Ni Tanzania tu ndiko elimu inadogoshwa na kuonwa kama njia ya kutajirikia. Elimu na utajiri havina uhusiano wa moja kwa moja ndiyo maana matajiri wengi duniani hawana elimu sana japo biashara zao zinaendeshwa na wenye elimu. Ni mawazo haya haya ndiyo yanayofanya tushindwe kuondokana na ufisadi kwa sababu kila anayepata kanafasi anataka aibe haraka haraka atajirike ili asije kuchekwa kwamba elimu yake haijamsaidia. Na kama jamii, hatutakaa tupige hatua mpaka tutakapoachana na mawazo haya.
Nenda kwenye nchi zilizopiga hatua huko ukaone hasa nini lengo la elimu. Si ajabu kumkuta profesa mashuhuri sana na aliyeandika mavitabu yanayotumika duniani kote anaishi maisha ya kawaida tu na anakwenda kazini kwa baisikeli au ki Corolla chake cha mwaka 2000. Kazi yake kubwa na wajibu wake kwa jamii ni kufanya utafiti na kuandika mawazo yake kwa ajili ya vizazi vijavyo. Na jamii inamheshimu sana kwa mchango wake huo.
Kama lengo lako ni kutajirika basi usisome sana utapoteza muda. Elimu ya form 4 au 6 inakutosha; japo napo hakuna guarantee kwamba utatajirika.
Maisha mnayakompuliketi mno ndiyo maana mnafikia mpaka mnashindwa kuyaishi na kuyafurahia. Wasomi wetu leo wameacha jukumu lao na kila mmoja anakimbilia siasa kwa sababu huko ndiko kuna utajiri wa haraka haraka. Na huko atafisadika weee ili tu usomi wake uonekane. Kama jamii tumepotea!