Nani mmiliki wa Magari ya Serikali?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani mmiliki wa Magari ya Serikali??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMC, Jan 11, 2012.

?

hii kero ina umuhimu kiasi gani kwako katika huu mwaka

Poll closed Jan 18, 2012.
 1. Nakubali hii ni kero ya muhimu kutatuliwa kwa sasa

  100.0%
 2. Hii si kero ya muhimu kutatuliwa kwa sasa

  0 vote(s)
  0.0%
 1. M

  MAMC Senior Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wana JF, Wabongo mambo mengi tunayaona! yanatuuzi! lakini hatufanya kitu! hata kama fursa/ tuko kwenye nafasi ya kufanya kitu! kisa eti utaonekana mnoko/kauzu!!

  Japo sijafanya research, ukweli huwa hauongopi! unadadisi mdogo tu utakuonesha kuwa zaidi 30% ya magari ya Dar ni ya Serikali, na zaidi ya 70% ya magari ya gharama/kifahari hapa town yanamilikiwa na serikali.

  Hivyo basi kwa kuwa mmiliki wa hii "block" ya traffic hapa town na uenda nchi nzima ni mmoja, akiwa na ufanisi na nidhamu katika ununuzi,usimamiaji wake basi tutapata japo kau-nafuu katika magumu mengi tunayo yapata hapa Tanzania.
  Magari ya serikali yananunuliwa na kodi zetu!! Iweje madereva wake wawe wajeuri , waendeshe kihuni, na mafedhuri barabarani!! Hii si ni sawa na msemo wa “mwizi aibe then kama haitoshi pia aue mwenye shamba” – kodi tulipe then zitumike kutunyanyasa!
  Hao wenye jukumu la kusimamia magari ya serikali – bila shaka wanaweza kufanya hata hili dogo katika huu mwaka “masiha yako chaguo lako”

  Na kama mna simamia basi hatuoni - hairizishi!! Hata ku-copy “best practice” saa nyingine ina ruhusiwa – iga hata makaburu [tbl, coca cola,nk) , teknolojia inaruhusu!! kila gari ya serikali weka tangazo “ KAMA DERVA ANAENDESHA VIBAYA AU KAPAKI SEHEMU MBAYA [e.g bar, Gest,sokoni] PIGA NAMBA HII XXXX] uone jinsi wasamalia wema watakavyo wafukua hao wanao abuse “Mali ya Umma”

  Hili haliitaji mzungu, wala semina, wala PPRA mana kizingizio siku hizi ni PPRA process!!

  Ieleweke kuwa tunasema si kwa sababu ya umbea, ni kwa sababu tunaipenda nchi yetu, kama kila mtu akisema anajijali lwake, ajue ni kama kurusha mavi angani, lazima baadhi yatakuangukia tuu!

  mfano mzuri ni hali ya dala dala, maguta, bajaji barabarani hivi sasa!! naamini kero zake [kuchomekewa, kupigwa pasi, kutukanwa, simama ghafla, n.k] zinawakuta balabala! kwenye ma - vogue yao - hata wale waliokuwa na dhamana ya kuweka mfumo bora wa usafiri waumma mijini, bali wakachagua kutofanya!!
   
Loading...