Nani ilimkututa kama hii

Usiombe mkuu kuna wakati niliitwa kutoa morning speech, sa ile nimefika mbele kila mtu nkaona ananishangaa km ktuko flani ila vile nilivyodeliver content hakuna aliyeamini. Bt inferiority complex ilinidominate sana.
Mimi there was a time sikua na nguo za home
Wakati nikiwa primaly.
Nilidharaulika sana.marafiki walinisema vibaya.
Yani sikuiz nazinunua mno nadhani nilikua affected
 
Niliwahi kuwa na demu mkali, halafu mambo safi kwao. Siku moja akanikaribisha kwa famlia yao jioni kwa ajili ya chakula, mwanaume nikaoga safi, nikapiga pamba, nikaibuka ukweni. Tukiwa sitting tuanangalia tv, nikagundua watu wananon'gonezana kitu kisha wanaiangalia wanacheka sana kicheko kile cha kuvunja mbavu, dada zake demu na kaka zake na ndugu wengineo, wazazi hawakuwepo. Tukaenda dining kupata msosi, hali ya kicheko ipo pale pale. Nikajua wamefurahi tu miye kuwepo. Ila dem hakuwa na furaha, sikujali, (nadhani simu zingeshamiri kwa kipindi kile angenistua kwa sms). Badae nikaaga, nikasindikizwa ila demu hakuniambia kitu.

Nafika home flesh, stori za hapa na pale mara aunt yangu akaniuliza" hilo shati umevaaje? ".kujicheki kumbe nimeligeuza aisee na nilivaa tai ya kipepeo. Ile mikunjo ya shati kwa ndani imesimama hatari. [emoji849][emoji849][emoji849]. Nikawaza, niksunganisha doti, kumbe ndo mana ukweni walikuwa wananicheka! Nilifedhaika sana[emoji26][emoji26][emoji26], toka siku hiyo na mapenzi na yule dem yalifia pale, sikutaka hata kumuangalia usoni. Ingawa aliumia sana.
 
hahahahaha!nacheka lkn inahuzunisha sana daaa!
 
Uliambiwa tangu mwanzo usimwamvie mtu yoyote lakini wewe ukapuuza ukamwambia huyo unaemwita mjomba bila kujua kumbe ni shangazi
 
Pole sana mkuu. Magumu uliyopitia yalikupa ujasiri wa kusoma kwa bidii ili utoke kwenye maisha ya shida uliyokua nayo. Halafu kuna wanafunzi wanapewa kila kitu kwao wakifika shule wanacheza tu na kukua.
 
Ndo hapo unaweza jiuliza sijui why mungu anawanyjma watu wenye uhitaji na kuwapa wasio na uhitaji.
Lkn ukirud nyuma unagundua Mungu bado anakupenda na kakundalia mamb mazur kwa mbele kikubwa ni kukaza.
 
Haya maisha yanatokea mbali ,
Nakumbuka Nisha vaa tishet kiuko Kama surual ili kusubiria surual zikauke ndio nivae vuta picha kola ya tishet ipite kiunoni alaf uivae Tena kama tishet iyo kola inaukua hatari ndio maana sijawai Cheka mtu kwa mavazi maana najua nilikopitia
 
Ndo hapo unaweza jiuliza sijui why mungu anawanyjma watu wenye uhitaji na kuwapa wasio na uhitaji.
Lkn ukirud nyuma unagundua Mungu bado anakupenda na kakundalia mamb mazur kwa mbele kikubwa ni kukaza.
Kukaza Na kujituma. Wakati Niko Kidato cha tatu nilipitia hali mbaya Sana nyumbani. Sehemu pekee ya kupata faraja ilikua shule. Nilisoma kwa bidiii sana kwa sababu ya Yale maisha niliyoyapitia. Namshukuru Mungu bidii yangu haikuniangusha.
 
Usiombe mkuu kuna wakati niliitwa kutoa morning speech, sa ile nimefika mbele kila mtu nkaona ananishangaa km ktuko flani ila vile nilivyodeliver content hakuna aliyeamini. Bt inferiority complex ilinidominate sana.
Acha kabisa kaka! Mpaka namaliza darasa la saba, sikuwahi kuvaa viatu!

Japo nilikuwa na akili sana darasani ila nlikuwa sijiamin kutokana na wenzangu wote darasa zima wana viatu mie sina.

Kile kipindi huwa kinajirudia akili mwangu mara kwa mara..

Ee Mungu nisaidie wanangu utakaonijalia wsiishi maisha kama yale.
 
Hahahaaa acha utani mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…