Nani aliyemnyonga kamanda wa Polisi Zanzibar?

wasiojulikana wamevuka maji??
 
unataka kusemaje mkuu
 
Wazanzibari kwa majungu wapo vizuri
Huyo kamanda alikua mkuu wa idara ya maadhimisho,zanzibar
Kazi yake kupanga gwaride na wapufa matarumbeta wakati wa sherehe za kitaifa,
Hata kama aluchukua mke wa mtu tutaambiwa tu alipinga kukamatwa kwa uamsho,ili tu serekali ionekane imemuua
Serikali ina.njia nyingi za kummaliza mtu kama huyo bila ya kumuua ikiwemo kumpa u RAS kama chagonja au ubalozi kama Mangu
Acheni majungu,tunasubiri kuapishwa kwa maalim seif siyee
 
Zenji kwa majungu aisee ni mwisho kabisaa
 
Mtoa mada umemchafua sana marehemu, kwa maelezo hayo mafupi unamaanisha marehemu hakuwa na siffa yoyote ya kuwa askari bali alikuwa akitumika vibaya. Over
 
Taarifa hii ni ya kupuuzwa kwaa kiasi fulani.


Jamaa alijinyonga.hata familia inalijua hilo.

Kufungwa kamba ni jambo linasemekana tu ili kumtoa katika fedheha ya kujinyonga lakini ukweli hamna kamaba wala nini.

Mtu kama yule akamatwe afungwe kamba,akabwe alafu asipige kelele tu awe kimya tu..?

Kusema kwamba nyuma ya nyumba kulikuwa na hzo kama watu wanasisika wakikamata majani ni uongo tu wa kutaka kuwatoa watu kwenye reli kwamba jamaa alijinyonga.lakini inasemwa kwamba huwenda hicho kilichosikika ni ile purukubshani zake mwenyewe akijaribu kujinasua baada ya kujitundika na kupiga kelele ni ngumu hivyo lazima apapatike kwanza na hizo papara huwenda ndo walizosikia watu wakasema labda wavamizi

ALAMA za vidole zilizokutwa ni alama za vidole vyake mwenyewe ambayo alikuwa akijikamata kwa lengo la kujipapatua na kujitoa katika kitanzi baada ya kujitundika.

Ushahidi wote unaonesha kwamba alijinyonga,haiwezekani mtu kaama yule avamiwe alafu awe kimya tu uongo huo.

Sema wazanzibari kwa fitina siwawezi,wao kuitupia bara kila kitu sio ajabu sana.

sirro hakufika kwa sababu jamaa alijinyonga na kwamujibu wa jeshi mtu akijinyonga amedhalilisha jeshi na hastahiki kuzikwa kwa heshima.

Kwa chep chake jamaa sirro ilikuwa aje kabisa na timu maalum ya viongozi wa polisi wapige gwaride la heshima na timu hiyo iliandaliwa kabisa,lakini ilipothibitika kwamba kajinyonga mwenyewe kitu hicho kiliahirishwa moja kwa moja kutokana na kujinyonga kwakwe.

Viongozi waliokuja msibani walikuwa wao binafsi tu sio kiniaba ya kazi na chep cha marehemu,hyo ypte ni kutokana na kujinyonga kwake ni fedheha kwa jeshi na hata kidini pia aliyejinyonga ni kama kaua hvyo anakuwa kama kafanya uasi na anakosa baadhi ya stahiki zake.

Huwenda alirogwa mpaka ikapelekea kujinyonga,kama alirogwa basi dhambi ni za huyo aliyeroga.

Kama hakurogwa basi malipo yake yapo kwa Mola subhaana.
 
Wewe jamaa ni bonge la K
 
Niliwahi kusikia watu wanasema ADHABU YA MSALITI NDANI YA JESHI NI KUUWAWA

sijui ni kweli?
 
Wema hawana maisha! Apumzike kwa Amani!
Aliyeandika hii habari ameonesha kulikuwa na uhasimu huko huko visiwani, sioni anahusisha aje haya na ya bara. Kwa upande wa bara, kama ilivyo kwa visiwani, serikali zinatakiwa kufanya uchunguzi wa mauaji ya mwananchi na mtumishi huyu, iwekwe wazi na hatua zichukuliwe kwa watakaobainika kuhusika na udhalimu huu.
 
Awe uamsho au la, ni sheria gani unayoihusisha ambayo itakubaliana na yaliyomtokea marehemu? Kwamba kwa kuwa uamsho anastahili yaliyompata?
 
Mkuu jamaa hajauliwa inasemwa kajinyonga.

Angekuwa ameuliwa angezikwa kiheshima na mpama sirro angekuwepo pale.
 
Ni wapi huko kwa "wale ambao wametoka huko siku nyingi".

Maandiko yako yanaashiria una "inferiority complex".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…