Wanajamvi habar za wakat huu? natumai wengi wenu hali zenu ni njema na mnaendelea kulijenga taifa hili kwa moyo wa uzalendo na wenye kutukuka.
twende moja kwa moja kwenye somo tajwa hapo juu, hivi kati ya hawa wanaojiita wayahudi na waarabu nani mwenye haki katika nchii inayoitwa israeli? nikirejea kwenye kitabu kitakatifu biblia napata majibu ya swali langu kwamba hawa wanaojiita wayahudi na waarabu hawana haki katika nchi hiyo wote ni wavamizi tu walianza kuvamia waarabu miaka 2000 iliyopita na akaja hawa wanaojiita wayahudi wakaivamia rasmi mwaka 1948, hivi vita vilivyopewa jina la israel-palestina vitakuwepo baina yao daima kwa sababu kila mmoja baina yao anajua siri ni nani alikuwa na haki katika nchi ile kwa hiyo atakae kuwa na nguvu ndo ataweza kuimiliki nchi ile
Ongozana nami ili ujue ukweli wa mambo;
Neno la bwana likanijilia,kusema
Ezekieli6:1
mwanadamu, uelekeze uso wako uitazame milima ya israeli , ukaitabirie
Ezekiel6:3
Bwana mungu asema hivi; ni jambo baya , jambo baya namna ya peke yake ; angalia linakuja.
Ezekiel 6
Na wewe mwanadamu, bwana mungu aiambia hivi nchi ya Israel; ni mwisho; mwisho umezijilia pembe nne za nchi
Ezk 7
Ajali yako imekujilia we ukaye katika nchi hii majira yamewadia, siku ile inakrbia, siku ya fujo wala si ya shangwe milimani
Ezk 7
Nami nitapatia katika mikono ya wageni pawe mateka yao na katika mikono ya maovu wa dunia pawe mawindo yao, nao watapanajisi
Ezk 7:21
Kwa sababu hiyo nitawaleta watu wa mataifa walio wabaya kabisa nao watazimilki nyumba zao
Ezk7:24
Tena watajifungia nguo za magunia na utisho utawafunika, na aibu itakuwa juu ya nyuso zao na upaa juu ya vichwa vyao vyote
Ezk7
Nami nitanyosha mkono wangu yuu yao na kuifanya nchi kuwa mganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa dibla, katika makao yao yote,nao watajua kuwa mm ndimi bwana. Ezk
Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni na yeye aliyekaribu atakufa kwa upanga, na yeye atakayesalia na kuhusuriwa katika mji atakufa kwa njaa na hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu juu yao. Ezk 6
Kila mahali mkaapo miji itaharibika na mahali palipoinuka patakuwa ukiwa na sanamu zenu za jua zikatwe na vinyago vyenu vivunjwe na kazi zenu zifutwe kabisa ezk 6
Lakini nitasaza mabaki ,maana mtakuwa na baadhi ya watu watakao ukimbia upanga kati ya mataifa , mtakapokuwa mmetawanyika katika nchi za watu Ezk 6:8
Bwana atakupeleka wewe na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako, huko utatumikia miungu mingine ya MITI NA MAWE
Nawe utakuwa mithali na dharau kati ya mataifa tote huko atakakokuongoza bwana
NAZO ZITAKUWA JUU YAKO KWA ISHARA ZA AJABU NA JUU YA UZAO WAKO MILELE.