Nani anamiliki magari ya UDA?

Nani anamiliki magari ya UDA?

wa habari juu ya umiliki wa shirika la Uda ambalo kampuni yake ndiye mmiliki wake kwa sasa.Kisena alikuwa akijibu tuhuma zilizotolewa bungeni na baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa kampuni hiyo, Patrick Mtani.PICHA: SELEMANI MPOCHIKampuni ya Simon Group imesema kwamba ni mmiliki wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) kwa asilimia 76 huku serikali ikimiliki hisa asilimia 23.Kampuni hiyo imesema ilinunua hisa za UDA kutokakwa waliokuwa wamiliki ambao ni Jiji la Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena, alizungumza na waandishi wa habari jana kufafanuakuhusu kauli ya Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, aliyoitoa bungeni Alhamisi iliyopita kuwa UDA ni mali ya serikali kupitia Msajili wa Hazina na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.Kisema alisema serikali inamiliki hisa zenye thamani ya Sh. 3,488,651 huku Simon Group ikimilikihisa zenye thamani ya Sh. 7,880,303.Nyingine ni hisa zenye thamani ya Sh. 3,631,046 kutoka Jiji la Dar es Salaam na kuwa thamani yan hisa zote ni Sh. 15,000,000.Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alihoji utaratibu uliotumika wakati wa uuzaji wa hisa zilizokuwa za UDA.Kisena alitoa uthibitisho huo kwa kutoa mikataba mbalimbali waliyo kubaliana kuanzia Kamati ya Kudumu ya Bunge ilipotembelea kampuni hiyo mwaka 2011 na kukubaliana pande zote mbili zichukue hatua kuhakikisha uwekezaji unawanufaisha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kupata usafiri wa uhakika.Kisena alieleza kuwa inawezekana wabunge wanaohoji suala la UDA ni kukosa taarifa za uhakika kuhusiana na umiliki wa UDA.Aidha alisema Novemba15, 2011 walikaa na Msajili wa Hazina, Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mwanasheria wa Jiji kuzungumzia malalamiko yanayotolewa juu ya uwekezaji katika UDA na kubaini malalamiko yalikuwa ni Shirika kuuzwa kwa bei ndogo.¡°Tulikutana wote tukakubaliana kuunda bodi nami nikasema waseme bei yao nitalipa, mwisho tukakubaliana kwa pamoja tulipe kiasi cha Shilingi bilioni tano, ukiangalia hizi nyalaka utaona saini ya Meya Dk. Didas Masaburi, Robert Kisena na John Msella mwakilishi wa hazina,¡± alisema Kisena.Alisema baada ya makubaliano walikutana na kamati ya bunge na kila mwana hisa alipeleka taarifa yake kamati ikaagiza wakae pamoja wakubaliane kwa pamoja Agosti 16, 2013.Alisema walikutana tena wakiwamo wabunge wa Jiji la Dar es Salaam Agosti 22, 2013 wanahisa wakakubaliana kuuza hisa zao ili wakawekeze kwenye Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (DART) na kuwa Agosti 28, 2013 wanahisa pamoja na kamati ya jiji ikiongozwa na Mkuu wa mkoa walikubaliana kupeleka suala hili kwenye kamati ya bunge.¡°Tulipokubaliana tulikwenda Dodoma kukutana na kamati ya bunge tukiongozana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadiki meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi wajumbe kutoka TRA, mimi mwenyewe pamoja na Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe, na wabunge wote wa Dar es Salaam,¡± alisema.Alisema katika kikao cha mwisho walichokaa Dodoma kamati ilikubaliana na maamuzi yaliofikiwa na wanahisa kuachia kampuni ya Simon Group kuendesha shirika hilo.Alisema makubaliano hayo yalisainiwa na Dk. Masaburi; Msajili wa Wizara ya Fedha, Mwakibinga Mhelela na Robert Kisena, Mkurugenzi wa Simon Group.SOURCE: NIPASHE
 
Huu utawala dhalimu hautabaki madarakani milele. Hivyo mara tu watakapotolewa madarakani watakaoingia madarakani watakuwa na haki na kila sababu ya kuwakamata wote waliokwapua mali ya umma, kuwafungulia mashtaka na kuwapandisha kizimbani na hata kuwafilisi mali zao zote walizozipata kwa njia ya haramu. Na ushahidi dhidi ya hawa wadhulumu utakuwepo wa kumwaga.

Ndo maana nikasema hata tukijua tutachukua hatua?
 
Huu utawala dhalimu hautabaki madarakani milele. Hivyo mara tu watakapotolewa madarakani watakaoingia madarakani watakuwa na haki na kila sababu ya kuwakamata wote waliokwapua mali ya umma, kuwafungulia mashtaka na kuwapandisha kizimbani na hata kuwafilisi mali zao zote walizozipata kwa njia ya haramu. Na ushahidi dhidi ya hawa wadhulumu utakuwepo wa kumwaga.

Hapo umenena lakini kwa jinsi tulivyo sasa hata useme bado haisadii we check suala la ESCROW lilivyopigwa danadana. Watu tumetulia tulii.
 
UTAWala wa awamu ya 4 watawALA WAMEPIGA PESA SANA NA KUTUACHA Wnanchi masikini hizi UDA ni za vigogo
 
Hivi mali zote zile za UDA thamani yake ni kama shilingi ngapi za kitanzania?

Maana hapo kwenye maelezo ya Mr Kusena kuna figure tofauti .Ukijumlisha hizo hisa za serikali na Simon Group unapata tshs.11,368,954.Halafu akasema jumla ya hisa zote ni 15,000,000.Halafu walitaka kununua jumla kwa shilingi bilioni tano. Hapa ni mkanganyiko tupu yaani ni magumashi mwanzomwisho.
 
Wala sio povu mi mtu mdogo sana ispokuwa sisi wa bongo hata tukijua hamna hatua yoyote tukayochukua zaidi kusema humu tuu na baada ya hapo sled itafungwa kwa kifupi ni kujifurahisha tu

Kwa hiyo kama huwezi kuchukua hatua inayopaswa hutakiwi kuhoji?
 
Hayo ma uda yasiwatie shida. Mabasi mengi yameanza kufa na yaliyopo yamechoka mbaya. Hayawezi kudumu muda mrefu.
kwa kukopesha mabasi ya ovyo kwa dhamana ya viwanja vyenye thamani kubwa kabisa kama depot ya uda kurasini na stand ya station wajanja watapata wanachokitaka. wajuzi wa usafiri wanasema uda haitaweza kulipa mkopo hivyo mali zake za msingi kutwaliwa na kampuni kubaki garasha.
 
Mmiliki ni Simon Group ambayo inamilikiwa na Robert Kisena
 
Tukijua ni vizuri zaidi ktk kumbukumbu zetu na hata vizazi vijavyo siku zote naamini kuna siku mageuzi yatatokea hapa chini ya utawala tafauti na huu wahusika wote walohusika ktk kashfa hizi itabidi warudishe/wafilisiwe/wafikishwe mbele ya Law.hata kama ni warithi wao/watoto wao watakuja wajibishwa kwa hili sote tuungane na tulitie akilini we acha waibe tu zotawatokea puani
 
Kuna mambo makubwa yapo chini ya kapeti na wakubwa wanajua na wapo kimya
 
Back
Top Bottom