Nani anahusika na usajili wa TP Mazembe

Nani anahusika na usajili wa TP Mazembe

Kwani Aliyemuita Singano ,Mess ninani? Simba hao hao. Leo hawezi tena?acha aende pesa Za TP zinakuuma nini Mkuu.
Akifanikiwa huko watataka kumsajili ili kumuharibia tu,juzi kati walikua busy kutaka kumsajili hassan kessy dogo machale yakamcheza,yan mikia wana roho mbaya sana,roho zimewauma sana singano kwenda tp
 
Wabongo! Wabongo! There back at your keyboard buttons criticizing the big power Sport club of Tp Mazembe?

Unadhani una upeo mkubwa Sana kuliko jopo la wataalam wa usajili TP Mazembe? Wanajua wanachokifanya kuliko wewe mtanganyika wa dumila,

Samatta was never such a deal, but Mazembe made him to be who he is now! Football is a game of chance and have turned into business and investment.

Nyamaza usiyoyajua! Waachie wenyewe! Khaaaaa!
Sawa mwalimu kashasha nazan mambulula wamekuelewa wanadhan Tp mazembe ni simba au yanga
 
Nimeshangaa timu bora ya Africa inamsajili singano
Alafu wanawauza wachezaji wao tegemezi wawili kwenda ubeligiji ambao ni meshak Elia na zola

Singano anamiaka 27 ataipa nini tp mazembe angekuwa na miaka 22 tungesema angeweza kudevelop kisoka ila huyu jua limeshazama

Ninavyoona Tp mazembe wanawakala mtanzania anayewaingiza chaka na anapiga ten percent

Wameshindwa kumuona hata rashid juma ndio wakachukue ile mashoto inakimbia bila plan uwanjani

Ila boss wa Tp mazembe atakua ameyumba sana kiuchumi

Mazembe inaanza kupotea taaratibu baada ya miaka kumi na tano kwenye pik ya juu
Roho mbaya, Wivu, Chuki, Fitina, Husda vimewajaa.

Mnatamani kuona wenzenu wakiwa chini siku zote roho ya hivi kiongozi wenu ni yule msemaji wenu poyoyo.
 
Singano bado yupo vizuri tu lakini hakuendana na mfumo wa Azam. Kinachohitajika kwake ni kumuongezea utimamu wa mwili na saikolojia kidogo. Nadhani Mazembe wameliona hilo na wanauwezo wa kulirekebisha.

Kuna mdau kalimnganisha Singano Na Rashid Juma na kushangaa kwa nini Mazembe wasimchukue Rashid Juma badala yake wakamchukua Singano. Ukimlinganisha Rashid Juma na Singano kidogo wanalingana ila Rashid Juma bado anamapungufu kwenye umaliziaji na hasa anapokuwa ndani ya boksi la adui bado hajaweza kutulia. Na hili tatizo ni la muda mrefu kiasi sasa sijui benchi la ufundi kla Simba limeshindwa kumrekebisha. Ndio maana msimu mzima sijui hata kama ana goli lolote kwenye ligi japokuwa anafika mara nyingi sana golini. Ila kwa kasi Rashid Juma ana kasi sana kumzidi Singano. Singano naye anamzidi Rashid Juma kwenye maamuzi pale anapofika golini lakini hata ufundi Singano ni fundi zaidi.

Kadri muda unavyoenda naamini Rashid Juma atakuwa vizuri ukizingatia kazuungukwa na mafundi watupu na umri bado unamruhusu kujifunza tumpe muda tu. Ila benchi la ufundi la Simba nalo lina kazi ya ziada kumjengea utulivu anapokuwa ndani ya boksi la adui kwani mbio zote na kukokota mpira kutoka mbali vinakuwa havina faida kama ataendelea kuwa anakosa magoli ya wazi.
 
Hahahahahahahahah mchezaji wa miaka 27 sio mchezaji wa majaaribio sio mchezaji wa kumuweka sawa kisaikolojia wala utimamu wa mwili ,27 years old ni mchezaji wa kwenda kuisaidia timu sio mchezaji wa majaribio wala Development.
 
Tp mazembe inasajili wachezaji wengi wa type hiyo na inawapeleka katika development squad kuwaimarisha sasa nashangaa mnavoponda na siku zote uelewe kua usajili ni gambling waweza sajili mchezaji mzuri sana na akaja akachemka.
Kikubwa wanachoangalia ni kipaji cha mchezaji.
Tutajie hao wachezaj walio wa Development wakiwa na miaka 27 kama ya Singano tuwajue.
 
Wabongo kinacho tuuma ni kuna Ajib amechezea nafasi baada ya kugoma kwenda Mazembe. Mtashangaa maajab atacheza vizuri tu.
 
Umri kwenye mpira ni kila kitu
Huyo singano hadi aje afiti kwenye mfumo itakua umri umeenda sana

Mpira ni kitu kinachoonekana mkuu hata club kubwa huwa zinapuyanga kusajili
Sielewi kwanini unatwseka, mazembe wameona singano anawafaa wewe unaathirika nini? Hivi huoni mazembe mbovu ni manufaa kwa klabu zetu? Na pia kwanini unachukia mafanikio ya wenzio? Hivi ungependa singano aende kagera sugar au ndanda akasotee mshahara?
 
Hahahahahahahahah mchezaji wa miaka 27 sio mchezaji wa majaaribio sio mchezaji wa kumuweka sawa kisaikolojia wala utimamu wa mwili ,27 years old ni mchezaji wa kwenda kuisaidia timu sio mchezaji wa majaribio wala Development.
Ko ulitaka singano asajiliwe timu gani?
 
Kwa uzi huu.... WITCH IS REAL
Tanganyika ndo inaongoza duniani kwa rohombaya,chuki na husda,ndio maana zile timu zao haziendelei miaka nenda rudi.
walishamfuta Singano kwenye ramani ya soka,
Mtu hata timu ya kitaani kwake hawezi kuombwa ushauri eti anasema TP mazembe wamechemka
 
Back
Top Bottom