Nani kakosea mahesabu, ni Spencer Lamek wa ITV au Rais Pombe Magufuli?

dansmith

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
2,305
2,094
Baada ya Rais JPM Kumaliza kutangaza baraza lake fupi la wachapa kazi km anavyooliita alirushu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.swali Minamoto utata ni lile aliloulizwa na Spencer lamek wa ITV kuwa mbona baraza lake lina sura zile zile zimerudi kama sura kumi hv.MH Rais alimkosoa kwa kujiamini kuwa lameki h?ta hesabu kakosea walirudi ni 7 tuu sio 10 .hebu tujikumbushe waliokuwa awamu ya nn tena ya mwisho na wamerudi tena ili kujua nani alikuwa sahii mimi ninaowakumbuka ni wafuatao
1January makamba
2 Mwigulu nchemba
3 William lukuvi
4 Harrison mwakyembe
5 Ummy mwalimu
6 Hussein mwinyi
7 Jenista mwagama
8 George simbachawene
9 Charles kitwanga
10 Charles mwijage
11Makame mbarawa
NB : sospeter Muhongo sijamuhesabu tunajua yaliyotoke.swali nani alikosea kupiga mahesabu ni Spencer lamek au jpm .na Sitaki kuamni ni jpm kwa maana jamaa kwa hesabu na kukariri hafai
Nasilisha km na mimi nimekosea nikosoeni
 
Naona bado mnaendelea kujifariji!!

Hivi uchaguzi si umepita?
 
Kama ndivyo basi ni kwamba, machoni mwa Magufuri, wale ambao walikuwa manaibu waziri wakati wa JK hawakuwa Mawaziri lakini waliokuwa mawaziri ambao wamerudi ndo hao 7!!!! Kwamba, Nchemba; tupa kule... alikuwa naibu; Ummy, tupa kule... Kitwanga na Mwijage.... wote tupa kule; hawakuwa mawaziri bali ni manaibu!!
 
Magufuli alimaanisha waliokuwa mawaziri kamili kwenye awamu iliyopita na pia wamekuwa mawaziri kamili kwenye awamu hii ambao ni Jenista Mhagama, George Simbachawene, William Lukuvi, Mak?me Mbarawa, Sospeter Muhongo, Harrison Mwakyembe na Hussein Mwinyi. Hao wengine walikuwa ni manaibu waziri.
 
Alimaanisha mawaziri au manaibu?
Tuanzie hapo then tuendelee.
Hivi Dada Ummy alikua waziri wa nini?
 
Inasikitisha sana pale mtu unaposhindwa kutambua muundo wa Serikali katika kila Ngazi na unaanza maneno tena ambayo hayatusaidii na wala sio kipaumbele cha wa TZ kwa sasa.

Kwa kifupi swali liliuliza idadi ya Ma Waziri wa Serikali ya JK. Ina maana hujui kuwa kuna Ma Waziri na Ma Naibu Mawaziri???? Ulikimbia darasa la DS???

Penda kuanzisha mada zenye kujenga hapa ni jukwaa la GT's.

Queen Esther
 
Kwenye cabinet(baraza la mawaziri) naibu waziri haesabiwi kama member wake, kwahiyo mhe. Rais huenda alitumia sababu kama niliyoisema kumjibu mwandishi lameck.
 
Magufuli yuko sawa walio rudi kama mawaziri ni saba..!
 
Swali Minamoto???, h?ta??, Nasilisha?? Makosa ya kuandika yakizidi unaonekana mjinga.
 
Back
Top Bottom