Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,042
- 1,305
Nani angemsikia ?
Tulikuwa kijiweni, akafika kaka Uledii
Asema changamkeni, akatupa mredii
Ana kitu mkononi, twendeni kwa zawadii
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Akaagiza mabapa, vijana tufurahini
Mtu asitoke kapa, kinywaji hiki kunyweni
Akayavaa malapa, akenda zake chooni
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Alipofika chooni, bila ya kujiuliza
Akanywa cha mkononi, sumu ya kujimaliza
Kinachoua majani, naye kikamchakaza
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Akaongeza na nyagi, huku akituambia
Punguzeni hili vagi, mimi ndio najifia
Punde akawa ja chigi, huku akigugumia
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Akimlaumu Dani, kwanini kamsaliti
Rafiki wa ubavuni, aliyemwibia binti
Anaenda kaburini, kamuachia banati
Ndoa ni ya kanisani, yeye kaingia kati
Tumemfukia jana, kaenda tusipojua
Moyo wake ni mpana, ila amejiiua
Ilimpata sonana, pombe hakumuagua
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Abuuabdillah ✍️
Tulikuwa kijiweni, akafika kaka Uledii
Asema changamkeni, akatupa mredii
Ana kitu mkononi, twendeni kwa zawadii
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Akaagiza mabapa, vijana tufurahini
Mtu asitoke kapa, kinywaji hiki kunyweni
Akayavaa malapa, akenda zake chooni
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Alipofika chooni, bila ya kujiuliza
Akanywa cha mkononi, sumu ya kujimaliza
Kinachoua majani, naye kikamchakaza
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Akaongeza na nyagi, huku akituambia
Punguzeni hili vagi, mimi ndio najifia
Punde akawa ja chigi, huku akigugumia
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Akimlaumu Dani, kwanini kamsaliti
Rafiki wa ubavuni, aliyemwibia binti
Anaenda kaburini, kamuachia banati
Ndoa ni ya kanisani, yeye kaingia kati
Tumemfukia jana, kaenda tusipojua
Moyo wake ni mpana, ila amejiiua
Ilimpata sonana, pombe hakumuagua
Nani angemsikia, mapenzi yamemuua
Abuuabdillah ✍️