Nani awatete wahusika wa mtoto wa Box?

Nani awatete wahusika wa mtoto wa Box?

Stream line

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2015
Posts
393
Reaction score
243
Ijulikane kuwa wahusika wa,mtoto wa box wamefungwa kwa miaka 15. Kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Naapa mbele ya Yasu Eloi wetu Jaji Feleshi hakitoa hukumu ya haki na ya kitaalamu au kisayansi ya sheria.

Kwanini nasema hivyo; haihitaji kujua kuwa mtoto wa box ameishi ktk mazingira hayo kwa mda labda wa miaka yote lakini hakufa!

Iweje leo anapotolewa ktk mazingira hayo mtoto wa box anafariki!

Ushauri wangu; Adhabu yao ya kusababisha mateso ndiyo ilikuwa haki yao ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Mfano, ni dhahiri mtoto alikuwa akijisaidia, na ni lazima ilikuwa kazi kweli ili kumsafisha, hayo ni mateso.

Nani basi aliyemuua mtoto wa box; ni dhahiri aliyemuua mtoto huyo ni wale waliomtoa ktk mazingira yake zoefu na kumpeleka ktk mazingira mapya bila kuzingatia sayansi ya mazingira.

Mfano. Tuitazame hali ya wachimba madini waliookolewa huko Amerika ya Kusini.

Wale waliandaliwa mazingira (chumba maalumu) kilichofanana na kule shimoni walipokuwa.

Mifano ni mingi, kuwa ukimtoa mtu ktk mazingira aliyoyazoea kwa ghafla basi tegemea mtu huyo kufa. Asante.

Mwisho nashauri waokozi wa mtoto Nasra wachukuliwe hatua kali sana kisheria ili kwamba kitu kama hiki kikitokea bali ile sayansi tuliyojifunza mashuleni ifanye kazi na si kukimbilia kufanya kama waliyoyafanya kwa Nasra na kumtisha kwa midoli mtoto asiyeijua midoli.
 
niliangalia taarifa ya habari jana na kugundua hawa wazazi wamefungwa kwa uzembe wao, coz et mahakama iliwataka wakubali shitaka la kuua bila kukusudia baada ya kubalishwa kwa shitaka lao la mwazo la ukiukaji wa haki ya binaadamu kwa kusababisha mateso ya mtoto wao huyo wa box
 
niliangalia taarifa ya habari jana na kugundua hawa wazazi wamefungwa kwa uzembe wao, coz et mahakama iliwataka wakubali shitaka la kuua bila kukusudia baada ya kubalishwa kwa shitaka lao la mwazo la ukiukaji wa haki ya binaadamu kwa kusababisha mateso ya mtoto wao huyo wa box

na wao wakakubali kukubali
 
So yule mtoto angeendelea kukaa kwenye boksi?

Ktk kumwokoa ilitakiwa kitu cha kwanza baada ya kimgundua mtoto huyo ni kuchunguza maisha anyoishi. mf. kula, yaani aina ya vyakula na kiasi cha mwanga aliouzoea. Ndipo pole pole wangeanza kumnyang'anya mazingira yake aliyoyazoea. kitendo hicho kingecjukua hata mwezi mzima. Lakini naamini hao waokozi hawakufanya hivyo na ndo sababu ya kufa kwake.
 
Kwa taratibu za JMT yeyote anayeshitakiwa kwa makosa ya mauaji ni lazima awe na wakili wake wa kumtetea mahakamani(mara nyingi huwekwa na Jamhuri lakini pia huzuiwi kuwa na wako binafsi) hivyo kwa yaliyotokea sidhani kama hao washtakiwa walikuwa katika hali ya sintofahamu na kukosa mtetezi wa kisheria.

Cha msingi kama hawajaridhika na hukumu ni kufuata utaratibu tu wa kukata rufaa mahakama ya juu zaidi i.e Court of Appeal
 
Back
Top Bottom