Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,730
- 7,979
Uogozi wa kisiasa unahitaji mambo mawili: Ushawishi na uwezo wa kujenga matumaini kwa watu. Ushawishi unategemea makundi ya watu walio katika uongozi kwa kipindi husika na matumaini hujengwa na namna Serikali inavyokidhi matakwa ya wananchi na matarajio waliyo nayo kwa siku za usoni.
Ni kwa misingi hii, muundo wa kioungozi na kiutendaji wa CCM na Serikali yake tangu Uhuru au tuseme tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, umekuwa ukiibua watu walio na ushawishi kutoka kila kona au makundi tofauti ya kijamii kwa lengo la kupata ushawishi.
Ni kupitia ushawishi ndipo wakaibuliwa vijana kama akina Nape, Mwigulu, Makamba, pia akina Nchimbi, Kamala na wengine wengi tu. Ushawishi pia ulionekana katika balance za uteuzi ili kupata uwakilishi wa kimaeneo.
Kunahitaji hesabu kali sana katika hili, si suala la kumteua yeyote tu unayempenda. Sote tunajua kazi kubwa iliyofanywa na hao vijana watatu wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita.
Aidha, kwenye suala la matumaini, juhudi zilikuwa kubwa za angalau kuonyesha kujali matatizo na mazingira ya nchi ili kujenga matuamaini kwa wananchi. Rais Mstaafu Kikwete na Waziri Mkuu wake wa kwanza walipoingia madarakani, walipambana na ukame na njaa.
Hata hivyo, viongozi hawa waliwajaza matuamaini wananchi kuwa hakuna mtu ambaye angelikufa kwa njaa. Wakawajaza matuamaini kuwa wataleta mvua ya kutenengeneza kutoka Thailand. Ushawishi na Matuamaini ni msingi mkubwa katika siasa. Ukikosa mambo haya jiandae kushindwa vibaya kwenye chaguzi zozote zile.
Nikirejea kwenye swali la msingi. Nikiiangalia timu ya CCM iliyopo sasa hivi, huku nikiamini Kinana ambaye ndiye Kampeni Meneja wa Mkapa na Kikwete, huku akifanya miujiza ya kuirudisha CCM iliyokuwa imepotea kwa dhana ya "Mawaziri Mizigo" hata Rais wa sasa akaingia magogoni hatakuwapo (Huenda akaendelea kuwa Katibu Mkuu hadi wakati huo lakini sidhani).
Timu ya CCM leo ina akina Paul Makonda, Polepole. Kwa mtizamo wangu, sijamuona kati ya hao ambaye anaweza kusimama peke yake jukwaani akaongea akaeleweka, akaaminika na wananchi wakatoa kura. Wanachama wenzangu wa CCM, tunaamini katika kura au kuna mbinu nyingine tunaitarajia kuitumia 2020.
Nikija kwenye swali la Pili. Hili ndilo kizungmkuti. Bajeti ya 2016/2017 ndio inaishia na haijatoa dalili nzuri za utekelezaji wa "kero ndogo ndogo" za wananchi, si vijijini wala mjini. Dar es Salaam tumejenga kilomita NNE za Moroco-Mwenge (mtanikumbusha barabara nyingine iliyojengwa Dar).
Huko mikoani ndio hata usiseme. Hali sio vile kama ilivyokuwa enzi ya JK ambapo mabuldoza yalikuwa kila pembe ya nchi yetu. Ni mabuldoza haya ndiyo yaliyomjenga Raia wetu. Ila leo kiukweli yamepungua sana. Scheme za umwagiliaji zilikuwa kila kona biala kusahau vocha za pembejeo. Wananchi wameshaambiwa LIVE mazao yao yakiliwa na maji au jua, wajiandae kufa sio vinginevyo.
Tukija kwenye mzunguko wa Fedha, huku ndiko hatari. Tunajua siku fedha haipatikani kiurahisi lakini wapo wanaodiriki kusema hawajawahi kuona mzunguko wa pesa mgumu zaidi ya huu. Mbaya kuliko yote, spidi ya siku namna zinavyoondoka.
Hata kama tungelikuwa na akiba ya fedha inayoendana na maji ya Bahari, bado hatutaweza kutimiza hata robo ya tulichowaahidi wananchi. Hakuna Ilani ya miaka 10. Ilani ni miaka mitano kwa hivyo vyote tulivyoahidi tumebakiwa na siku 1306 tu ili kufika Jumapili ya tarehe 25 Oktoba 2020. Kwa wanaokumbuka mfumo wa "deadline" ulivyo, kila ukiwa unakaribia ndipo hakuna unalolifanya.
Hakuna ubishi matumaini ya watu yamepotea sana katika awamu hii kuliko awamu zozote. Hakuna kundi ambalo halijaisoma namba hadi sasa. Suala la Bashite limeshusha sana umaarufu wa Rais wetu, nje na ndani. Tulizoea habari za nchi jirani kututania tuwaazime buldoza wetu. Lakini hali haipo kwa sasa. Upepo umebadilika. Kwa hakika Bashite, hatasahaulika na CCM 2020.
Na huku tumebadili mfumo wetu uliokuwa unatoa fursa ya kuchapisha na kugawa kanga na Tisheti kwa wingi. Nawauliza CCM, 2020 Ni nani atakayekuwa kinara wa kuinadi CCM kwa wananchi na atawaambia kitu gani? Binafsi naona naona CCM imeshakufa rasmi, kwani kuna watu hata ndani ya CCM hawataipigia kura.