Nani anamiliki mali za wakimbizi wanaoingia nchini?

Wisest man

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
993
332
Mkoa wa kigoma ni moja ya eneo linalotumika kuwapa hifadhi wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini mwao. Warundi, wakongo na wanyarwanda ni miongoni mwa watu wanaohifadhiwa kwenye makambi yaliko mkoani kigoma.

Bila shaka kabla ya wakimbizi hao kupatiwa hifadhi ya muda nchini walikuwa wakimiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika kama mifugo, nyumba, mashamba/ardhi na hata biashara. Je! Wanapokimbilia Tanzania kupata hifadhi tena wengine wakikaa miaka mingi kwenye makambi ya wakimbizi nani anachukua ardhi yao kipindi chote wanapokuwa nchini? Je! Serikali ya Tanzania na nchi wanakotoka wakimbizi hao hufanya wanahakikisha wakimbizi hao pindi wanaporudi makwao wanakuta haki zao hazijapotea?
 
Mambo ya wakimbizi ni biashara ile kama ulikua haujui...na wakimbizi hua wana ndugu zao wanabaki huko wanapotokea na pia jamaa hua wanaenda kwao kutembea..na pia wanasikilizia resettlement.....
 
Una maanisha wanatafuta makazi mapya nchini huku kule kwao wakiwaachia ndugu zao?
 
Hoja ya msingi ni resettlement...kupelekwa kwenye makazi ya kudumu either ulaya au marekani halafu pia wanapoondoka ndugu zao hua wanabaki maana haiwezekani wakaondoka ukoo mzima hivyo vitu vinatumiwa na wwngine na wengine hufikia hatua ya kuviuza...
 
Mkoa wa kigoma ni moja ya eneo linalotumika kuwapa hifadhi wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini mwao. Warundi, wakongo na wanyarwanda ni miongoni mwa watu wanaohifadhiwa kwenye makambi yaliko mkoani kigoma.

Bila shaka kabla ya wakimbizi hao kupatiwa hifadhi ya muda nchini walikuwa wakimiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika kama mifugo, nyumba, mashamba/ardhi na hata biashara. Je! Wanapokimbilia Tanzania kupata hifadhi tena wengine wakikaa miaka mingi kwenye makambi ya wakimbizi nani anachukua ardhi yao kipindi chote wanapokuwa nchini? Je! Serikali ya Tanzania na nchi wanakotoka wakimbizi hao hufanya wanahakikisha wakimbizi hao pindi wanaporudi makwao wanakuta haki zao hazijapotea?
una umri gani mkuu kabla sijakupa tusi binafsi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom