Nani Aliruhusu CUF Lipumba Kufanya Doria Kutumia Walinzi wa Chama

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Kuwepo vikundi vya kiulinzi ndani ya vyama vya siasa ni dalili tosha huu ndio mwanzo wa kupotea kwa amani nchini,
Tumesikia msemaji wa CUF Lipumba akidai kuwa vijana wake walikuwa katika doria ya kawaida ndipo wakavamia mkutano wa CUF Maalin Sheif huko kinondoni. Je huyo msemaji alipata mamlaka wapi ya kuwa na kikosi cha ulinzi kilichovamia mkutano huo na kujeruhi watu.
Huu mgogoro huu wa ndani ya CUF isiwe ikaja kuwa na makundi ya vijana ndani ya vyama vya siasa wanaoweza kupigana wao kwa wao.
Vyombo vya usalama vichukue hatua za haraka kuzuia kwa vikundi hivi kuwepo la sivyo amani na kuvumiliana kisiasa inaweza kutoweka.
 
kuna kitu mamlaka inataka kitokee cuf kwa gharama yeyote nadhani,siro ashasema ni ushamba si uhalifu,kambaya bado yuko mtaani huku akijichanganya na maelezo ya kipuuzi na uongo.mara aseme vijana wa chadema,mara eti waliitiwa mwizi walipofika maeneo ya hotel hawakuingia ndani.haya yote yamefanyika na ushahidi upo dhahiri shahiri.inaumiza sana.
 
Kuwepo vikundi vya kiulinzi ndani ya vyama vya siasa ni dalili tosha huu ndio mwanzo wa kupotea kwa amani nchini,
Tumesikia msemaji wa CUF Lipumba akidai kuwa vijana wake walikuwa katika doria ya kawaida ndipo wakavamia mkutano wa CUF Maalin Sheif huko kinondoni.
Huu mgogoro huu wa ndani ya CUF isiwe ikaja kuwa na makundi ya vijana ndani ya vyama vya siasa wanaoweza kupigana wao kwa wao.
Vyombo vya usalama vichukue hatua za haraka kuzuia kwa vikundi hivi kuwepo la sivyo amani na kuvumiliana kisiasa inaweza kutoweka.

Bowie ungekuwa ni mgeni hapa jukwaani/nchini ningeona unachochangia hukijui lakini naona kama uko kiupotoshaji zaidi. Ni hivi iko wazi kabisa hicho kitendo kina baraka zote za ccm na serekali. Ni dhahiri mgogoro unaonendelea ndani ya Cuf unaratibiwa na serekali ya ccm dhidi ya Maalim Seif kutokana na kitendo chake cha kususia uchaguzi wa ZnZ baada ya kuporwa ushindi wake. Zinafanyika mbinu chafu za wazi na nyuma ya pazia ili kumvunja nguvu Maalim kwa kitendo chake cha kuicha nchi na hasa chama cha ccm dhidi ya wizi wa kura inaouendesha kila uchaguzi unapotekea.

Hapa unajaribu kuonyesha eti tatizo ni vikundi vya ulinzi kitu ambacho sio kweli. Inaeleweka kabisa kuwa Lipumba aliondoka kwenye chama tena kwa kususa hicho cheo baada ya makubaliano anayofahamu yeye kutoka ccm. Baada ya muda ikatokea yaliyotokea uchaguzi wa ZnZ, na kwa kuwa lengo la ccm halikutimia hasa huko ZnZ, ccm watakutumia udhaifu au kosa la Cuf kutoijadili barua ya kujiuzulu ya Lipumba kumrudisha ili aivuruge Cuf kwani tayari Lipumba hana uchungu tena na Cuf bali hela, na hilo lilidhihirika pindi alipojiuzulu tena kipindi muhimu cha uchaguzi. Hilo genge la Lipumba lilianza pindi alipovamia mkutano wa Cuf kulazimisha kurudi kwenye nafasi yake na serekali ikakaa kimya. Visa vingi vya wazi vimeendelezwa kwa mkono wa serekali kuihujumu Cuf iliyo chini ya Maalimu Seif, kama fedha za ruzuku kupewa Lipumba wakati hakushiriki kuleta hata kura moja kwa Cuf wakati wa uchaguzi. Hili unalosema eti sijui vikundi naona kama unapotosha kwa makusudi, katika kikao cha juzi kilichovamiwa ni kundi la Lipumba lililojipa mamlaka ya kulinda wakati wao sio polisi, cha ajabu hata magari yaliyotumika na wavamizi wa mkutano huo yapo kwenye ofisi za Cuf ya Lipumba na sio polisi kama inavyotarajiwa. Huyo muhuni aliyekamatwa na kujeruhiwa na wananchi baada ya kuvamia ana uhusiano wa karibu na Lipumba. Leo hii unamsikia Kambaya anakuja na maelezo ya kujichanganya eti ni vijana wa cdm toka Arusha huku magari ya uvamizi yako ofisi za Cuf!! Ameona utetezi ule umeleta sintofahamu anabadilisha maelezo eti walikuwa wanalinda mkutano wakapigiwa kelele za wezi. Picha zipo zikionyesha hilo kundi lao likipiga watu wa Cuf ya Maalim. Maajabu ya mwaka eti polisi wanataka Cuf ya Seif iliyofanyiwa uhuni wakae waelewane na Cuf ya Lipumba. Ajabu lingine la karne eti Sirro anasema walioonyesha bastola hadharani ni ushamba, na wala kwake sio jinai!!!

