Mie nimekaa mkao wa kula nasubiri mchapo wetu na New Castle na huo wa kesho hautanipita. I hope L'pool watacheza kwa ari na siyo midabwada waliyoonyesha katika siku za karibuni.
Aibu yaoooo chezea kupakatwa wewe......hahahahaha
Simba oyeeeeeeeeeeeee......
mhhh! Ntakununia sasahv yaan hunitakii mema?
Acha kujidanganya, zinapocheza Simba na Yanga, probability kubwa huwa ni kwamba Simba itashinda, regardless iwe mbovu kiasi gani. Lakini Yanga ikiwa mbovu, matokeo huwa mabaya zaidi kwao, ndo kama yale ya 5-0Tatizo mpira wa Simba na Yanga hautabiriki.
Alafu hivi ni kwa nini wasichana na wanawake wazuri hapa bongo wote ni washabiki wa Simba? Sijawahi kuona mbaya, ila upande wa pili pale jangwani, sina la kusema!
Kitenge huwa akiiongelea Yanga kwa uchungu, utaona sauti yake kama inaelekea kukauka hivi! Jamaa atakuja kuzimia studioKitenge ni Simba?? Mbona anapenda sana kuipamba Yanga! Toka yuko redio one alikuwa akiongea mambo ya yanga anashindwa kabisa kuficha mahaba. Labda!! Ila kwa ninavyomsikiaga akiongea kuhusu simba au yanga, huwa anaonyesha mahaba makubwa sana kwa yanga.
Hahahahaha lol!!!! Sasa wewe hutaki kuona soka la uhakika ambalo litakufanya hata kiti ukione cha moto kwa dakika zotee 90!? Mie nataka kuona kandanda kama hilo hata ukishinda unajipiga kifua kwa maringo, siyo kushinda katika mechi hovyoooo midabwada mitupu mwanzo mwisho. Lini umejifunza kununa? 🙂🙂
Hao Waganda si ndio wameshindwa kuivusha nchi yao kufuzu CAN, uhatari wao uko wapi sasa? Hao Wabongo uliowataja ni wa normal sana hatuna hofu nao, Mnyama lazima afe na hiyo mechi haina sare/ suluhu alizozizoea.
mimi nataka magoli bana nikitaka burudani huwa naangalia Arsenal full kuburudika,hahahahaha!!
hahahhahahahahhahahahahahahahahaha jamani rahaaa si rahaaaaaa