Nani atavaa viatu vya maximo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani atavaa viatu vya maximo?

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Mar 24, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  HABARI iliyotolewa siku si nyingi zilizopita kwamba zoezi la kupokea maombi ya wanaoomba kumrithi kocha Marcio Maximo kufundisha timu yetu ya taifa limefikia tamati.

  Kwamba zoezi hilo sasa limefungwa ni kiashiria cha kumalizika kwa hatua moja kubwa kuelekea kumpata mrithi huyo wa kocha Maximo.

  Tunasikia makocha wengi wa nje na wa ndani wachache wameomba kuajiriwa kwenye nafasi hiyo nzito kuliko zote za ufundishaji soka nchini mwetu.

  Wakati zoezi hilo likiendelea, naomba nitoe rai kwa wahusika kufanya kila linalowezekana tumpate kocha bora kuliko Maximo.

  Nitashangaa jamaa zangu walioapa kuwa na Maximo kwa hali zote, wakishtushwa na kauli yangu hiyo na kuitafsiri kuwa namchukia kocha huyo kutoka Brazil.

  Lazima wote tukubaliane na ukweli kwamba binadamu anapotafuta maendeleo, siku zote huhitaji kupiga hatua kutoka pale alipofikia kwenda mbele au juu.

  Maximo amefanya mengi makubwa na mazuri kwa soka yetu, 0basi anayekuja awe na ujuzi na uwezo mkubwa zaidi wa kututoa hapo kutupeleka mbele au juu zaidi, kutegemea uelekeo wetu kama ni juu au mbele.

  Mshtuko hapo unatoka wapi? Je tunataka kocha ajaye aturudishe nyuma kutoka alipotuacha Maximo? Hapana, hata kama baadhi yetu wanampenda Maximo kwa kiasi gani, taifa lao ni bora zaidi kuliko Mbrazil huyo ambaye ni mwajiriwa wetu.

  Nitafurahi sana kama kocha ajaye kwa ajili ya timu yetu ya taifa atatengeneza hali kama ambayo kocha Kostadin Papic wa Yanga ameitengeneza kwenye klabu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani.

  Naomba isitafsiriwe kwamba nampigia debe kocha huyo kukabidhiwa mikoba ya Maximo maana nasikia naye amejitosa kuiomba. La hasha, nitakachokizungumza ni kitu tofauti kabisa.

  Hata hivyo, kama ataonekana bora kuliko waombaji wengine, kwa nini asipewe kazi hiyo?

  Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, ni jambo lililo wazi kabisa kwamba Watanzania wengi tumejigawa makundi mawili, la kumpenda, kumfurahia, kumsifia na kumtetea Maximo wakati wote na lile la kumchukia, kumkejeli na kumlaumu kocha huyo wakati wote!

  Sitazungumzia sana makundi hayo hasimu yaliyo na sura za ushabiki wa Yanga na Simba kwani nilishayaongelea vya kutosha kwenye safu hii katika makala iliyokuwa na kichwa cha habari "Kwa nini Marcio Maximo atenganishe Watanzania?" (Raia Mwema, esemba 16-22, 2009).

  Kitu kibaya ni kwamba upande unaomshabikia kocha huyo hauoni hata kosa lake moja siku zote wakati ukweli ni kwamba, kama ilivyo kwa kocha yeyote duniani, Maximo naye anakosea kosea kibinadamu.

  Upande usiomshabikia hauoni hata zuri au jema moja alilofanya kocha huyo wakati ukweli ni kwamba amefanya mazuri mengi mno ya kustahili sifa.Hapo ndipo ninapoyaona makundi hayo kuwa na tabia za ushabiki wa Yanga na Simba.

  Kwanza, mashabiki wake 'hawabadili dini' tangu utotoni na pili, husifu sana upande wao tu na kubeza sana upande mwingine wakati wote hata kwa kupotosha ukweli!

  Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo, kinachonijia akilini mwangu, baadhi ya wale walio upande wa Maximo kwa sasa watabadili upande na kuwa upande wa kumbeza kocha atakayemrithi ambapo baadhi ya wale wanaombeza Maximo kwa sasa watakuwa washirika wa kocha atakayemrithi!

  Hii ni kwa sababu ushabiki wa kumuunga mkono na kumbeza Maximo, umejijenga katika hali ya kumhusisha Maximo kama mtu binafsi au mtu asilia (natural person).

  Upinzani huo wa Watanzania hao unamhusu Maximo kama Maximo kiasi cha watu kuliweka taifa lao nyuma ya kocha huyo, kama mtu asilia, yaani Marcio Maximo na si kama taasisi, yaani kocha wa timu ya taifa!

  Aidha, wanaombeza kocha huyo kwa kila kitu kwa sasa, walikuwa wanasisitiza kwa muda mrefu kwamba kocha huyo aondoke, aje mwingine wa kutupa mafanikio. Kwa hiyo sasa akija huyo mwingine watakuwa naye pamoja kwani kuja kwake badala ya Maximo ndiko walikokuwa wanakuhitaji.

  Kwa upande mwingine, waliokuwa wanamshabikia Maximo walikuwa wanapinga kocha huyo kuondoka kwa hoja kuwa alishaiweka soka yetu kwenye njia sahihi, hivyo alistahili kuendelea nayo kwa hatua inayofuata.

  Kwa msingi huo, kukwama katika kutuletea mafanikio kwa kocha atakayemrithi Maximo litakuwa jambo la faraja kwao la kuthibitisha kuwa walikuwa sahihi kuwa na msimamo kwamba Maximo angeendelea kuwa nasi.

  Kwa hiyo ushabiki wa Maximo utaendelea kutawala vichwa vyetu hata baada ya kocha huyo kuondoka ambapo wanaomuunga mkono sasa, huko mbele watasikika wakisema "ona sasa, mlimbeza sana Maximo, kiko wapi na kocha wenu wa sasa. Maximo alikuwa bonge la kocha,si kama huyu mbabaishaji wenu."

  Na wale wanaompinga Maximo sasa watajibu "huyu ndiyo kocha bwana, hamuoni vitu anavyovifanya, Maximo aliviweza hivi?" Hapo sasa tutakuwa hatujadili mikakati ya kuendelea kisoka bali tutakuwa tunawajadili watu kwa kuwalinganisha.

  Hali itakuwa mbaya zaidi kwa kocha huyo mpya, kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa sasa wa Maximo, akishindwa kuleta mafanikio licha ya kuwa na kina Juma Kaseja, Amir Maftah, Athumani Idd "Chuji" na Haruna Moshi "Boban" ambao kwa viwango vyao vya soka si wa kuachwa nje ya timu ya taifa na kocha yeyote mwenye uelewa hata mdogo wa uongozi (sizungumzii utaalam wa kufundisha soka).

  Hali ikiwa hivyo, atabezwa kocha huyo na watabezwa wachezaji hao na mashabiki, wa kiapo wa kocha Maximo.

  Kiashiria cha kwanza cha kuendelea kwa malumbano ya kumhusu Maximo ni kauli zilizowalazimisha baadhi ya makocha wazawa kujitokeza kuomba nafasi hii.

  Kauli nyingi zilizosomeka magazetini za kuwaomba Watanzania hao wachangamkie ajira hii zilielekezwa kwenye kuwasuta kama:

  "Haya, ombeni kazi hii tuone kama mtafanya vizuri zaidi ya Maximo, maana mlikuwa mnachonga sana kuhusu uwezo wa kocha huyo".

  Kama shinikizo la kuomba kazi hiyo ni hilo, hata mimi nawaunga mkono makocha wazawa walioacha kuomba kazi hii. Itakuwaje uombe kazi ambayo baadhi ya watu hawatasubiri kuona mafanikio yako bali watasubiri kwa hamu kuona unakwama, ili wakuzomee?

