Mkuu, awali ya yote ni vema ukatofautishwa rushwa ndogo ndogo wafanyazo waganga njaa katika kujiongezea kipato na Grand corruptions inayotafuna nchi na kupalilia umasikini ktk nchi hii Tajiri kwa Rasilimali za kila aina tuliyopewa na Muumba wa Ardhi na Mbingu. Wafanyakazi na watumishi wengi wa umma huwa wana program inajulikana kama salary maintenance kwa kuwa serikali hupretend kuwalipa mishahara isiyoendana na hali halisi ya maisha... Tofauti na Grand corruptions ambapo unakuta syndicate inaliingiza nchi kwenye madeni ya matrillion na hatimae kuishia kusaini mikataba ya kishenzi kuruhusu maliasili zetu kuvunwa bure bure kwa msaada wa watu wa nchi wahisani/washirika wa kimaendeleo!!! Hapa Tanzania sekta zote zimejaa rushwa kubwa kubwa ili wanazidiana kulingana na ukwa wa deals, Kwa mtazamo wangu Wizara ya Nishati na Madini inaongoza wakifuatiwa kwa karibu sana na Ujenzi, Fedha, Usafirishaji, Ardhi, Uvuvi, Maliasili na Utalii, Ulinzi, tawala za mikoa ...ya mwisho kwa kuhujumiwa ni EA, Muungano na Elimu...Kwa ujumla matatizo yetu yako zaidi katika uongozi, mfumo na uendeshaji usiokuwa zingatia kuwajibika na uwajibikaji...