mtanzania anayefaa ni bwana william erio wa ppf.
Huyu anauchungu sana na wanachama wa ppf hivyo atakuwa na uchungu pia na watanganyika pindi tukimpa nchi aiongoze.
Huyu hulipwa kamshahara kadogo tu kama milioni 12 kwa mwezi, landcruiser vx v8 na dereva, housing allowance ya shs milioni 4 kwa mwezi. Fuel allowance ya shs. 1.2 milion japo ana fully fueled vx, kila baada ya miaka mitatu hulipwa vijisenti vichache kama group endowment shs 540 milioni, gratuity shs 108million na samani za nyumbani tshs 60milion.
Huyu anajitahidi sana kutosafiri sana nje ya nchi, anamzidi kidogo sana rais wa sasa, 50% ya muda wake wa ajira yuko nje ya nchi na perdiem yake sio kubwa kihivyo, ni analipwa tshs 1,820,000 (usd 810x1.25x1800) kwa siku kuanzia siku ya kuondoka hadi ya kurudi.
Safari za ndani ya nch analipwa tshs 500,000 kwa siku hata kama ni bagamoyo. Ni kiongozi mzuri atakaye tufaa watanganyika.
Uzuri mwingine ni ana gene ya uongozi maana ni mjomba wa rais mstaafu, bw. Benjemini william mkapa, kwa hiyo atatufaa wadanyika
nawasilisha pendekezo langu.