  Je miongoni mwa mahasimu wako hao wakiwa katika nafasi ya kufanikisha kukwama kwako wakikukwamisha kwa makusudi ili wakusute itakuwaje? Hao watakwambia; "wewe ulitusemea mbovu sana wakati wa Maximo, mbona sasa unachemka?"

  Makocha wazawa wana haki ya kikatiba kumkosoa kocha kutoka nje na wanapotumia haki hiyo hawalazimishwi kuomba kazi ya kocha huyo baadaye kwani pia wana haki ya kikatiba ya kutoomba kazi hiyo.

  Baadhi yetu tulikosea kuwashinikiza kuiomba na wala tusishangae kwa nini hawakuiomba licha ya kumkosoa kocha kutoka nje. Kukosoa na kuomba kazi ni vitu viwili tofauti.

  Nilitangulia kusema kuwa napenda sana kocha ajaye wa timu yetu ya taifa atengeneze, kwa taifa, hali aliyoitengeneza kocha Papic wa Yanga kwa klabu hiyo.

  Maana yangu hapa ni kwamba wakati Dusan Kondic akiwa na Yanga, soka ya timu hiyo ilikuwa ya kutanguliza mpira mbele na kufukuza sana. Haikupendeza kabisa. Baadhi yetu, nikiwa mmoja wao, tulichoshwa kuona soka bovu la ushindi wa kulazimisha la mabingwa wetu hao wa soka wa msimu unaomalizika.

  Mimi nilishauri kupitia safu hii kuwa Yanga wangetafuta kocha mzuri baada ya Kondic kumaliza mkataba wake ili icheze soka ya kuvutia na ya ushindi. Nilishambuliwa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kwa kigezo cha kocha huyo kuiwezesha Yanga kubeba ubingwa.

  Kuna baadhi ya wenzetu walitupiana maneno makali gazetini kwa sababu mmoja alitoa maoni kuwa Kondic hakuwa kocha mzuri huku mwingine akisema kuwa Mserbia huyo alikuwa kocha mzuri mno.

  Kama Yanga wangefanya kosa la kumwajiri kocha mwenye ujuzi mdogo kuliko Kondic, leo hii kelele za mashabiki wake kadhaa zingehusu kumlilia Kondic na kuwavuruga wachezaji.

  Kwa bahati nzuri Papic amejidhihirisha kuwa kocha mzuri sana, aliyeibadili Yanga kwa muda mfupi sana na kuwafanya mashabiki wake waimarishe umoja wao katika eneo hilo la kutathmini kazi ya kocha wao.

  Hakuna malumbano kabisa ya nani zaidi kati ya Waserbia hao wawili, Kondic na Papic, kwa sababu wana Yanga wote sasa wanashukuru kwa makubwa aliyowafanyia Kondic na kuukubali uwezo mkubwa alionao Papic.

  Ni katika muktadha huo, naomba sana kocha wa kupewa timu ya taifa awe mwenye uwezo mkubwa zaidi ya Maximo ili atusogeze kutoka pale atakapotuacha Maximo huku Watanzania wote tukiungana katika kumkubali badala ya kuanzisha ligi mpya ya "afadhali ya Maximo" na "tokeni hapa na Maximo wenu!"

  Wote kumshukuru sana Maximo kwa kazi yake nzuri tunayoiona iliyotuinua kutoka mahali fulani chini na kutufikisha mahali fulani juu na wote kufurahia vitu vya hali ya juu vya kocha mpya pamoja na kujadili vitu vya maendeleo ya soka yetu.

  Itapendeza kama muda ukiwadia tukiwa wamoja pamoja na kocha wetu mpya kama Yanga walivyo wamoja pamoja na Papic wao.
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu ratiba ya michuano ya wawali kombe la mataifa ya Afrika imeshatoka. Mpaka sasa naona kama tayari Tanzania imetolewa kabla hata ya kucheza mechi moja, tayari zengwe limeanza kwa kocha mgeni kabla hata hajaja, watu wanataka turudi kule kule kwa makocha wanaoleta uswahili,ni fact kuwa tuko hatua nyingine, yaani tumepiga hatua tatu mbele, japo lengo letu ni kupiga hatua 10 mbele. Maximo ametusaidia. Hata kocha wa Yanga mwenyewe akiwa na credentials achukuliwe tu kama kazi yake inaonekana.
   
 3. G

  Gokona Member

  #3
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau najua wengi wetu ni wapenda soka na hasa ni washabiki wa ligi ya ukerewe,binafsi mimi ni mdau mkubwa wa Man u na hapa nyumbani kama kawaida mimi ni mtoto wa wekundu wa msimbazi wale wanaoshinda ligi za ndani bila kufungwa na ligi za nje vilevile.sasa hapa nyumbani mkataba wa maximo ndio huo unaondoka je nani mnaona anafaa kubeba jahazi hilo kwa hapa nyumbani? au inabidi tutafute kina shehata?
   
 4. senator

  senator JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  ...Naona ushabiki damu wako tunafanana..Kwa ss maximo amkabidhi mikoba TWALIB HILLAL...kucha wa timu ya taifa ya Oman.
   
 5. bona

  bona JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  tunataka kocha aliyeiongoza timu qualification za world cup na wakafanikiwa ku qualify, kocha aliyewai fundisha timu uk premier league, french ligue 1, italia seria a, ujeruman bundesliga, hispania laliga au ligi za brazil au argentina tena kwa mafanikio yanayoonekana kutoka alipoichukua timu hadi alipoiacha! nje ya hapo hatufai!
   
 6. h

  housta Senior Member

  #6
  Mar 29, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna pesa za kuwalipa hao unaowataka?Investment zenyewe kwenye michezo zipo?Au unadhani udhamini ndio unainua kiwango cha soka?Mikakati na utekelezaji wa TFF upo vipi?Kuna mengi behind everything.Kujenga timu nzuri ya taifa NI LAZIMA mikakati iwepo ya kuondoa USimba na UYanga.Invest heavily kwenye Soccer Academies za vijana.After 10yrs matunda yataonekana.Kwa sasa bado sana!Nakupa mfano tu:Capello anayeifundisha England anapokea mshahara way above 4mln pounds.Na huyo ndio hao makocha unaosema wamefundisha top leagues duniani.Am sure hatuna pesa za kuweza kumlipa mtu mmoja japo close to 1bn TSH.Sasa niambie hapo unaweza kupata kocha wa hizo top leagues?
   
 7. G

  Gokona Member

  #7
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi najua makocha wazuri ulaya wapo tatizo gharama zao kubwa,sasatutumie kitu kinaitwa KAZEN theory ili tujaribu kuona tatizo lipo wapi ili tutatue kwa makocha wetu ambao tunaweza kuwamudu badala ya kulaumu au kuangalia symtoms za tatizo,mimi nafikiri kuna jamaa kasema Twalib Hilal ni mfano tu maana makocha hao tunaowataka htuwawezi na si kila kocha anaetoka nje anafaa nyinyi mashahidi MO alileta kocha wa African Lyon ameshindwa ku deliver results.Tatizo langu ni kuwa kocha mzawa atapata ushirikiano na sponsors? na je TFF wakiwa wanamlipa hawatamsumbua? hapo nina kigugumizi wadau nitoeni shaka
   
 8. Mujuni2

  Mujuni2 Senior Member

  #8
  Mar 29, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumpeni Phiri, ni mgeni lakini sio expensive kivile, na ana CV ya kutosha, mfano mdogo tuu kaifanyia makubwa Zambia alipokuwa head coach.
   
Loading...