Nikushauri kama huna la kuchangia kaa kimya na sio kupotosha ukweli ulio wazi. Tuheshimiane kwani sisi ni watu wazima na wala sio watoto wa kuamini hicho ulichoandika hapo juu.
 
Hivi unajua cuf ilianzishwa Nani na yupo wapi ni wakati wa kusalitiana kama lipumba na seif walivyo mfanyia mapalala pale tanga mwaka nimesahau zambi ya usaliti haifi hata zito ipo siku chadema watajua walichomfanyia zito si sawa hata silaa kabla zito hawajamtuhuum nae alimuona msaliti yalipo mkuta na yeye akalala mbele tena akaenda mbali kuwa hataki siasa yuko wapi sasa hata mbowe kuna siku nae hatapitia kipindi hiki hivi mnakumbuka bunge la katiba tundu lisu alivyo ivuruga cuf mpaka cuf wakasema hatakaa akanyage zanzibar kichwa chake kitakuwa chao leo ni hero Zanzibar siasa ziaache tulishafiwa chama lakini niaaacheeeee nina mengi ngoja niachie hapa
 
Bowie ungekuwa ni mgeni hapa jukwaani/nchini ningeona unachochangia hukijui lakini naona kama uko kiupotoshaji zaidi. Ni hivi iko wazi kabisa hicho kitendo kina baraka zote za ccm na serekali. Ni dhahiri mgogoro unaonendelea ndani ya Cuf unaratibiwa na serekali ya ccm dhidi ya Maalim Seif kutokana na kitendo chake cha kususia uchaguzi wa ZnZ baada ya kuporwa ushindi wake. Zinafanyika mbinu chafu za wazi na nyuma ya pazia ili kumvunja nguvu Maalim kwa kitendo chake cha kuicha nchi na hasa chama cha ccm dhidi ya wizi wa kura inaouendesha kila uchaguzi unapotekea.

