Nani kauza tiketi zaidi ya uwanja?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Usalama wa watanzania ulikaribia kuhatarishwa na wale wote waliouza tiketi nyingi mno kuliko uwanja za kuingia uwanja wa mkapa kuangalia mechi ya taifa stars v Uganda. Hii ilikuwa na malengo gani? Kuibia watu? Kuua watu? Kuumiza watu, kusababu wasitii Sheria bila shuluti au nini?

Watu hawa wachukuliwe hatua haraka
 
yaani mpka jana ticket zinazoreport TRA EFD department... ni kama ustadhi na kitu moto😁😁😁 jana kuna watu wamepiga hela za kula bata mpka june 30 2019
 
Walikua wanatafuta hela ya kuwalipa kamati na posho,pole ziende kwa walio umia kwa kuvunjika natauma salamu za rambirambi kwa familia iliyompoteza mtoto wao,so sad.
 
Bongo mambo uwa hayaishi salama ,bila figisu figisu mara hivi mara vile.

Mara watu wamekanyagana , mtoto kupoteza maisha ,inasikitisha sana.

Alafu wazazi nao tujifunze wakati mwingine ,kama kuna ulazima wa kupeleka mtoto sehemu kama ile chochote chaweza kutokea .
 
Mjini shule. Watu wanaishi mjini kwa mission town. Ni mwendo wa kutumia fursa. Ngoja tuone iwapo sheria itachukua mkondo wake au wataachwa tu waendelee na hizo dili zao mbovu.
 
Pole kwa familia iliyopoteza mtoto, kiukweli uwanja wa taifa mechi kubwa usalama ni mdogo sana. Mimi alimanusura nipoteze mtoto siku ya Nkana fc na Simba, na niliapa sitakaa nirudie tena kwenda na mtoto taifa. Haswa wakati wa kuingia na kutoka, no shida sana.
 
Lile genge la wasanii waliopewa ticket Za Bure kugawia Wananchi usishangae walipewa Na Za Magendo kuuza

Watu Kama elf 30 walikuwa Nje ya Uwanja wakati ndani washajaa watu elf 63
 
Lile genge la wasanii waliopewa ticket Za Bure kugawia Wananchi usishangae walipewa Na Za Magendo kuuza

Watu Kama elf 30 walikuwa Nje ya Uwanja wakati ndani washajaa watu elf 63
Unaweza kuthibitisha pasi na shaka kuwa hao elf 30 walikuwa na tiketi??Unaendaga uwanjani??unajua kuna watu huwa wanaenda uwanjani wakiwa hawana hela ya kiingilio wala tiketi lakini wanataka kuingia??unajua kitu kinaitwa Fungulia mbwa??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom