Nani malaya kati ya mwanamke na mwanaume

Nani malaya kati ya mwanamke na mwanaume

lazima ukae

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2013
Posts
791
Reaction score
417
Habari zenu wanajamvi.

Kwa miaka ya hivi karibuni kumekua na kesi nyingi za wapendanao hasa wale ambao tayari wameshafunga pingu za maisha kuchepuka toka njia kuu na kuwa wapenzi wengine wa pembeni.

Katika nyumba nyingine unaweza kuta mama ndie anaekosa uaminifu kwenye ndoa wakati baba haangaiki na michepuko au unaweza kuta baba ndie anayehangaika na michepuko wakati mama hana hayo mambo ya michepuko.

Ukimuuliza mwanamke atakuambia kwamba wanaume ndio wanaoongoza kwa kutokua waaminifu kwenye ndoa wakati ukimuuliza mwanaume nae atakuambia kwamba wanawake ndio ambao hawatulii kwenye ndoa zao.

Napata mtihani kujua jinsia ipi ndio inayoongoza kwa kutokua na uaminifu kwenye ndoa ndio maana leo nimeona niilete hii kwa great thinkers ili tujue ukweli uko wapi.

Karibuni wanajamvi tuweze kupata mawazo tofauti tofauti.
 
Habari zenu wanajamvi,

Kwa miaka ya hivi karibuni kumekua na kesi nyingi za wapendanao hasa wale ambao tayari wameshafunga pingu za maisha kuchepuka toka njia kuu na kuwa wapenzi wengine wa pembeni.

Katika nyumba nyingine unaweza kuta mama ndie anaekosa uaminifu kwenye ndoa wakati baba haangaiki na michepuko au unaweza kuta baba ndie anayehangaika na michepuko wakati mama hana hayo mambo ya michepuko.

Ukimuuliza mwanamke atakuambia kwamba wanaume ndio wanaoongoza kwa kutokua waaminifu kwenye ndoa wakati ukimuuliza mwanaume nae atakuambia kwamba wanawake ndio ambao hawatulii kwenye ndoa zao.Napata mtihani kujua jinsia ipi ndio inayoongoza kwa kutokua na uaminifu kwenye ndoa ndio maana leo nimeona niilete hii kwa great thinkers ili tujue ukweli uko wapi.

Karibuni wanajamvi tuweze kupata mawazo tofauti tofauti.

hili swali ni sawa na kuuliza kuku na yai kipi kilitangulia.
 
Hivi mleta mada, mtu akikuadithia "amepita sehemu fulani akawaona malaya" hautoweza kujua jinsia yao?
 
Malaya ni mwanamke anayefanya ngono na wanaume zaidi ya mmoja!
 
Umalaya ni kama rushwa. Lazima awepo mtoaji na mpokeaji. Umalaya hivyo hivyo. Lazima awepo malaya mtoaji na malaya mpokeaji!
 
wanafanya umalaya na nani?

mwanaume ki-asili ni ruksa kuwa na mahusiano ya kingono na zaidi ya mwanamke mmoja. Ila mwanamke si ruksa kuwa na mahusiano ya ki-ngono na mwanaume zaidi ya mmoja. Na akikiuka hila anakuwa malaya.
 
yoyote anaweza kuwa malaya.. wait! ngoja nijibu hv.. wanawake malaya na wanaume malaya pia
 
Huyu katoa maana yake
 
Attachments

  • 1422790009635.jpg
    1422790009635.jpg
    49.4 KB · Views: 1,452
Kiasili me anauwezo wa kuweka mimba kwa zaidi 1 lakini ke hawezi pokea mimba ya zaidi 1 ndo mana akaitwa malaya kwakua anafanya bila faida
 
mwanaume ki-asili ni ruksa kuwa na mahusiano ya kingono na zaidi ya mwanamke mmoja. Ila mwanamke si ruksa kuwa na mahusiano ya ki-ngono na mwanaume zaidi ya mmoja. Na akikiuka hila anakuwa malaya.

Ruksa ilitolewa na nani?
 
Mwenyezi Mungu aliagiza watu waoane ili kutimiza haja za maumbile yao...hakuamrisha watu kuonjana kama kuku...au kudinyana hovyo.....
Mtu yoyote anayeshiriki ngono na mtu ambaye hakuidhinishwa naye kisheria nikiwa namaanisha ndoa...huyo mtu moja kwa moja ni malaya..haijalishi awe mwanamke au mwanamme kwani lile tendo hukutanisha watu wawili.....
 
Kwa tafsiri ya kikamusi:Malaya ni mtu yeyote mwanaume au mwanamke anayefanya mapenzi kwa kuyanunua au kuyauza.source Mackie hassan wa baraza la kiswahili.
 
Me naona walokole ndiyo wanaaongoza kwa umalaya kwa kivuli cha mikesha. Umalaya ni akili ya mtu, na ni katabia fulani mtu anakuwa nacho kutokana na mazingira anayokuwa nayo.
 
Umalaya ni matendo/tabia kama matendo mengine,wote wanaume na wanawake wanaweza kuwa malaya!
 
Back
Top Bottom