kuchangia shida binafsi wa wananchi!
Kwani walipoiomba kazi hiyo hawakuijua?
 
Mkuu kama wanaichukulia hiyo kazi kama ajira , wakumbuke kuwa hata wafanyakazi wa chini kabisa wanatozwa kodi.
Hakuna namna, lazima walipe kodi.

Ni kitu cha ajabu wao wenyewe ndiyo wawe waamuzi wa kuamua kama walipe kodi au la. Haki hiyo wakipewa watu wote, nani atalipa kodi nchi hii?
 
wote ni wananchi Wabunge wajishushe tu,
kuna wananchi makampuni yanawapunguza, au kufungwa na kila kipato chao kama kiinua mgongo wanakatwa tena kwa asilimia kubwa tu. tena hata kama mtu alikuwa namillion 10 anaishia kupata million saba huku akiondoka anajua uwezekano wa kuajirika haupo na anategemewa nyumbani au ukoo in daily basis. Hajawahi kulalamika, kuandamana wala hata kukufuata maana aliamini ni sehemu ya uzalendo japo inauma. Sasa muwakilishi unapoanza kujitetea badala ya kuwatetea waliokutuma kwa tatizo hilohilo sio sawa.Pia sio sawa unapoambiwa wewe ukatwe unatoa visingizio "kama vipi wakatwe watumishi wote" kana kwamba unakomoa. Onyesha commitment yako kwa Taifa, Mungu atakufanikisha kama ukiwa mkweli hata kama ukiacha ubunge HUtakuwa ombaomba
 
Si kila mtu! Ni yule sheria zinasema alipe kodi.....si tuliona watu wakipata bidhaa bila kodi, wengine wanapata mishahara bila kulipa kodi...ndio ilivyo hivo...sheria!
 
wote ni wananchi Wabunge wajishushe tu,
kuna wananchi makampuni yanawapunguza, au kufungwa na kila kipato chao kama kiinua mgongo wanakatwa tena kwa asilimia kubwa tu. tena hata kama mtu alikuwa namillion 10 anaishia kupata million saba huku akiondoka anajua uwezekano wa kuajirika haupo na anategemewa nyumbani au ukoo in daily basis. Hajawahi kulalamika, kuandamana wala hata kukufuata maana aliamini ni sehemu ya uzalendo japo inauma. Sasa muwakilishi unapoanza kujitetea badala ya kuwatetea waliokutuma kwa tatizo hilohilo sio sawa.Pia sio sawa unapoambiwa wewe ukatwe unatoa visingizio "kama vipi wakatwe watumishi wote" kana kwamba unakomoa. Onyesha commitment yako kwa Taifa, Mungu atakufanikisha kama ukiwa mkweli hata kama ukiacha ubunge HUtakuwa ombaomba
Ni tatizo kubwa kwa baadhi ya viongozi wetu.
Wengi wao wanaona kama kulipa kodi ni jukumu la wengine si wao wenyewe.
 
Tz kuna ubaguzi sana katika ulipaji kodi, kuna exemption za ajabu ajabu tu, iletwe sheria itayolazimisha kila mtu kulipa income tax kuanzia kwa Rais hadi mtumisha wa chini, tofauti iwe ni rate tu.

Vilevile suala la posho kama wanakata kodi wakate kwa watu wote, wabunge na wafanyakazi wa serikali posho zao hazina kodi wakati wafanyakazi sekta binafsi posho zao zinalimwa kodi, hivi hizi vyama vya wafanyakazi wanashindwa kuvalia njuga mambo ya wazi kama haya.
 
Ni tatizo kubwa kwa baadhi ya viongozi wetu.
Wengi wao wanaona kama kulipa kodi ni jukumu la wengine si wao wenyewe.

Jukumu la kulipa kodi na la kwetu makapuku wao waheshimiwa kazi yao kuitumbua kodi yetu.Ndugu yangu tulipokosea ni pale tulipokubali kubaguliwa wachache waitwe waheshimiwa wengi tuitwe Malofa au Vilaza.
 
Ni tatizo kubwa kwa baadhi ya viongozi wetu.
Wengi wao wanaona kama kulipa kodi ni jukumu la wengine si wao wenyewe.
Magu amuombe waziri wake apeleke mabadiliko ya bidhaa ya vifungu vya Katiba kuhusu kodi, exemptions za income tax isiwepo, Rais, mawaziri na wabunge waanzie kuchangia kodi na wao ili uchungu tuusikie wote wakiweka rate mbovu mbovu.
 
nyerere alisha waambia na mkawa mnaimba kwamba nchi hii ni ya wakulima na wafanyakazi so hawa ndo wanakatiwa kulipa kodi
 
Magu amuombe waziri wake apeleke mabadiliko ya bidhaa ya vifungu vya Katiba kuhusu kodi, exemptions za income tax isiwepo, Rais, mawaziri na wabunge waanzie kuchangia kodi na wao ili uchungu tuusikie wote wakiweka rate mbovu mbovu.
Viongozi wetu wakijua uchungu wa kulipa kodi pengine wstsitumia kodi hiyi vizuri.
 