Hapa unajaribu kuonyesha eti tatizo ni vikundi vya ulinzi kitu ambacho sio kweli. Inaeleweka kabisa kuwa Lipumba aliondoka kwenye chama tena kwa kususa hicho cheo baada ya makubaliano anayofahamu yeye kutoka ccm. Baada ya muda ikatokea yaliyotokea uchaguzi wa ZnZ, na kwa kuwa lengo la ccm halikutimia hasa huko ZnZ, ccm watakutumia udhaifu au kosa la Cuf kutoijadili barua ya kujiuzulu ya Lipumba kumrudisha ili aivuruge Cuf kwani tayari Lipumba hana uchungu tena na Cuf bali hela, na hilo lilidhihirika pindi alipojiuzulu tena kipindi muhimu cha uchaguzi. Hilo genge la Lipumba lilianza pindi alipovamia mkutano wa Cuf kulazimisha kurudi kwenye nafasi yake na serekali ikakaa kimya. Visa vingi vya wazi vimeendelezwa kwa mkono wa serekali kuihujumu Cuf iliyo chini ya Maalimu Seif, kama fedha za ruzuku kupewa Lipumba wakati hakushiriki kuleta hata kura moja kwa Cuf wakati wa uchaguzi. Hili unalosema eti sijui vikundi naona kama unapotosha kwa makusudi, katika kikao cha juzi kilichovamiwa ni kundi la Lipumba lililojipa mamlaka ya kulinda wakati wao sio polisi, cha ajabu hata magari yaliyotumika na wavamizi wa mkutano huo yapo kwenye ofisi za Cuf ya Lipumba na sio polisi kama inavyotarajiwa. Huyo muhuni aliyekamatwa na kujeruhiwa na wananchi baada ya kuvamia ana uhusiano wa karibu na Lipumba. Leo hii unamsikia Kambaya anakuja na maelezo ya kujichanganya eti ni vijana wa cdm toka Arusha huku magari ya uvamizi yako ofisi za Cuf!! Ameona utetezi ule umeleta sintofahamu anabadilisha maelezo eti walikuwa wanalinda mkutano wakapigiwa kelele za wezi. Picha zipo zikionyesha hilo kundi lao likipiga watu wa Cuf ya Maalim. Maajabu ya mwaka eti polisi wanataka Cuf ya Seif iliyofanyiwa uhuni wakae waelewane na Cuf ya Lipumba. Ajabu lingine la karne eti Sirro anasema walioonyesha bastola hadharani ni ushamba, na wala kwake sio jinai!!!

Nikushauri kama huna la kuchangia kaa kimya na sio kupotosha ukweli ulio wazi. Tuheshimiane kwani sisi ni watu wazima na wala sio watoto wa kuamini hicho ulichoandika hapo juu.
Yaani mtu anakiri uhusika wake katika tukio kama lile halafu bado yuko mtaani?
 
Ajabu na kweli, halafu eti hapa utasema hakuna mkono wa serekali? Huku kamanda wa polisi anatoa maelezo eti kuonyesha bastola hadharani ni ushamba sio jinai!!!
 
Kuwepo vikundi vya kiulinzi ndani ya vyama vya siasa ni dalili tosha huu ndio mwanzo wa kupotea kwa amani nchini,
Tumesikia msemaji wa CUF Lipumba akidai kuwa vijana wake walikuwa katika doria ya kawaida ndipo wakavamia mkutano wa CUF Maalin Sheif huko kinondoni.
Huu mgogoro huu wa ndani ya CUF isiwe ikaja kuwa na makundi ya vijana ndani ya vyama vya siasa wanaoweza kupigana wao kwa wao.
Vyombo vya usalama vichukue hatua za haraka kuzuia kwa vikundi hivi kuwepo la sivyo amani na kuvumiliana kisiasa inaweza kutoweka.
Kichwa cha habari kiko tofauti na maelezo yako, nafikiri ungeishia kwenye swali (kichwa cha habari) ili upate majibu toka kwa wadau!
 
Bowie ungekuwa ni mgeni hapa jukwaani/nchini ningeona unachochangia hukijui lakini naona kama uko kiupotoshaji zaidi. Ni hivi iko wazi kabisa hicho kitendo kina baraka zote za ccm na serekali. Ni dhahiri mgogoro unaonendelea ndani ya Cuf unaratibiwa na serekali ya ccm dhidi ya Maalim Seif kutokana na kitendo chake cha kususia uchaguzi wa ZnZ baada ya kuporwa ushindi wake. Zinafanyika mbinu chafu za wazi na nyuma ya pazia ili kumvunja nguvu Maalim kwa kitendo chake cha kuicha nchi na hasa chama cha ccm dhidi ya wizi wa kura inaouendesha kila uchaguzi unapotekea.

