Nani muasisi wa Program ya Wasukuma Ulizeni?

kyalankota

JF-Expert Member
Jul 27, 2014
2,594
1,460
Ni nani muasisi na lengo lake ni nini?
Je, ni mtani wa wasukuma au?
Je, ni kweli ndivyo walivyo?
Kama ni utani kwanini wasitaniane live badala ya mitandaoni?
 
Kuna watu kwa makusudi kabisa wanataka kuikuza hii ishu ya utani kwa wasukuma, wanataka kuilazimisha ihusiane na mambo ya kisiasa, lengo lao ni kupandikiza chuki za ukabila. Watu hawa tuwapinge.

Utani ni jambo zuri tu na mimi nikiwa msukuma, hatuchukizwi na utani huo.
 
Hayo ni matani tu mtandaoni usichukulie kila kitu serious uraondoka na heart attack,
 
Kila kabila kuna wale ambao huitwa washamba, kwani huwezi kujua kila jambo.
Kwa nini kila kitu kiwe kwa wasukuma tu?
Tutajua tu mwisho wake.
 
Kila kabila kuna wale ambao huitwa washamba, kwani huwezi kujua kila jambo.
Kwa nini kila kitu kiwe kwa wasukuma tu?
Tutajua tu mwisho wake.
Utaninwa wasukuma ulianzaga zamani sana, hii ya juzi ni kuikuza tu.
Nakumbuka tulikua tukiwataniaga wasukuma kua mmoja akija Dar akanunua shati la Tshs 10,000/= basi akirudi nalo Usukumani mwenzie akamuona, nae lazima aje mjini kununua shati kama hilo tena kwa bei hiyohiyo.

Ikitokea akakuta bei imeshuka basi hawezi kununua maana atajua kua hilo lililoshuka bei litakua ni feki sio original. Hivyo atang'ang'ania kua ye anataka shati la alfu 10 kama la mwenzie. Kinachofanyika ni wajanja wa mjini kumzunguka na kumletea shati lilelile lililoshuka bei lakini kwa bei ileile ya alfu 10.

Huu utani niliusikia miaka ya 1990 na uliwahusu wasukuma tu
 
Ni kweli utani wa kimakabila upo. Lakini inapokuwa kila kabila ni mtani wa wasukuma, hapo ndo tatizo linapoanzia. Au ni kwa sababu kiongozi wa nchi anatoka usukumani? Vyovyote iwavyo inaonesha kuna watu nyuma ya kampeni hii. Lakini wasukuma haiwasumbui sana kwani utani kwao si kitu kipya.
Watajichosha wenyewe na kamoeni zao mbaya.
Hatimaye nalo litapita !
 
Back
Top Bottom