Nilimsikiliza Mbunge mmoja nadhani wa Sumbawanga yule, akimwambia Waziri wa fedha na Mipango eti amefanya hivyo kwa sababu hajui uzito wa jimbo, eti hizo pesa zikikatwa kodi utawaumiza wananchi, upuuzi mtupu. Sasa mimi namwambia hizo pesa zikikatwa kodi zitawarudia wananchi vizuri zaidi kupitia huduma za jamii kama madawa, kusomesha watoto wao, barabara nk.

Maneno kama yale ya Ndg, Mheshimiwa samahani ningeyasikia kwa ndg yangu wa kijijini ambaye hata shule ni kuunga, nisingeshangaa hata kidogo maana uelewa wake ndio hapo unapoona, sasa Mbunge ambaye anaishauri serikali mambo mbalimbali ya kiuchumi, kisheria nk, lakini inaonesha hajui hata wajibu wake.

Haiwezekani mpitishe sheria ya kumtoza kodi mfanyakazi wa ngazi ya chini anayesitafu akiishia kupata kiinua mgongo cha milioni 40 mfano, baada ya kuwa ameitumikia nchi yake kwa uadilifu mkubwa kabisa kwa zaidi ya miaka 30, na pia unatunga sheria nyingine ya kutomkata kodi Mh Mbunge aliyetumikia nchi kwa miaka 5 tu huku akilipwa mshahara mkubwa, marupurupu kibao, na analipwa zaidi ya 200milioni pasipo kodi.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Kataeni kupitisha bajeti rais avunje Bunge turudi kwenye uchaguzi tuone, maana hamna namna nyingine. Mnadai pesa kubwa kwa mambo yenu binafsi na huku mnadai maendeleo majimboni kwenu, mnataka serikali itoe wapi pesa kwa ajili ya huduma za jamii, kama maji, afya, shule, umeme nk zitatoka wapi kama sio kodi.
 
Nilimsikiliza Mbunge mmoja nadhani wa Sumbawanga yule, akimwambia Waziri wa fedha na Mipango eti amefanya hivyo kwa sababu hajui uzito wa jimbo, eti hizo pesa zikikatwa kodi utawaumiza wananchi, upuuzi mtupu. Sasa mimi namwambia hizo pesa zikikatwa kodi zitawarudia wananchi vizuri zaidi kupitia huduma za jamii kama madawa, kusomesha watoto wao, barabara nk.
Maneno kama yale ya Ndg, Mheshimiwa samahani ningeyasikia kwa ndg yangu wa kijijini ambaye hata shule ni kuunga, nisingeshangaa hata kidogo maana uelewa wake ndio hapo unapoona, sasa Mbunge ambaye anaishauri serikali mambo mbalimbali ya kiuchumi, kisheria nk, lakini inaonesha hajui hata wajibu wake. Haiwezekani mpitishe sheria ya kumtoza kodi mfanyakazi wa ngazi ya chini anayesitafu akiishia kupata kiinua mgongo cha milioni 40 mfano, baada ya kuwa ameitumikia nchi yake kwa uadilifu mkubwa kabisa kwa zaidi ya miaka 30, na pia unatunga sheria nyingine ya kutomkata kodi Mh Mbunge aliyetumikia nchi kwa miaka 5 tu huku akilipwa mshahara mkubwa, marupurupu kibao, na analipwa zaidi ya 200milioni pasipo kodi. Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Kataeni kupitisha bajeti rais avunje Bunge turudi kwenye uchaguzi tuone, maana hamna namna nyingine. Mnadai pesa kubwa kwa mambo yenu binafsi na huku mnadai maendeleo majimboni kwenu, mnataka serikali itoe wapi pesa kwa ajili ya huduma za jamii, kama maji, afya, shule, umeme nk zitatoka wapi kama sio kodi.
Halafu watu na akili zao wanataka wasilipe kodi!
Siasa siyo ajira, wajifunze kuishi maisha wanayoyatetea bungeni.
 
Kwa kweli nitashangaa serikali inayosema inawatetea masikini, halafu inawaacha hawa wanaolipwa fedha lukuki na serikali hiyo hiyo wasilipe kodi!
 
Hoja ikipanuka zaidi wabunge hawatotakiwa kulipa kodi, iwapo, viongozi wengine wenye vyeo vya kisiasa hawatolipa kodi.

Sheria ni msumemo. Lazima ikate kotekote. Hiyo itawagusa kuanzia:Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu,Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya.
 
Back
Top Bottom