Hapa unajaribu kuonyesha eti tatizo ni vikundi vya ulinzi kitu ambacho sio kweli. Inaeleweka kabisa kuwa Lipumba aliondoka kwenye chama tena kwa kususa hicho cheo baada ya makubaliano anayofahamu yeye kutoka ccm. Baada ya muda ikatokea yaliyotokea uchaguzi wa ZnZ, na kwa kuwa lengo la ccm halikutimia hasa huko ZnZ, ccm watakutumia udhaifu au kosa la Cuf kutoijadili barua ya kujiuzulu ya Lipumba kumrudisha ili aivuruge Cuf kwani tayari Lipumba hana uchungu tena na Cuf bali hela, na hilo lilidhihirika pindi alipojiuzulu tena kipindi muhimu cha uchaguzi. Hilo genge la Lipumba lilianza pindi alipovamia mkutano wa Cuf kulazimisha kurudi kwenye nafasi yake na serekali ikakaa kimya. Visa vingi vya wazi vimeendelezwa kwa mkono wa serekali kuihujumu Cuf iliyo chini ya Maalimu Seif, kama fedha za ruzuku kupewa Lipumba wakati hakushiriki kuleta hata kura moja kwa Cuf wakati wa uchaguzi. Hili unalosema eti sijui vikundi naona kama unapotosha kwa makusudi, katika kikao cha juzi kilichovamiwa ni kundi la Lipumba lililojipa mamlaka ya kulinda wakati wao sio polisi, cha ajabu hata magari yaliyotumika na wavamizi wa mkutano huo yapo kwenye ofisi za Cuf ya Lipumba na sio polisi kama inavyotarajiwa. Huyo muhuni aliyekamatwa na kujeruhiwa na wananchi baada ya kuvamia ana uhusiano wa karibu na Lipumba. Leo hii unamsikia Kambaya anakuja na maelezo ya kujichanganya eti ni vijana wa cdm toka Arusha huku magari ya uvamizi yako ofisi za Cuf!! Ameona utetezi ule umeleta sintofahamu anabadilisha maelezo eti walikuwa wanalinda mkutano wakapigiwa kelele za wezi. Picha zipo zikionyesha hilo kundi lao likipiga watu wa Cuf ya Maalim. Maajabu ya mwaka eti polisi wanataka Cuf ya Seif iliyofanyiwa uhuni wakae waelewane na Cuf ya Lipumba. Ajabu lingine la karne eti Sirro anasema walioonyesha bastola hadharani ni ushamba, na wala kwake sio jinai!!!

Nikushauri kama huna la kuchangia kaa kimya na sio kupotosha ukweli ulio wazi. Tuheshimiane kwani sisi ni watu wazima na wala sio watoto wa kuamini hicho ulichoandika hapo juu.
Unapotoa hoja unatumia lugha za kidoplomasia zaidi mie siko hapa kumtetea Lipumba wala CCM nimeuliza Nani aliruhusu hao wanaojiita walinzi wa Lipumba ruhusa ya kuvamia kikao hicho cha CUF kinondoni. In general lazima tuangalie masuala ya usalama wa nchi yetu kwanza badala ya kukimbilia mambo ya vyama. Kama kweli unavyotuhumu kwa maelezo yako one day justice will prevail.
 
DSC_0037.jpg

Green-Guard.jpg
Hivi vikundi ni hatari kwa amani, wao wanasema hawatoi mafunzo ya kijeshi bali ni mafunzo ya ukakamavu lakini wakikakamaa sana ipo siku wanaweza kulizidi nguvu jeshi la polisi. Bora vifutwe hela za vyama zipelekwe kwenye masuala ya maendeleo !
 
Unapotoa hoja unatumia lugha za kidoplomasia zaidi mie siko hapa kumtetea Lipumba wala CCM nimeuliza Nani aliruhusu hao wanaojiita walinzi wa Lipumba ruhusa ya kuvamia kikao hicho cha CUF kinondoni. In general lazima tuangalie masuala ya usalama wa nchi yetu kwanza badala ya kukimbilia mambo ya vyama. Kama kweli unavyotuhumu kwa maelezo yako one day justice will prevail.

Unauliza nani aliruhusu au unatania? Magari yaliyotumika kufanya uvamizi yako kwenye ofisi za Cuf huku yakiwa yamevunjwa vioo. Mmoja wa wavamizi amekiri alitumwa na Lipumba ama basi ni mtu wa karibu wa Lipumba. Hiyo tabia ya hilo kundi la Lipumba ni ngeni? Iweje kila anapokwenda Lipumba anapata ulinzi mkali wa polisi kitu ambacho sio kawaida kwa kiongozi wa upinzani? Unaweza ukatuambia hatua zozote zilizochukuliwa baada ya Lipumba kwenda kwenye kikao cha Cuf na kuvuruga mkutano mbali ya kufanya uharibu wa mali katika hotel ilikofanyikia mkutano? Ukiona mamlaka husika ziko kimya huku zikitoa lugha za utata basi huhitaji kumtafuta mchawi.
 
Back
Top Bottom